Jinsi ya kuzuiya tatizo la simu kupata moto mara kwa mara

Nov 16, 2018
1
4
image.jpg


Habari...

Software Support Tanzania Tunafahamu Tatizo la simu kupata moto ni tatizo kubwa sana miongoni mwa watumiaji mbalimbali wa smartphone. kuna sababu nyingi sana zinazoweza kusababisha simu kupata moto na ndani ya sababu hizi zipo sababu nyingine ni za kawaida tu hivyo huna haja ya kuwa na wasiwasi kila mara unapo sikia simu yako ina joto la kawaida.


Lakini kama simu yako imekuwa ikipata joto mara kwa mara tena hata kama hutumii simu hiyo basi ni wazi hilo ni tatizo kubwa na linahitaji kurekebishwa mara moja. Sasa zifuatazo ni hatua ambazo ukizichukua pengine unaweza kudhibiti tatizo hili lisiweze kutokea. Pia kama tatizo hili alijatokea kwenye simu yako basi nadhani ni wakati wa kuweza kufuata hatua hizi ili kuhakikisha tatizo hili halitokei kwa namna yoyote ile. Basi bila kupoteza muda let’s get to it..

Yaliyomo
  1. Chaji Simu Yako na Chaja Sahihi
  2. Chaji Simu Yako Kwa Usahihi
  3. Kumbuka Kuzima Sehemu ya Location na WiFi Kumbuka Kupumzisha Simu Yako
  4. Zima Programu Zote Baada ya Kutumia
  5. Ondoa File za Cache Mara kwa Mara
  6. Usiweka Kava Lenye Kuziba Kabisa Simu Yako
  7. Usiweke Simu Yako Sehemu iliyo Jibana au Yenye Joto Kali Simu Kupata Joto Sana ni Dalili ya Battery Kufa

1. Chaji Simu Yako na Chaja Sahihi
Jambo ambalo lina changia kwa asilimia 90 simu kupata moto ni pamoja na battery ya simu yako, ni muhimu kuhakikisha unazingatia usalama wa battery yako kwa kuchajia na chaji ambayo ni sahihi. Chaji sahihi ni ile ambayo inakuja na simu yako au ile ambayo inaendana na simu kwa namna zote ikiwa pamoja na kiasi cha umeme inachotoa.

Mara nyingi watu hutumia chaji tofauti na simu zao ili kuweza kuharakisha simu kujaa chaji au kwa sababu ya kutokua na chaji sahihi, lakini napenda kukwambia ni vyema kuacha kuchajia simu yako kwa hizo kwani chaji inayotoa umeme mdogo zaidi au mkubwa zaidi zote zinaweza kuharibu battery ya simu yako na kusababisha simu kuanza kupata moto sababu ya seli za battery kuchoka.

2. Chaji Simu Yako Kwa Usahihi
Ni kweli kwamba wengi wetu tunajua kuwa simu ikiisha chaji basi ni lazima kuweka kwenye chaji muda huo huo kwani hata hivyo ndio kazi ya simu yako, lakini ni vyema kuanza kutengeneza mpango wa kuchaji simu yako kwani battery ya simu kama ilivyo vitu vingine nayo pia ina muda wake wa mwisho wa matumizi, matumizi haya hufikia mwisho kwa haraka zaidi kulingana na jinsi unavyochaji simu yako mara kwa mara.

Sasa basi kama kuna ulazima ni vyema kuweka mpango wa kuchaji simu yako angalau mara mbili kwa siku, wakati wa mchana chaji simu yako hadi asilimia 50 na tumia mpaka usiku na uchaji mpaka iweze kujaa wakati wa usiku. Pia kumbuka kuvua kava la simu yako kwani hii inaweza kusababisha simu kupata joto pale inapochajiwa.

3. Kumbuka Kuzima Sehemu ya Location na WiFi
Application nyingi kwenye simu yako zina uwezo wa kuwasha sehemu ya location bila hata wewe kujua, kwa mfano app kama ya Uber inaweza kutumia sehemu ya location bila hata wewe kujua na endapo sehemu hii ikibaki ON kwa muda mrefu husababisha simu yako kupata joto sana.

Tatizo hili ni kubwa kwa watu wengi na pia ni moja ya sababu ya simu nyingi kuisha chaji kwa haraka zaidi. Hivyo basi hakikisha unazima WiFi na GPS kila mara unapo anza kuhisi simu yako inapata moto au kila mara baada ya kutumia app kama Uber na nyingine kama hizo.

4. Kumbuka Kupumzisha Simu Yako
Ni kweli kuwa hata simu yako inachoka kwa matumizi ya muda mrefu, hakikisha unapumzisha simu yako mara kwa mara baada ya kuitumia kwa muda mrefu hii ufanya processor ya simu yako kupoa na hivyo pia kufanya simu yako kupungua moto kwa haraka zaidi, pia hii husaidia battery kuweza kudumu na chaji kwa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom