Jirani wa ajabu huyu

mamkuu5

JF-Expert Member
Nov 24, 2014
1,139
716
Salaam wanajamii wenzangu,mwenzenu ninajirani angu najitahidi kumuelewa ila mh ngumu sasa.

Akipata matatizo hasa yakuugua kuuguliwa hasemi kama anamatatizo unayasikia kwa watu basi kwaaibu kwasababu ulionao wanasema pole nawewe unasema pole,lakini habari zetu tukiamua kukaa kimya atakuja mpaka kuuliza kinachoendelea kama sio yeye hata basi mumewe atakuja!

Nimekua najiuliza mwanzoni alikua anasema tunasaidiana fresh tu ,tena ukizingatia hana wazazi wala ndugu wakaribu hapa mjini,ila gafla akaacha kabisa na sometimes anatukana watoto wangu na kuwakoromea ikabidi niwazuie hata kucheza kwake.

Najiuliza ni Mungu anaamua kudhihirisha tofauti zetu au kaingiwa nini?hatujawahi kumuacha akiwa na shida tatizo ninini?anaongea na mumewangu anajichekesha kweli ila mimi hata akiniona anakimbia mara nyingine,jana asubuh alimsalimia mumewangu,mume wangu akamjibu mbona mke wangu humsalimii?mimi ni mwema sana kwako kuliko mkewangu au unalipi jingine?akakimbilia ndani leo hajarudia tena na tulipomsalimu hakujibu.

Nafikiria kuachana nae kabisa hata kumsalimia maana hajibu,ntakua nakosea?
 
jina lako linaonesha wewe ni tatizo kwa kuwa nimepata one side story sishauri

hapa sio polisi ambapo atakayewahi ndio mwenye haki
 
Wewe ni jipu, punguza kumsengenya na kumsema vibaya jirani yako...huna chochote ninyi ndo.mnaosumbua mitaani watu hawanywi maji...dhibiti mdomo uone kama hatakuheshimu...we kutwa kumsengenya jirani yako, acha tabia hiyo, umemaliza mtaani sasa unatuletea umbeya wako jf, unastahili kupigwa ban usichafue jukwaa kwa umbeya....
 
Salaam wanajamii wenzangu,mwenzenu ninajirani angu najitahidi kumuelewa ila mh ngumu sasa.

Akipata matatizo hasa yakuugua kuuguliwa hasemi kama anamatatizo unayasikia kwa watu basi kwaaibu kwasababu ulionao wanasema pole nawewe unasema pole,lakini habari zetu tukiamua kukaa kimya atakuja mpaka kuuliza kinachoendelea kama sio yeye hata basi mumewe atakuja!

Nimekua najiuliza mwanzoni alikua anasema tunasaidiana fresh tu ,tena ukizingatia hana wazazi wala ndugu wakaribu hapa mjini,ila gafla akaacha kabisa na sometimes anatukana watoto wangu na kuwakoromea ikabidi niwazuie hata kucheza kwake.

Najiuliza ni Mungu anaamua kudhihirisha tofauti zetu au kaingiwa nini?hatujawahi kumuacha akiwa na shida tatizo ninini?anaongea na mumewangu anajichekesha kweli ila mimi hata akiniona anakimbia mara nyingine,jana asubuh alimsalimia mumewangu,mume wangu akamjibu mbona mke wangu humsalimii?mimi ni mwema sana kwako kuliko mkewangu au unalipi jingine?akakimbilia ndani leo hajarudia tena na tulipomsalimu hakujibu.

Nafikiria kuachana nae kabisa hata kumsalimia maana hajibu,ntakua nakosea?
Mimi nakushauri waiteni yeye na mmewe muongee nao ili kujua kinachowakabili
 
aiseee una mume bora kumchana live 'mume wangu akamjibu mbona mke wangu humsalimii?mimi ni mwema sana kwako kuliko mkewangu au unalipi jingine?' Harudii tena
 
Wewe ni jipu, punguza kumsengenya na kumsema vibaya jirani yako...huna chochote ninyi ndo.mnaosumbua mitaani watu hawanywi maji...dhibiti mdomo uone kama hatakuheshimu...we kutwa kumsengenya jirani yako, acha tabia hiyo, umemaliza mtaani sasa unatuletea umbeya wako jf, unastahili kupigwa ban usichafue jukwaa kwa umbeya....
Kumsengenyaje kwa mfano?
 
Pia nimemsemaje wakati haongei na mimi?atasikiaje mdomo wangu ukifunguka?best uweunafikiria kwanza au uwe unasoma vizuri,kukurupuka huku utakuja tukana wakwe punguza ujuaji
 
"Hapo uliposema ananijichekesha kwa mumeo na kuongea naye" ndo chanzo cha kuanzisha thread, zingine umejazia tu. "WIVU wa kimapenzi ni HATARI kwa afya yako."
 
Mara kadhaa kwenye thread mbali mbali umekua ukikwazana na wana JF hasa pele mnapotofautiana mitazamo, labda ww ndo mwenye matatizo...

Na suala la malezi kwa watoto kibongo hata jirani ana wajibu wa kumkanya mtoto pale anapokosea, kuna jirani yetu mmoja ctamsahau amenicharaza sana kila aliponikuta na makosa but it was for my own good.
 
Hii dunia kuna changamoto mingi mno mtu akikataa ujamaa na wewe kwanini wewe utake ujamaa nae...tena mi naona amenipunguzia mzigo maadam moyoni mwangu na amani kwamba hakuna nilchomfanyia yaani namfungia vioo mara dufu mpaka siku akiona yafaa tuzungumze tena akianza mi sina shida na sintomuuliza ilikuwaje ukiwa unanichunia...Hapana asee...Take ur time na mimi nachukua zangu...
 
huenda kapata maneno ya wachochez toka kwa majirani wachonganishi. na pia sijafahamu huyo asiyekusalimu na mume au mke . lakini pia kama wewe ni mtu wa dini sana na kusali huenda yeye ana mambo ya ushirikina pengine akijaribu kukuchezea wewe anashindwa hivyo anakuchukia na nafsi inamsuta. lakini kwa hali hiyo nakushauri jitengeni nae maana anaweza kuwadhuru watoto wenu, mtu ambaye hakusalimii na alishawahi kuwafokea watoto si ajabu akawawekea sumu ama akawafanya chochote. nina imani kubwa sana jirani atakuwa na ushirikina na kwako amedunda, simuhukumu ila tabia inashtua. endeleeni kumtumaini Mungu karibisheni viongozi wenu wa dini kwa mujibu ya imani ili wawe wanawaombea. pia jaribu kushirikisha majirani ambao pengine watakuwa nao wameona matendo yake kadhaa au wanajua chochote kuhusu huyo mtu.
 
“I don’t know the key to success, but the key to failure is trying to please everybody.”
Bill Cosby
Nimekuelewa.sana mkuu,umebadilisha fikra na mtazamo wangu,umenisaidia kujua mpaka wangu kwa kuishi na watu,asante hata mama yangu hajawahi niambia hili,ubarikiwe sana na Mungu akutane na haja za moto wako
 
Inaonesha kama familia yenu ndiyo tatizo; hii ya kufikia kusema ni kwanini unamsalimia mume wangu haijakaa vizuri; nyie ni vizabizabina hamueleweki, mwacheni mama wa watu akomae na maisha yake.
 
Back
Top Bottom