Jisamehe, Ruhusu yaliyopita yapite

Jisamehe, Ruhusu yaliyopita yapite

Kibenje KK

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2016
Posts
284
Reaction score
442
Kuna Mama Mmoja Baada ya kuwa anafatilia sana Masomo yangu Mtandaoni na Kwenye Tv & redio siku moja akaniomba Namba Inbox kisha kuomba Tuonane, nilimuuliza maswali kadhaa kisha nikakubali tuonane, Nakumbuka aliomba kunitoa lunch kwenye Hotel moja nzuri.

Wakati tunapata lunch tulianza mazungumzo.

Kwanza akanipongeza na kuniambia ananifatilia sana, kila siku lazima apitie kwenye kurasa zangu kusoma.

Huku akilia kaniambia Kuwa kwa Sasa ameolewa na Mzungu na anaishi Uingereza na Tayari ana watoto naye wawili lakini jumla ana watoto watano, watatu aliwazaa na wanaume watatu tofauti kabla hajakutana na Huyo mzungu. Anasema pamoja na kuwa Kwenye Ndoa na mzungu huyo kwa miaka Sita na japokuwa mzungu huyo anampa kila kitu anachokihitaji lakini hajawahi kufurahia maisha.

Anasema kila siku mara huwa anakumbuka mambo aliyokuwa akifanya nyuma, wanaume ambao alikwisha lala nao, wengine alikua akiwaibia, anakumbuka aliwahi kutoa Mimba kadhaa,ulevi, anakumbuka mwanaume aliyempenda sana na kumuacha bila sababu. Akawa anajihukumu anasema japokuwa ana kila kitu sasa hivi lakini hafurahii maisha.

Nikamwambia, "Furaha inatengenezwa na wewe mwenyewe" HAUWEZI KURUDI NYUMA NA KUBADILISHA HISTORIA YAKO MBAYA lakini unaweza kutengeneza kesho nzuri kuanzia.

Watu wengi wanashindwa kusonga mbele sababu hawajajisamehe dhambi na makosa waliowahi kufanya nyuma, kila siku unajihukumu mwisho unashindwa kufanya lolote kwenye maisha sababu ya kujihukumu.

Ukitubu Mungu anakusamehe, hakikisha na wewe unajisamehe. Mtume Paulo alikua Muuaji lakini Mungu alimtuma kuhubiri neno lake, Musa aliua lakini Mungu alimtumia kupelekea wana wa israel nchi ya Ahadi.

Mungu anasamehe na kusahau. Jisamehe pia na sahau, usikubali kubeba makosa na madhambi ya nyuma mwaka 2021.
Kubeba mambo mabaya ya zamani ni kama kushikilia kaa la moto litakalokuunguza na kukuumiza kama ukiendelea kulishikilia. Ni bora uliachie ili uwe na furaha.

Instagram 👉kelvinkibenje
 
Hivi jamani hawa wanawake wana nini hasa eti !!!

Utasikia Nina miaka 5 naye ila sina furaha hata kidogo"
 
Wewe kajamaa kadogo labda upate ushauri kutoka kwa mama D

Ndoa za hivyo zipo nyingi sana. Na Kati ya hizo nyingi unakuta mtu ameoana na mtu sababu ya upweke, kulipiza kisasi, kupata umaarufu na kupunguza ngumu wa maisha. Niliwahi kumsikia mama mmoja mtu mzima mwenye zaidi ya miaka48 anasema

Namnukuu "Yaani Mimi nikiwa na mume wangu huwa sipati hisia yoyote, mara nyingi huwa najaribu kufunga macho na kuvuta hisia niko na (akataja mchepuko wake) ili nihisi kitu vinginevyo namuonaga anakukuruka tuu......"

Na hapa jukwaani pia tumewasikia wanaume wakisema wake zao baada ya ndoa hawawavitii ndani, ndoani kunakua hakuna flavor kwa hiyo wanazifuata kwa michepuko. Tofauti Kati ya kuchepuka kwa mwanamke na mwanaume ni moja. Mwanaume ambaye yuko vizuri kiafya na kiuchumi ana uwezo wa kubalance na kumiliki mwanamke zaidi ya mmoja; lakini Mwanamke akianza kuchepuka anahamisha moyo, akili na mwili moja kwa moja anahamishia kule alikonogewa.

Mungu utusaidie viumbe wake kuweza kuishi na tunaowependa kwanza na kujenga maisha tunayoyatamani

Kuhani Noah Jasmoni Tegga Ushimen Extrovert mrangi
 
Tatizo watu hawataki kukua wanawaza ya utotoni yaani yaliyopita..

Wengine eti schhol mate au monitor wa darasaa alikuwa ex hao ni watu wasiotaka kusonga mbele kiakili ila kimwili wana mvi kbsa.

Mimi mtu nikishamsikia anasema enzi zangu shule ya msingi nlikuwa handsome / beautiful huwa namzarau sana,,,, watu wa ivo hawanaga mawazo mapya,,,.

Mimi tukiwa na wewe nawaza tutakomaaje mbele,,, sio nilikotoka.
 
Tatizo watu hawataki kukua wanawaza ya utotoni yaani yaliyopita..

Wengine eti schhol mate au monitor wa darasaa alikuwa ex hao ni watu wasiotaka kusonga mbele kiakili ila kimwili sana mvi kbsa.

Mimi tukiwa na wewe nawaza tutakomaaje mbele,,, sio nilikotoka.

Ukiwa kwenye mshusiano kuachana inaweza kuwakuwa kosa, lakini kuuishi bila furaha na kuishia kucheat ni kosa pia na zaidi ni kujikosea nafsi zaidi

Ifike mahala watu wachague kuacha moja na kushika moja
 
Kuachana inatokea na haikwepeki ila kucheat tunao uwezo wa kuacha kucheat na tukaimarisha mahusiano yetu,,, shida tu unapowaza ya nyuma
 
Ndoa za hivyo zipo nyingi sana. Na Kati ya hizo nyingi unakuta mtu ameoana na mtu sababu ya upweke, kulipiza kisasi, kupata umaarufu na kupunguza ngumu wa maisha. Niliwahi kumsikia mama mmoja mtu mzima mwenye zaidi ya miaka48 anasema

Namnukuu "Yaani Mimi nikiwa na mume wangu huwa sipati hisia yoyote, mara nyingi huwa najaribu kufunga macho na kuvuta hisia niko na (akataja mchepuko wake) ili nihisi kitu vinginevyo namuonaga anakukuruka tuu......"

Na hapa jukwaani pia tumewasikia wanaume wakisema wake zao baada ya ndoa hawawavitii ndani, ndoani kunakua hakuna flavor kwa hiyo wanazifuata kwa michepuko. Tofauti Kati ya kuchepuka kwa mwanamke na mwanaume ni moja. Mwanaume ambaye yuko vizuri kiafya na kiuchumi ana uwezo wa kubalance na kumiliki mwanamke zaidi ya mmoja; lakini Mwanamke akianza kuchepuka anahamisha moyo, akili na mwili moja kwa moja anahamishia kule alikonogewa.

Mungu utusaidie viumbe wake kuweza kuishi na tunaowependa kwanza na kujenga maisha tunayoyatamani

Kuhani Noah Jasmoni Tegga Ushimen Extrovert mrangi
We ungekuwa hauko katika pingu ningekukwibilia mbali 😝😍 bahati yako tu
 
Hahahaaa akili za extrovert wanazijua mwenyewe.
Sasa ukapate kitubio maana ushatenda dhambi..... " Usitamani mwanamke asiye mke wako"
 
Samtaimu haina jinsi 😋 wanasemaga wanawake wazuri wako kwa watu so tuliobaki ni kugombania nafasi kwenye mahusiano yaliyo legalega
 
Tatizo kubwa hapo wanawake wanachaguliwa hawachagui, lkn wanawake wangekuwa wanachagua hii dunia ingekuwa powa sana.
Matokeo yake mwanamke anaangukia popote bila kutegemea kasheshe ndiyo inapoanza.
 
Ndoa za hivyo zipo nyingi sana. Na Kati ya hizo nyingi unakuta mtu ameoana na mtu sababu ya upweke, kulipiza kisasi, kupata umaarufu na kupunguza ngumu wa maisha. Niliwahi kumsikia mama mmoja mtu mzima mwenye zaidi ya miaka48 anasema

Namnukuu "Yaani Mimi nikiwa na mume wangu huwa sipati hisia yoyote, mara nyingi huwa najaribu kufunga macho na kuvuta hisia niko na (akataja mchepuko wake) ili nihisi kitu vinginevyo namuonaga anakukuruka tuu......"

Na hapa jukwaani pia tumewasikia wanaume wakisema wake zao baada ya ndoa hawawavitii ndani, ndoani kunakua hakuna flavor kwa hiyo wanazifuata kwa michepuko. Tofauti Kati ya kuchepuka kwa mwanamke na mwanaume ni moja. Mwanaume ambaye yuko vizuri kiafya na kiuchumi ana uwezo wa kubalance na kumiliki mwanamke zaidi ya mmoja; lakini Mwanamke akianza kuchepuka anahamisha moyo, akili na mwili moja kwa moja anahamishia kule alikonogewa.

Mungu utusaidie viumbe wake kuweza kuishi na tunaowependa kwanza na kujenga maisha tunayoyatamani

Kuhani Noah Jasmoni Tegga Ushimen Extrovert mrangi
Kuna vitu kwenye maisha vinahitaji msimamo na uamuzi usiyo yumba. Ila kama utataka kila kitu kiwe unavyotaka ni ngumu.. Mengine unaacha hekima ya Mungu iingilie kati kabla ya uharibifu zaidi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom