Jinsi ya kuwa Real Estate agent/broker hapa TZ

badison

JF-Expert Member
May 29, 2015
1,450
2,758
Naomba kwa anayejua atujuze wote tupate kujifunza., ni eneo lenye mashiko kwa sasa.

I submit
 
Unatakiwa kuingia darasani kwanza, kwa maana unatakiwa kusomea hiyo fani.
Kuanzia mwakani baada ya kupelekwa muswaada bungeni na kuwa sheria ni lazima kwa kila anayejihusisha na mambo ya Real Estate awe amesomea na awe na cheti toka kwenye board inayosimamia hayo masuala.
Ni muda muda muafaka sasa kwenda kusomea.
 
Estate agent ni eneo pana kiasi na lina makundi mengi sijui wewe unataka eneo lipi?

1. Je ni kununua na kuuza real estate properties?

2. Kusimamia real properties kwa niaba ya mtu mwenye mali?

3. Kuunganisha na kushughulikia miamala ya uhamishaji wa miliki kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine?

4. Kufanya biashara ya kulist properties kwa ajili ya wenye uhitaji kucheki na kuwasiliana na wenye property kwa ajili ya kuuza au kupanga?

5. Kutafuta na kuuza taarifa za hali ya soko la real properties ndani ya Dar es Salaam?

Unataka kufanya ipi kati ya hizo maake zinahitaji utaalam tofauti kama uelewa wa sheria hadi utaalam wa property management.
 
Back
Top Bottom