Jinsi ya kuwa na sehemu ya dharura wakati wa moto ndani ya nyumba

ikigijo

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
1,821
1,874
Habari wadau!

Tumekuwa tukijadiliana mambo mengi ya siasa, mapenzi, afya, kilimo nk! Leo naomba niongelee suala la moto.

Kumekuwa na majanga mengi ya moto yanayosababishwa na shoti ya umeme, jiko, pasi, friji nk. Na vyanzo vingi vya moto vimekuwa vikianzia jikoni, sebuleni! Mtaongezea kulingana na uzoefu wenu pia.

Sasa je, unafanyaje ili kuwa na sehemu ya kutokea ya dharura ambayo wanajua ni familia yako tu? Assume moto ni mkubwa hauwezi kuzimika kwa fire extinguisher.

Mawazo yenu wadau!
 
Onana na mafundi wazuri upande wa grilles watakusaidia, huwa katika moja ya dirisha za nyumba yako utachagua moja wanatengeneza mfano wa kijimlango ndani ya dirisha na kinakuwa na kitasa kwa ajili ya kofuli(wenyewe wanaita Escaper window) ukiwa kwa nje huwezi kuona, ni mfumo mzuri sana utakusaidia siyo wakati wa moto tu hata ukiwa na maadui itasaidia kuokoka.

Inashauriwa dirisha hili liwe chumbani kwa wazazi na funguo ziwe sehemu itakayojulikana na familia nzima.
 
Bora bajeti ya grilles peleka kwenye electrical fance, kwenye madirisha weka vioo tu itakuwa rahisi kuvunja na kuescape. Au uchimbe handanki ndani ya nyumba Moto ukiwaka chapu mnadumbukia na kutokea nje.

Kingine jiko weka separate na nyumba ya kulala hii Ni njia ya asili ya wazee wetu jiko linajitegemea kabisa kupunguza risk ya Moto.​
 
Pia unaweza kudhibiti matukio ya moto kutofika mbali na kuleta madhara makubwa

Mfano kwenye nyumba yako chukua kwa tahadhari hizi

1. Fire extinguish jikoni, sitting room na chumbani atleast ziwe hata nne,

2. Jikoni, weka gas nje, toboa ukuta pitisha mpira wa gas nje kuzuia majanga ya moto yanayosababishwa na gas

3. Milango weka ya mbao achana na milango ya grill/chuma

4. Jenga mjego wako kwa kuweka gypsum board hii haishiki moto, tofauti na celling board inakamata moto haraka na kusambaa nyumba nzima.
 
Ukiweka madirisha ya kuweza kupita au laini jua wezi watajimwaga kwako,ukiweka mlango utakao kuwa rahisi kufunguka basi wazee wa fatuma watatumia nyundo.

Sehemu zote nilizo zizitaja tumeweka ulinzi mkubwa sana hata kupenya wala pakutokea ni ngumu.
 
Pia ni jambo la muhimu sana wengi tunajisahau, ila ingefaa kuwa na dirisha la kutokea ambapo mnaijua wanafamilia, hilo dirisha liwe ukigonga tu kwa ndani linafunguka kwa urahisi
 
Ukiweka madirisha ya kuweza kupita au laini jua wezi watajimwaga kwako,ukiweka mlango utakao kuwa rahisi kufunguka basi wazee wa fatuma watatumia nyundo.

Sehemu zote nilizo zizitaja tumeweka ulinzi mkubwa sana hata kupenya wala pakutokea ni ngumu
Unaweka dirisha ambalo kwa ndani linakua ni rahisi kufungua ukipiga teke kwa ndani dirisha linafunguka,
 
Onana na mafundi wazuri upande wa grilles watakusaidia, huwa katika moja ya dirisha za nyumba yako utachagua moja wanatengeneza mfano wa kijimlango ndani ya dirisha na kinakuwa na kitasa kwa ajili ya kofuli(wenyewe wanaita Escaper window) ukiwa kwa nje huwezi kuona, ni mfumo mzuri sana utakusaidia siyo wakati wa moto tu hata ukiwa na maadui itasaidia kuokoka.

Inashauriwa dirisha hili liwe chumbani kwa wazazi na funguo ziwe sehemu itakayojulikana na familia nzima.
Kwamba chumba cha wazazi kiwe free entrance,watoto au dada wa kazi anaweza ku access?sio sawa,nadhani mambo yote ya moto ikiwemo vizima moto lazima vikae sehemu kusipo na kizuizi na ni rahisi kufikika na yeyote.

Kulingana na dizaini ya nyumba ni vema likakaa kwenye korido au dinning
 
Pia unaweza kudhibiti matukio ya moto kutofika mbali na kuleta madhara makubwa

Mfano kwenye nyumba yako chukua kwa tahadhari hizi

1. Fire extinguish jikoni, sitting room na chumbani atleast ziwe hata nne,

2. Jikoni, weka gas nje, toboa ukuta pitisha mpira wa gas nje kuzuia majanga ya moto yanayosababishwa na gas

3. Milango weka ya mbao achana na milango ya grill/chuma

4. Jenga mjego wako kwa kuweka gypsum board hii haishiki moto, tofauti na celling board inakamata moto haraka na kusambaa nyumba nzima.
Kibongo bongo dawa ni Escaper window tu mkuu hizo fire extinguishers kuna stage unakuta umekuja kustuka moto umefika hata waje fire guard na lorry zao zile kuukuu hawafui dafu.

Kama unakumbuka 2015 yule jamaa wa kipemba ilikufa familia nzima buguruni yeye akiwa zamu ya ulinzi bandarini?wale moto ulishakuwa mkali grilles za milango ya nje zimeshashika moto hazikamatiki moto mkali hata majirani sasa wakawa wameshakaa mbali maana huo moto tena hausogeleki wao familia nzima watu 9 wakaenda kujifungia kwenye chumba kimoja wakaungua wote tu-assume hiki chumba ndo kingekuwa na hili dirisha si wangeokoka wote?

Ukisema uweke milango ya mbao nyumba zenyewe mnajenga umbali metre 100/00 kati ya jirani na jirani nje ya miji huko kila siku kilio kuvamiwa,hiyo #2 ni nzuri maana hata case ya juzi jamaa aliyekufa na familia yake yote kama huu mtungi ungekuwa nje yasingetokea yale.
 
Yote niliyotaka kusema umesema mkuu, sina la kuongeza.
 
Escaper window ni muhimu na pia nimejadili post ya chini, ila pia usichukulie poa hizi fire extinguisher na njia nyingine za kukabili janga la moto zinasaidia na zinaokoa madhara makubwa sana, chukulia mfano Escaper window (EXIT) unayoitegemea ndiyo moto umeanzia huko, ni lazima na ni vyema pia kuweka na more options za kupambana na moto kuliko kuweka tegemeo kwenye njia moja tu ya kuepukana na janga la moto.
 
Kwamba chumba cha wazazi kiwe free entrance,watoto au dada wa kazi anaweza ku access?sio sawa,nadhani mambo yote ya moto ikiwemo vizima moto lazima vikae sehemu kusipo na kizuizi na ni rahisi kufikika na yeyote.

Kulingana na dizaini ya nyumba ni vema likakaa kwenye korido au dinning

Kwani humo chumbani unaweka nini cha ajabu mkuu kiasi hata wanao wasiingie kama ni pesa si zinawekwa bank?

Na mara nyingi haya matukio ya kufa moto hutokea usiku ni case chache sana moto ukauwa watu mchana so ikitokea usiku hata nyie wazazi mtakuwepo tu,nimesema siyo moto tu upo unavyoishi wewe kuna watu hawakupendi wanaweza kupanga kukuvamia hii sehemu ikakuokoa so tuseme ndo wameshaingia ndani utarudi corridor kufungua utoke?pia dinning hawashauri panaweza kuwa uchochoro wa kupita wezi ikiwa bahati mbaya wameona hili dirisha.

Vyovyote ilivyo ni chaguo la mtu ila ni muhimu sana nyumba kuwa na hiki kitu.
 
Kibongo bongo dawa ni Escaper window tu mkuu hizo fire extinguishers kuna stage unakuta umekuja kustuka moto umefika hata waje fire guard na lorry zao zile kuukuu hawafui dafu.

Kama unakumbuka 2015 yule jamaa wa kipemba ilikufa familia nzima buguruni yeye akiwa zamu ya ulinzi bandarini?wale moto ulishakuwa mkali grilles za milango ya nje zimeshashika moto hazikamatiki moto mkali hata majirani sasa wakawa wameshakaa mbali maana huo moto tena hausogeleki wao familia nzima watu 9 wakaenda kujifungia kwenye chumba kimoja wakaungua wote tu-assume hiki chumba ndo kingekuwa na hili dirisha si wangeokoka wote?

Ukisema uweke milango ya mbao nyumba zenyewe mnajenga umbali metre 100/00 kati ya jirani na jirani nje ya miji huko kila siku kilio kuvamiwa,hiyo #2 ni nzuri maana hata case ya juzi jamaa aliyekufa na familia yake yote kama huu mtungi ungekuwa nje yasingetokea yale.

Milango ya mbao mkuu ni tofauti na milango ya grill tukubaliane hilo kwanza, mlango wa mbao unaweza fungua au kuvunjwa kwa wepesi kuliko wa chuma
 
Njia rahisi ambayo wengi hatuifikirii ni kuwa na nyundo nzito( 20kg walau) hizi nyundo ziwemo kadhaa ndani ya nyumba.Inachukua si zaidi ya dakika tano kubomoa ukuta kupata upenyo wa kutoka nje kwa kutumia nyundo yenye uzito huo.Mapigo matano tu,tayari umepata tundu kubwa ambalo linatosha watu kutoka nje.
 
Kibongo bongo dawa ni Escaper window tu mkuu hizo fire extinguishers kuna stage unakuta umekuja kustuka moto umefika hata waje fire guard na lorry zao zile kuukuu hawafui dafu.

Kama unakumbuka 2015 yule jamaa wa kipemba ilikufa familia nzima buguruni yeye akiwa zamu ya ulinzi bandarini?wale moto ulishakuwa mkali grilles za milango ya nje zimeshashika moto hazikamatiki moto mkali hata majirani sasa wakawa wameshakaa mbali maana huo moto tena hausogeleki wao familia nzima watu 9 wakaenda kujifungia kwenye chumba kimoja wakaungua wote tu-assume hiki chumba ndo kingekuwa na hili dirisha si wangeokoka wote?

Ukisema uweke milango ya mbao nyumba zenyewe mnajenga umbali metre 100/00 kati ya jirani na jirani nje ya miji huko kila siku kilio kuvamiwa,hiyo #2 ni nzuri maana hata case ya juzi jamaa aliyekufa na familia yake yote kama huu mtungi ungekuwa nje yasingetokea yale.

Fire extinguish inaweza kufanya mambo mawili makuu either kuuzima moto kwa kiwango cha moto uliopo au pia kuzima sehemu unapotaka kutokea ni hivyo mkuu usiwaze mambo mengi sana jaribu kuwaza lilopo karibu sio mambo mengi mengi, unatakiwa ufikirie haraka janga likitokea sasa sahivi unawaza mambo kibao na kubisha vitu kibao, akili yako ndiyo ina determined namna utakavyo okoa familia yako na wewe, familia zilizokufa na janga la moto unakuta walikosa other means,

sasa sisi hapa tunajadiliana na kufundishana nini cha kufanya moto ukitokea, au tunapunguzaje majanga ya moto hilo ndiyo la msingi
 
Njia rahisi ambayo wengi hatuifikirii ni kuwa na nyundo nzito( 20kg walau) hizi nyundo ziwemo kadhaa ndani ya nyumba.Inachukua si zaidi ya dakika tano kubomoa ukuta kupata upenyo wa kutoka nje kwa kutumia nyundo yenye uzito huo.Mapigo matano tu,tayari umepata tundu kubwa ambalo linatosha watu kutoka nje.

Nyundo ya kuvunja mlango au ukuta mkuu, usitumie njia ambazo zitakuchelewesha pia kutoka na utatumia nguvu nyingi sana, unapotumia nguvu sana akili inachoka, kumbuka jinsi unavyokaa ndani sana ule moshi ni carbonmonoxide ukiuvuta tu unaanguka chini una faint... So moto unapita unakuivisha tu
 
Kwani humo chumbani unaweka nini mkuu kiasi hata wanao wasiingie kama ni pesa si zinawekwa bank?

Na mara nyingi haya matukio ya kufa moto hutokea usiku ni case chache sana moto ukauwa watu mchana so ikitokea usiku hata nyie wazazi mtakuwepo tu,nimesema siyo moto tu upo unavyoishi wewe kuna watu hawakupendi wanaweza kupanga kukuvamia hii sehemu ikakuokoa so tuseme ndo wameshaingia ndani utarudi corridor kufungua utoke?pia dinning hawashauri panaweza kuwa uchochoro wa kupita wezi ikiwa bahati mbaya wameona hili dirisha.

Vyovyote ilivyo ni chaguo la mtu ila ni muhimu sana nyumba kuwa na hiki kitu.
Hicho chumba cha wazazk jamaa nimemuelewa sana hebu fikiria siku haupo na upo kazini pah janga la moto hilo unafikiri watoto watatokea wapi au watakusubiri mpaka utoke kazini, jamaa kasema vizuri wekeni njia ya kuikimbia moto na vifaa vyake kwenye vyumba vya watoto ili likitokea janga ni rahisi, mkuu usiweke complications nyingi, chagua mambo yatakayo kuwa rahisi kwenye nyumba yako kuikimbia moto
 
Back
Top Bottom