Jinsi ya kutengeneza juice

shabaan Dogo

Senior Member
Apr 27, 2014
197
79
Habari zenu wakuu
Naomba msaada wa kutengeneza juisi zifuatazo

(1)Juisi ya tangawizi
Nataka jua kiufasaha, na je naweza weka sukari au asali? Naomba mnijuze vizuri.

(2) Pia nataka kujua jinsi ya kutengeneza juisi ya karoti na vinavyowekwa humo au ni karoti tu hamna hata kuweka sukari?

(3)Juisi ya tende na maziwa.

(4) Juisi ya parachichi na maziwa.

Naombeni sana msaada wenu ili kujua kutengeneza aina zote za juisi nilizozitaja tafadhalini
 
Habari zenu wakuu
(1) naombeni msaada nawezaje kutenggeneza juic ya tangawizi nataka jua kiufasaha na je! Naweza weka sukari au asali naombe mnijuza vizuri
(2) Pia nataka kujua jinsi ya kutengeneza juic ya karoti na vinavyo wekwa humo au ni karoto tu hamna hata kuweka suger sukari?
(3) Nataka jua kutengeneza juic ya tende na maziwa
(4) Juic ya parachichi na maziwa naombeni saana msaada wenu ili kujua kutengeneza aina zote za juic nilizo zitaja tafadhalini


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Na mimi nitadoea maujuz!
Ngoja wataalamu wa mambo waje
 
Mi ntakusaidia Juice ya karoti
Kuna aina ya carrots zina sukari na zingine hazina sukari sana.Kwa juice carrots nyembaba na ndefu ndo zina sukari.Kama carrots zina sukari hakuna haja ya kuongeza sukari ,kama hazina sukari ya kutosha ongeza sukari kidogo wakati wa kublend.
Pia waweza weka tangawizi kipande kidogo wakati wa kublend inakuwa tamu balaa.
Hizo juice zingine mie sio mzoef.
 
Karanga zinakua mbichi au za kukaanga???

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kaka kuna jukwaa la mapishi, yaani ungepeleka hii shida yako kule ungejibiwa haraka na kwa ufasaha zaidi!
 
Juice ya Tende-Maaana hii natengeneza mwenyewe nyumbani na pia shemeji yao hutengeneza kwa matumizi ya nyumbani
:-Mahitaji ni Tende na Maziwa
-Kwanza unaichambua Tende kwa kutoa Kokwa zake,na kubakia na nyama tupu
Kisha unaiweka kwenye blender na kuchanganya na maziwa kisha unaisaga na ulaini wake inategemea na unataka uwe vipi,ila bora zaidi kuwa laini Zaidi ili maziwe yachanganyike vizuri na Tendena ilete maana halisi ya Juice licha ya kwamba Juice ya Tende unatumia kijiko kuinywa,hahaha.
-Wingi wa Maziwa na Tende inategemea na unataka iwe na umajimaji kiasi gani kuna Juice ya tende nzito na Nyepesi.Juice ya Tende haitiwi maji kabisaa ni maziwa tuu
Mie hupendelea Zaidi nyepesi kiasi,maana ndio unapata fleva vizuri.
Ukimaliza hapo unaiweka kwenye jagi kisha unaweka kwenye fridge,ila hii ni hiari sio lazima,unaweza kunywa hivyo hivyo bila ubaridi na ipo vizuri tu.
Angalizo:Juice ya Tende haitiwi Sukari mkuu wala kitu chochote artificial

Karanga na Habat al Sawda(Habba Soda):
Hivi huwa tunaita kama vikorombwezo,kama vile chips,ni kwamba unaamua uweke salad au pilipili.
Sasa hivi vyote havichangaywi mwanzo,ila hivi hutumika pale tu unapotaka kuinywa.
Yaani unatia kwenye glass kisha ndio unaweka karanga au Habba Soda au vyote kwa pamoja
Karanga bora zaidi ni za kukaangaa,ndio zinanyambuka vizuri,maana unazisaga zinakuwa kama chenga chenga


Asije mtu akakuambia kwamba Unachanganya Karanga na Tende na Maziwa,hapo haifiki jioni Juice yoote itachacha.
Wakati Maziwa na Tende hadi wiki inafika ikiwa kwenye Uhalisia wake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom