Tafakari Kuu ya Neno la Siku ya Leo

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Neno la leo linatoka katika kitabu Kitakatifu kilichoandikwa na nabii Yeremia 17: 5-8, nalo lasema hivi:-

5. Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
6. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
7. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.
8. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda

Mungu atubariki sana, tumtegemee yeye pekee. Tuwasahau waganga na waganguzi, wachawi, hirizi na vile vyote mwanadamu anavyovitegemea kwa nguvu zake mwenyewe.
 
...tumtegemee yeye pekee. Tuwasahau waganga na waganguzi, wachawi, hirizi na vile vyote mwanadamu anavyovitegemea kwa nguvu zake mwenyewe.

Kweli wachawi na hirizi hazifai kutegemea.

Je, na madaktari wa Amana hospitali tuwategemee tusiwategemee?
 
Mwinjilisti Luka Mtakataifu alikuwa ni daktari.
Kile ni karama au kipawa kutoka kwa Mungu mwenyewe.
Ila tiba ukianza kumbiwa mpaka umuue ndugu yako, hiyo mungu hataki.
wala hataki ufungwe chura mwilini ili akulinde na maadui zako.
 
Lakini daktari wangu wa Amana uliyeniruhusu nimtegemee alienda shule kusomea uganga kwa juhudi zake mwenyewe, hakushushiwa maono na upako usiku, isitoshe baada ya kazi huwa ni mzinifu aliyetopea. Huyu nae kwa nini ameshushiwa karama ya uponyaji mpaka ukubali nimtegemee?
 
Biblia ni mafundisho ya Mungu yaliyo tolewa kupitia wanaadamu na kila neno lilitolewa kwa kutegemea mahali, wakati, na aina ya watu. napia nivizuri kuutafsiri biblia kwa kusoma toka mwanzo wa habari unayo isoma ili upate maana kamili, wakati mwingine huwezi kutafsiri biblia kwa mstari mmoja tu. Inapo semwa amelaaniwa mtu yule amtegemea mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni mwake amemuacha Bwana. Ukristo upo kiroho zaidi kuliko kimwili, wakristo wanaamini ni Mungu pekee anaweza kutegemewa katika maisha yajayo ya milele na si mwanadamu, hii haimaanishi usimtegemee mwanadamu kabisa, hapana unaweza kumtegemea kwa mambo ya kimwili na kidunia zaidi ndio maana hata enzi hizo waganga walikuepo, hivyo kumtegemea mganga wako wa amana kwamaana ya kimwili sio dhambi, kumtegemea mwajiri wako sio dhambi nk lakini bila kwenda kinyume na maandiko matakatifu. mbarikiwe
 
dah big up sana naona sasa watu wanajua kuhusu biblia vp hata vifungu vidogo vidogo watu wanavijua sana imeenda shule bwana awabariki
:becky:
 
Biblia ni mafundisho ya Mungu yaliyo tolewa kupitia wanaadamu na kila neno lilitolewa kwa kutegemea mahali, wakati, na aina ya watu. napia nivizuri kuutafsiri biblia kwa kusoma toka mwanzo wa habari unayo isoma ili upate maana kamili, wakati mwingine huwezi kutafsiri biblia kwa mstari mmoja tu. Inapo semwa amelaaniwa mtu yule amtegemea mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni mwake amemuacha Bwana. Ukristo upo kiroho zaidi kuliko kimwili, wakristo wanaamini ni Mungu pekee anaweza kutegemewa katika maisha yajayo ya milele na si mwanadamu, hii haimaanishi usimtegemee mwanadamu kabisa, hapana unaweza kumtegemea kwa mambo ya kimwili na kidunia zaidi ndio maana hata enzi hizo waganga walikuepo, hivyo kumtegemea mganga wako wa amana kwamaana ya kimwili sio dhambi, kumtegemea mwajiri wako sio dhambi nk lakini bila kwenda kinyume na maandiko matakatifu. mbarikiwe

Imani hiyo unayoizungumza wengine (wenye Dini) hawana kabisa, lakini pamoja na hekima na imani aliyokuwa nayo Paulo, ilifikia point akamwambia Timoteo kuwa atumie Mvinyo kwa matatizo ya tumbo aliyokuwa nayo, lakini kwa imamni za hao ninaowasema ni lazima wangesema ni pepo tu na liombewe
 
Mkuu unadhani wakati huo watu walikua hawaumwi, watu walikua wanaumwa na walikua wanatumia dawa za wakat huo, kwahiyo kama huo mvinyo ndio dawa ilikuwa sahihi kwake kutumia,haijawahi kutamkwa wala kutokea kuna siku watu wasiende katika matibabu eti kwasababu yoyote ile,mungu ametuoa maarifa tuweze kujisaidia ikiwemo madawa, l
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom