Marcy
JF-Expert Member
- Aug 12, 2013
- 1,740
- 4,107
Kama mjuavyo, viwanja ambavyo havijapimwa huwa havina barabara, hivyo ili kupata njia, inabidi busara zitumike. Mimi, kwa kiherehere changu, nikamega sehemu kidogo ya kiwanja changu kwa mbele ili kupata barabara ya kupita gari na watu wa nyuma yangu waweze kuitumia.
Jirani niliyepakana naye upande wa pili wa hiyo barabara niliyotoa ndiye pasua kichwa. Kwa sasa anasema yeye ndiye aliyetoa barabara na ni sehemu ya eneo lake, hivyo ninapaswa kurudi nyuma hatua moja na nusu.
Nikaamua kuweka ukuta kuepusha mgogoro naye, lakini bado anataka ukuta wangu uvunjwe. Anadai nimejenga barabarani. Wenyeviti wote wapo upande wake, wakidai nimejenga barabarani. Ninapowaambia kuwa barabara ni sehemu ya eneo langu na jirani ndiye anayepaswa kurudi hatua kadhaa nyuma ili barabara iwe pana, hawanielewi na wamenikomalia. Jirani ana lugha isiyofaa, si mstaarabu, anatumia nguvu na mabavu ili nivunje ukuta.
Nimewaza kufunga kabisa hiyo barabara, ila nawaza majirani wa nyuma yangu watapita wapi. Naomba mnisaidie namna ya kushughulika na mtu wa namna hii maana wenyeviti wote wapo upande wake, nahisi wamepewa mlungula ili waikandamize haki yangu. Nimewaambia sitaki usumbufu na sijajenga ukuta kwenye eneo la mtu.