Jirani mkorofi: Je unawezaje kuishi naye…?

Jirani mkorofi: Je unawezaje kuishi naye…?

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
DSC_5287.JPG

Kuna wakati unaweza kulazimika kuhama nyumba kutokana na maudhi....

Majumbani mwetu ni eneo muhimu sana kwetu, kwani kuna dhima nyingi sana ambazo zinakamilishwa majumbani mwetu katika kutufanya tuzidi kusonga mbele kimaisha. Kuna methali ambayo inasema, "Ngombe anapoumia malishoni hukimbilia zizini." Hii ina maana nyingi , lakini moja inahusu nyumbani.

Tunaweza kupambana na kisirani kikubwa kwenye shughuli zetu za kila siku, tukajikuta tunalazimika kurejea nyumbani kwa ajili ya kupata amani. Kuna wakati majumbani mwetu kuna amani lakini jirani au jirani zetu ni kisirani kikubwa. Imeshatokea watu wakauza nyumba zao au kuhama nyumba walizopanga, kwa ajili ya kuwakimbia jirani wakorofi.

Jirani anaweza kuwa mkorofi kwa njia mbaimbali. Anaweza kuwa ni mwenye maneno yasiyoisha, anaweza kuwa mgomvi, anaweza kuwa mbea, anaweza kuwa mdokozi sana, anaweza kuwa ni mkosefu mkubwa wa adabu au vinginevyo.

Kuna wakati mimi mwenyewe nilikuwa na jirani ambao tulikuwa tunachangia nyumba. Kwa kweli, watu hawa, mtu na mumewe na watoto walikuwa ni walevi sana. Kila siku usiku na hata mchana walikuwa kwenye vita moja au nyingine. Kuna wakati tulikuwa tunashindwa hata kulala usiku kucha.

Kwa kweli ningekuwa naweza kuhama ningehama haraka sana, lakini sikuwa na uwezo huo. Hivyo ilibidi nijitahidi kutafuta njia au mbinu ya kuishi. Ukweli ni kwamba niliweza kufanikiwa kwa mbinu hizo kumudu kuishi.

Sikufundishwa au kusoma mahali mbinu hizo, bali nilizibuni mwenyewe. Kama una jirani mkorofi au kama utakuja kuwa na jirani mkorofi, naomba utumie mbinu hizi, kwani naamini zitakusaidia.

Jambo la kwanza nililofanya ni kubainisha kile wanachofafanya, yaani ukorofi wao. Jambo la pili nikabainisha wakati ambapo wanafanya ukorofi huo, na tatu nikabainisha namna wanavyofanya. Niliandika kabisa kila kitu, kwa mfano muda gani wanafungua mziki kama vile kuna shereha, wakati gani na kwa namna gani wanapigana, ni nani na nani wanapigana zaidi na mengine.

Nilibaini kwenye baadhi ya vitendo vyao, yale ambayo ni kinyume na sheria za nchi na yale ambayo yanakera, lakini siyo kinyume na sheria. Nilibainisha hivyo ili kuona kama itanilazimu nisaidiwe na vyombo vya dola kutafuta suluhu.

Halafu nilirejea kwangu mwenyewe. Nilijiuliza kuhusu kama mimi mwenyewe huwa sivunji taratibu ambazo kwa kawaida zingepaswa kuwakera jirani zangu. Lakini, nilijiuliza kama siyo tu mazingira ya kazi yangu ndiyo chanzo cha kuona
nakerwa? Nilikuwa napenda sana kufanya kazi za kuandika usiku, kwani mchana nilikuwa nafanya kazi za uwandani zaidi(field)

Kwa mfano, mtu anaweza kudhani jirani zake wanamsumbua sana kwa sababu, amegeuza nyumbani kwake ni mahali kwa kusalia au kufanyia tahajudi. Hivyo kelele kidogo tu, anaweza kuhisi kwamba, anasumbuliwa sana.

Nilibaini kwamba, hata mimi sikuwa safi sana kama nilivyokuwa nafikiria. Nilibaini kwamba, kuna wakati nilikuwa najaza uchafu mahali ambapo tulikuwa tunatupa uchafu, halafu sishughuliki kujua nani ameutupa uchafu huo. Kumbe hawa jirani walikuwa wanafanya kazi hiyo. Hawakuwahi hata mara moja kulalamika.

Lakini niligundua pia kwamba, nilikuwa ‘ninawashiti' waziwazi hawa jirani zangu na wakawa wanajua hilo. Hivyo kuna wakati walikuwa wanafanya visa vyao ili kunikera. Nilikuwa sijaoa, hivyo nikija na msichana hapo nyumbani, kama wakiwepo, ilikuwa ni vurugu ya kufa na kupona. Ndilo nililogundua baaada ya kujiuliza maswali.

Nilichofanya ni kuanza kuwaonyesha kwamba, nawaheshimu, nikawa nawalipa watu kuja kuzoa zile taka na siku nyingine nikija na vitu nyumbani nawagawia kidogo. Nilishangaa kwamba, walianza kupunguza visa vyao. Kwa mfano, hata wakiwa wamelewa na kuanza vurugu, nikitoka kuwachungulia kutokana na hali hiyo walikuwa wanapunguza kelele na walikuwa wakisema, ‘unaona fujo zako, hadi unamkera mtu asiyehusika.'

Nilizidi kuwafanyia kwa wema sana mambo mengi, bila kujigeuza b.w.e.g.e. Hatimaye niligundua kwamba jirani wengi huwa wanakera, wakati mwingine wakiwa hata hawajui kwamba, wanakera. Kuna wakati ujirani unakuwa mbaya kwa sababu, jirani wote ni wakorofi, hakuna aliyetayari kuwa na busara na kujishusha.

Kuna wakati hata hivyo unaweza kuwa mwema na ukajitahidi sana kuwafanya waone tatizo lao, lakini wakashindwa kuliona na kulikubali. Inapofikia hatua kama hiyo, inabidi kama nilivyosema awali uangalie kama jambo husika ni kinyume na sheria. Kama ni kinyume na sheria, inabidi uende kwenye vyombo vya sheria. Kama siyo kinyuime na sheria, inabidi bado uwe mpole na kutafuta mtu wa kati ambaye mtakaa naye na huyo jirani kujaribu kutafuta suluhu.

Ni vizuri kukagua kama maudhi ya jirani yanawakera jirani wengine. Kama yanawakera, kuna haja ya wewe kuanzisha umoja na hao jirani wengine, ambapo kwa pamoja mtakaa na kutazama namna ya kumsaidia au kumkabili jirani mkorofi na kumaliza kero zake. Kuna wakati jirani wengi wakiwa na kauli moja kuhusu kusumbuliwa na jirani, sheria inaweza kulitazama jambo hilo kwa makini.

Kama ni nyumba ya kupanga na jirani yako ni mpangaji mwenzako, ni vyema kumwona mwenye nyumba na kumweleza tatizo lako. Kuna uwezekano wa mwenye nyumba kuliona tatizo lako na kulielewa na hivyo kumpa notisi jirani huyo mkorofin ili ahame.

Nina uzoefu wa kutosha kwamba, mara nyingi vita ya majirani ni matokeo ya ujuaji wa majirani wote. Kama mmoja akiwa mwelewa, uwezekano wa kuyeyusha ukorofi wa mwingine ni mkubwa.
 
Vizuri sana kuwaheshimu majirani zako.

Surat An-Nisā' (The Women) - سورة النساء



4_36.png
Sahih International
Worship Allah and associate nothing with Him, and to parents do good, and to relatives, orphans, the needy, the near neighbor, the neighbor farther away, the companion at your side, the traveler, and those whom your right hands possess. Indeed, Allah does not like those who are self-deluding and boastful.



The Prophet Muhammad (peace be upon him) used to remind his companions to treat their neighbours well. He said:

'Whoever believes in Allah (Most High) and the Last Day, let him treat his neighbour well; whoever believes in Allah (Most High) and the Last Day, let him honour his guest; whoever believes in Allah (Most High) and the Last Day, let him speak good or else remain silent.'


sahih al-Bukhari and Muslim
​
 
Somo zuri mkuu ubarikiwe.Ni vile niko kwa phone like ingekuhusu
 
Aisee, nimejifunza kitu hapo!
Maana reaction yangu mimi ingekuwa kuwaignore na kuhama.
Umenikumbusha mbali; maishani sikuwahi kushare nyumba mpaka nilivyoenda kwa dada yangu; nyumba kubwa ilikuwa na bedrooms 4 na dada alichukua 3, so Jirani mmoja muuza nyanya Sokoni alikuwa anapiga mziki kwa nguvu yaani hamlali usiku (nyumba haina ceiling).

Nikamshawishi dada tukahamia kwenye nyumba yake ambayo hata madirisha ilikuwa bado.

And come to think of it; nafikiri yule Mdada alikuwa anatafuta company au attention tu kwani my Sis was working na hana muda, nami sio mtu wa kujichanganya sana.
 
Mtambuzi, kuna haja ya kutambua kuwa kuna watu wameumbwa na materials tofauti.
Wapo walioumbwa kwa dhahabu safi na wapo walioumbwa kwa kinyesi cha wanyama.
Hawa walioumbwa kwa kinyesi cha wanyama ni matatatizo mtindo mmoja, hata ufanyeje, hawatosheki wala hawaridhiki, ni lawama tu
 
Last edited by a moderator:
Kutana na majirani wote wakorofi lakini usithubutu kukutana na jirani ambaye ni Mzee wa Busara....hawa watu huwa wana visa chungu nzima ili mradi tu watafute chanzo cha kuja usiku kusugua makalio yao kwenye uso au kifua.
Sasa kasheshe jingine huwa ni pale kula wala wewe lakini kushiba ashiba yeye na kutwa mipanya haiishi ndani ya nyumba kumbe yaja jitwalia chakula au kufanya tu uharibifu wa mali zako.
cc: Zinduna
 
Last edited by a moderator:
Nyumba za kupanga balaa! Je ukikutana na mwenye nyumba mkorofi, wapangaji wakorofiii.Sijui utakimbilia wapi.Ni heri kujipanga kutaftua kwako kama utajaaliwa
 
Nyumba za kupanga balaa! Je ukikutana na mwenye nyumba mkorofi, wapangaji wakorofiii.Sijui utakimbilia wapi.Ni heri kujipanga kutaftua kwako kama utajaaliwa

Huna uwezo huo sasa wa kutafuta kwako, au hata ukipata kwako majirani waliokuzunguka wanakuletea kidamisi utauza nyumba ukajenge kwingine?
 
Jirani mwanamalundi,mzabzab,mwanamtokapabaya Zinduna balaa
 
Last edited by a moderator:
Hahahahaah, kaka Mtambiazi umenikumbusha mbali sana, nilikuwa na jirani anadai kuwa mm najidai, naringa, na kama nimesoma niende nikakae masaki, basi alikuwa anakusanya taka taka analeta kuweka kwenye geti langu, mm nazitoa naenda kutupa na wala simuulizi, na nikikutana naye namsalimia vizuri sana bila kuonyesha kinyongo chochote, alikaa na tabia yake hiyo mwishowe alijiona mjinga, na kuacha kabisa tabia hiyo. na yeye akawa ndiyo mlinzi wa getini kwangu.

Kwa hiyo ukikaa na jirani mkorofi wewe kuwa mkimyaa na mjinga kwake na usimesemeshe hata ukimkuta anafanya baya lolote pale kwako. sema sasa hao wanaofungua REDIO kwa nguvu mweeeh! sijui utafanyaje.
 
Mtambuzi siku hizi mbinu zako ndo naziweza.......

Enzi zile walaaaahiiiii pangechimbika...

Kweli utu uzima dawa
 
Last edited by a moderator:
Jirani mwanamalundi,mzabzab,mwanamtokapabaya Zinduna balaa

Amu umeua.. Bila kusahau matola na zomba wamepakana vyumba.. Wakianza kubishana siasa hapo si ni balaa hilo..

Usiombe uwe na jirani Natalia ndani ya new york city ha ha ha
 
Last edited by a moderator:
Amu umeua.. Bila kusahau matola na zomba wamepakana vyumba.. Wakianza kubishana siasa hapo si ni balaa hilo..

Usiombe uwe na jirani Natalia ndani ya new york city ha ha ha

umeona eee sasa kuna yule kiranga atakuongelea kiinglish ambacho hata malkia hakijui...
Wakina asprin watakukagulia watoto wako wote...
Huyo zinduna atakusuta kila siku...mwanamalundi unagombana na mkeo unaomba ushauri anakuambi'this is your private business hayanihusu''
kuna majirani wengine noma wanataka waishi kama bosnia na chechinia
 
Jamani mm hayo yote kaka nimeyafanya kwa jirani zangu lkn sina raha jamani kwa sasa nipo likizo nimenenepa kwa amani kwani nipo mbali nao ila kila niki wafikiria nakonda kwa mawazo nalipa bill zote usafi nafanya sana kuliko wao mimi nikama kiongozi kwenye hiyo nyumba nawapa uhuru wa kila aina ila wapi jamani kila nifanyalo kwao baya cjui niwafanyie nn now nimeamua kugeuza kwangu jela nikitoka nafunga nikirudi najifungia kwa kuwaogopa wao nakiri nwaogopa maana hawanipi amani wanataka waingie toilet wafanye mambo yao bila kufanya usafi ukisema tabu wamenigeuza ----- cjui hata la kufanya kujipendekeza kwa kuwapa zawadi kupiga nao stori vyote nimefanya naambulia kuambiwa nina mdomo cjui yote natafuta amani kaka looh ila wapi
 
Jamani mm hayo yote kaka nimeyafanya kwa jirani zangu lkn sina raha jamani kwa sasa nipo likizo nimenenepa kwa amani kwani nipo mbali nao ila kila niki wafikiria nakonda kwa mawazo nalipa bill zote usafi nafanya sana kuliko wao mimi nikama kiongozi kwenye hiyo nyumba nawapa uhuru wa kila aina ila wapi jamani kila nifanyalo kwao baya cjui niwafanyie nn now nimeamua kugeuza kwangu jela nikitoka nafunga nikirudi najifungia kwa kuwaogopa wao nakiri nwaogopa maana hawanipi amani wanataka waingie toilet wafanye mambo yao bila kufanya usafi ukisema tabu wamenigeuza ----- cjui hata la kufanya kujipendekeza kwa kuwapa zawadi kupiga nao stori vyote nimefanya naambulia kuambiwa nina mdomo cjui yote natafuta amani kaka looh ila wapi

Kama umepanga hama nyumba! Ya nini ujitese kwa mawazo..

Mimi ni bora nilipe hela nyingi kodi kuliko kupanga nyumba ya kushare vitu... Najijua mi mwenyewe kufanya kitu hadi nijisikie.
 
Yani mkata kiu umeongea ndugu yangu kwakweli yamenifika shingoni tatizo nikaribu na shughuli zangu alafu pana usalama na kupata nyumba. Nitabu mno maeneo hayo ila ushauri wako rafiki yangu naufanyia kazi
 
Kuna jirani wengine anakuja na pikipiki yake ana i test dirishani kwako zogo tupu
 
Mpangaji mwenzako anayefungua mziki kwa sauti ya juu sana unamwomba apunguze sauti anagoma, wewe nunua nyama kilo mbili, ziweke room mwako mezani tu na ufunge room yako halafu nenda likizo ya wiki mbili ili avute muozo huo, then urudi ukiwa kimyaaaaa!?
(Don't try this)

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom