Jirani yangu humpiga mkewe kila kukichwa. Nifanyeje?

Ushauri wangu ni kweli mambo ya ndoa za watu hayatuhusu ila huyo anayepigwa ni binadamu mwenzetu, hivyo toa taarifa kwenye vyombo husika tutokomeze unyanyasaji wa kijinsia
 
Yaani anapenda tu kumuonea pasi na sababu. Yaani akifika tu malangoni, mtaa wote unafugumiza harufu ya pombe bila kusahau maneno machafu machafu

Akiingia ndani anamkunyuga mateke na makofi ya kila rangi bila huruma. Inauma sana wakuu. Binti wa watu alikuwa na kasura kake soft soft, kwa sasa kuna alama ya kisu shavuni. Yaani nowdays anatembea kwa kuchechemea

Mkewe ana tabia nzuri tu maskini. Nikikosa mboga huwa namuomba ananigea kidogo nalia kiugali changu. Dah!

Naumia moyo. Nianzie mahakama ipi wakuu?
Mripoti kwa mama Dorothy gwajima
 
Unaweza kumshauri aende kutoa taarifa kwa viongozi wa mtaa au dawati la jinsia inaweza kumfanya jamaa akapunguza kichapo.
 
Huyo nampa hata hela akihitaji aende kwao, kupiga mtu mzima mnaotofautiana miaka miwili au mitatu siyo ujanja. Huu ni ulimbukeni, tubadilike kama umeshindwana nae mpe ruhusa aende kwao lakini siyo kumpiga kila siku
 
NIkikumbuka namna marehemu babangu alimtesa marehemu mama kwa vipigo kisa ulevi huniuma sana nikiona kuna watu wanaendekeza huo upuzi hadi leo, inapaswa mwanaume upigwe kama wewe mtu wa hivi.
 
Bado JF ina watu wapumbavu sana aisee. Nyie mnaosema asiingilie mambo ya watu hata kwa kutoa tu taarifa serikali ya mtaa/dawati la jinsia ni wapumbavu mno. Mlichoweza kujikomboa ni kununua tu smartphone ila akili zenu bado za kikoloni. Mleta uzi fanya mambo mawili muhimu;
1. Acha kugongea kitoweo kwa huyo mke wa mtu. Pambana na shida zako. Mtoto wa kiume kula ugali chumvi kuliko kugongea kitoweo kwa mke wa mtu.
2. Toa taarifa serikali ya mtaa au dawati la jinsia ili wao wamsaidie huyo mwanamke bila wewe kujiingiza direct.
 
NIkikumbuka namna marehemu babangu alimtesa marehemu mama kwa vipigo kisa ulevi huniuma sana nikiona kuna watu wanaendekeza huo upuzi hadi leo, inapaswa mwanaume upigwe kama wewe mtu wa hivi.
Pole sana mkuu. Mimi mzee wangu yuko hai ila kiukweli mahusiano yetu sio mazuri sana ni basi tu siku zinaenda... sababu mojawapo ni hilo suala la vipigo kwa mama. Huku ukubwani nilijiuliza swali gumu sana kwamba hata kama kwa mfano mama alikuwa anachiti bado hakukuwa na uhalali wa kutoa vipigo kiasi kile mbele ya watoto wake. Kina baba wengi wa kiafrika hawapendwi na watoto wao kwasababu ya manyanyaso watoto waliyoyashuhudia utotoni. Zile kumbukumbu huwa mbaya sana na hazifutiki. Binafsi kuna mama fulani alishawahi kuhusika kumnyanyasa mama yangu enzi nikiwa primary hadi leo sijasamehe ingawa yeye na mama walishamaliza tofauti zao. Mama kanisihi niachane na hilo suala ila mimi nimemjibu hili suala ni personal sana.
 
Yaani anapenda tu kumuonea pasi na sababu. Yaani akifika tu malangoni, mtaa wote unafugumiza harufu ya pombe bila kusahau maneno machafu machafu

Akiingia ndani anamkunyuga mateke na makofi ya kila rangi bila huruma. Inauma sana wakuu. Binti wa watu alikuwa na kasura kake soft soft, kwa sasa kuna alama ya kisu shavuni. Yaani nowdays anatembea kwa kuchechemea

Mkewe ana tabia nzuri tu maskini. Nikikosa mboga huwa namuomba ananigea kidogo nalia kiugali changu. Dah!

Naumia moyo. Nianzie mahakama ipi wakuu?
Wewe shida yako siyo kupigwa kwa hiyo pisi kali, bali unaogopa kukosa pa kuhemea pindi huyo demu akirudishwa kwa muumba wake.
 
Yaani anapenda tu kumuonea pasi na sababu. Yaani akifika tu malangoni, mtaa wote unafugumiza harufu ya pombe bila kusahau maneno machafu machafu

Akiingia ndani anamkunyuga mateke na makofi ya kila rangi bila huruma. Inauma sana wakuu. Binti wa watu alikuwa na kasura kake soft soft, kwa sasa kuna alama ya kisu shavuni. Yaani nowdays anatembea kwa kuchechemea

Mkewe ana tabia nzuri tu maskini. Nikikosa mboga huwa namuomba ananigea kidogo nalia kiugali changu. Dah!

Naumia moyo. Nianzie mahakama ipi wakuu?
Na Wewe anza kuwa na Ratiba ya Kumpiga Mkeo ili uone raha aayoipata huyo Jirani yako. Na unaonekan ni Mtu mmbeya sana hapo Kitaani Kwenu.
 
Anachokifanya mleta mada sio umbea, yaani ni ujinga sana kumpiga piga mkeo na kusababisha usumbufu kwa majirani, kwanza mtu wa hivyo akiwa na ujirani na mimi nitamtafutia ugomvi kiana tudundane ili ahisi inavyokua unapopambana na mwanaume.
 
Back
Top Bottom