Jirani yangu simwelewi

Jezebel

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2016
Posts
218
Reaction score
432
Nashindwa kumuelewa jirani yangu na ananifanya nisiwe comfortable.... Nyumba ninayoishi tupo watano kila mtu na kwake anaijtegemea wote ni vijana na hakuna mwenye familia. Tupo wadada wawili tu. Huyu dada jirani yangu alinikuta wakati akihamia hapo na mwanzoni alipata matatizo nikamsaidia kama kama ambavyo ningemsaidia binadamu yoyote. Aliumwa na hakuwa na ndugu karibu (kwao Shinyanga) hivyo nilimhudumia kwa ukarimu wote nilimpikia, na kumsaidia kufanya usafi hadi alipopata nafuu.

Baada ya kupona maisha yaliendelea japo hatukua na ukaribu zaidi ya salamu na mambo basic kama kushare bills. Kumbuka sisi ni vijana na pretty much ndio tumeanza kujitegema so hatujajiestablish kihiivyo...ila nimegundua huyu jirani yangu ni kama anawivu ama sijui ni kitu gani. Alipokuja kwangu kila alichokiona alitaka kujua ni menunua bei gani na vingine alidiriki kuniuliza umenunuliwa na mpenzi wako? Sikumbuki nilipotezeaje coz sionagi kama ni sawa ku disclose mambo yangu binafsi kwa mtu ambae sio wa karibu.

Ila naona ni kama tabia kila tukionana akiona nimebadilisha style atauliza umesuka bei gani, juzi kaniona na simu kaniuliza mbona hujanionyesha kitu kipya. yani hata nikinunua maybe kiblouse kipya lazima atauliza. Kinachonimaliza ni kwamba hata kama niko ndani napika ataongea from her room eeeeh jirani leo unapika samaki au leo unapika kitu flani? Hua namjibu kwa maneno machache tu.

Bottom line ni kwamba she makes me uncomfortable!!!!!!! Yani very uncomfortable!!!!! Akiona mpenzi wangu wangu yupo ndani atakuja kunigongea either aombe kitunguu au kibiriti.

Nisaidieni jirani wa hivi naishije nae?????
 
ninavyoona tatizo lipo kwako. hauna mazoea na watu.. huyo ni jiran ako.. so inabd umzoee maan nilivyoelewa yy anajitahd kwa hali na mali kukuzoea. anyways mwekee boundaries kwa kumwelezea anavozengua. tumeumbwa na kukulia katika mazingira tofauti so usishangae yy kuwa hivo. hajui kama anakukera.
 
Watu wa aina hii wapo sana. Wazoee tu. Ukute hakuna zaidi ya admiring tu.

Kuna kina dada flani hivi tunafanya kazi eneo moja. Kila mara wananiuliza nani ananisafishia viatu, nanunua wapi nguo, yadda yadda yadda. Mwingine aliomba shati nililovaa nikajua utani, bwana we.... niliishia kumpa tu.
 
Nakusubiri urudi
 
Mi nimechoka yani,saiv nikirudi kwangu as long as nimelipa bills na sina cha kuongea na mtu najifungia ndani kwangu. Naonaga ni bora kukeep distance na mtu mkaheshimiana kwa kwa mbali kuliko kuzoeana mkakwazana kirahisi over vitu visivyo na msingi.
 
Wapo wengi sanaa design hyo.....inaboa sanaa. Mjibu kwa shortcuts...try as much as u can not to have conversations wit her.

Inakera sanaa nimepitia hyo experience pia. Ni wivu tu nuthn else. Anajaribu kukufaham/kukuzoea kinguvu. Dnt allow that (Dnt be too soft, at tyms sting like a bee if u can)

Acha tu, watu hata akijua umekula nnje au kurudi na take away home ni shida sanaaa...majungu ++. U find niggas all over ur neck wanting to know how u make ur money nd all. Aaargh nilikuja kuhama tu.

Tip:
Ukipanga jaribu tafuta nyumba watu either waliokuzidi mafanikio au ur age mates whom u have much in common. Always hata ukiwa unajipikia iwe inside ur block. Kuna mazingira flan ya nyumba ukiyaona tu unajua hapa life linaenda fresh.
 
Huwezi kuchagua jirani wala ndugu, utachagua mke / mpenzi basi.... mvumilie hadi hapo utakapojenga yako nyumba. Upangaji kero .. hiyo tisa kumi utakutana na maudhi ya mwenye nyumba ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…