Jinsi ya kutengeneza chilli sauce

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,775
2,400
Somo langu la pili Leo ninamna ya kuunda chilli sauce kijana mama baba Dada acha kuzubaaa maisha yako yako mkononi mwako waweza badilisha maisha yako mwenyewe kwa kutumia mikono yako karibu darasani

Yafutayo ndiyo mahitaji kwa ajili ya kutengenezea chili souce;
a) Pilipili mbuzi nyekundu robo 1/4 kilo.

b) Nyanya kilo moja.

c) Kitunguu swaumu kikubwa kimoja.

d) Mafuta ya kula vijiko 7 vya chakula.

e) sukari vijiko viwili vya chai.

f) maji ya moto kikombe kimoja cha chai.

g) vinega vijiko 3 vya chai.

Baada ya kuandaa mahitaji hayo ya jinsi ya kutengeneza chili souce, twende kuona moja kwa moja jinsi ya kutengeneza chili souce

HATUA YA KWANZA.
-Kata Pilipili kuondoa mbegu.

-menya nyanya kuondoa mbegu pia.

-menya vitunguu swaumu kisha
vikatekate viwe katika vipande vidogo vidogo.

Nb; baada ya kumaliza hatua hiyo ya maandalizi chukua Brenda, kisha saga mchanganyiko wote wa malighafi ambazo nimezianisha kwenye hatua ya kwanza. Saga mchanganyiko huu mpaka uone imetoka rojo laini.

HATUA YA PILI.
Ukishamaliza kusaga mchanganyiko huu hapo juu jambo ambalo unatakiwa kulifanya ni;

*Chukua sufuria yenye nafasi ya kutosha kwa ajili ya kupika mseto huu.

*Weka sufuria yako jikoni, iache kwa sekunde kadhaa ili ipate moto pia kama kuna maji katika sufuria yaweze kukauka.

*Baada ya kuona sufuria yako imekwisha kupata moto, chukua mafuta ya kula yaweke kwenye sufuria, yaache yachemke.

* mafuta yakichemka chukua mseto wako mwagia katika sufuria yako, koroga mseto huo kuelekea upande mmoja kwa dakika 30 huku mseto huo ukiendelea kuchemka.

* Baada ya dakika 30 epua mseto huo na uuache upoe, kisha funga katika vifungashio kwani mseto huo utakuwa umeshakuwa chili souce.

Mpaka kufikia hapo utakuwa umekwisha kutengeneza chili souce ambayo inafaa kwa ajili ya matumizi ya binadamu kwani ni salama kwa ajili ya afya yetu.
2c4c949ac779631807e821bdc63d538c.jpg
 
Asante kwa kutuletea utaalamu
Nauliza expiry date ya hiyo bidhaa itakua baada ya muda gani? (Shelf life yake namaanisha)
 
Mkuu waweza tengeneza ukaweka ndani
Kwako ukawa unatumia kidogo kidogo

Nadhan ikianza kuharibika utajua
Tu ladha itabadilika

Mm sina utaalamu huo sanaa
Lakini kwawale wanao tumia kwa wingi kama biashara lazima. Wapeleke

Kwawadau wanao usika na uchunguzi wa chakula cha ninadamu wao ndio wanaweza toa jawabu
Sahiii zaidi
 
Safi sana watu wanapuuzia lakini ndio maisha yenyewe haya ndio njia ya kutoka sasa
 
Somo langu la pili Leo ninamna ya kuunda chilli sauce kijana mama baba Dada acha kuzubaaa maisha yako yako mkononi mwako waweza badilisha maisha yako mwenyewe kwa kutumia mikono yako karibu darasani

Yafutayo ndiyo mahitaji kwa ajili ya kutengenezea chili souce;
a) Pilipili mbuzi nyekundu robo 1/4 kilo.

b) Nyanya kilo moja.

c) Kitunguu swaumu kikubwa kimoja.

d) Mafuta ya kula vijiko 7 vya chakula.

e) sukari vijiko viwili vya chai.

f) maji ya moto kikombe kimoja cha chai.

g) vinega vijiko 3 vya chai.

Baada ya kuandaa mahitaji hayo ya jinsi ya kutengeneza chili souce, twende kuona moja kwa moja jinsi ya kutengeneza chili souce

HATUA YA KWANZA.
-Kata Pilipili kuondoa mbegu.

-menya nyanya kuondoa mbegu pia.

-menya vitunguu swaumu kisha
vikatekate viwe katika vipande vidogo vidogo.

Nb; baada ya kumaliza hatua hiyo ya maandalizi chukua Brenda, kisha saga mchanganyiko wote wa malighafi ambazo nimezianisha kwenye hatua ya kwanza. Saga mchanganyiko huu mpaka uone imetoka rojo laini.

HATUA YA PILI.
Ukishamaliza kusaga mchanganyiko huu hapo juu jambo ambalo unatakiwa kulifanya ni;

*Chukua sufuria yenye nafasi ya kutosha kwa ajili ya kupika mseto huu.

*Weka sufuria yako jikoni, iache kwa sekunde kadhaa ili ipate moto pia kama kuna maji katika sufuria yaweze kukauka.

*Baada ya kuona sufuria yako imekwisha kupata moto, chukua mafuta ya kula yaweke kwenye sufuria, yaache yachemke.

* mafuta yakichemka chukua mseto wako mwagia katika sufuria yako, koroga mseto huo kuelekea upande mmoja kwa dakika 30 huku mseto huo ukiendelea kuchemka.

* Baada ya dakika 30 epua mseto huo na uuache upoe, kisha funga katika vifungashio kwani mseto huo utakuwa umeshakuwa chili souce.

Mpaka kufikia hapo utakuwa umekwisha kutengeneza chili souce ambayo inafaa kwa ajili ya matumizi ya binadamu kwani ni salama kwa ajili ya afya yetu.
2c4c949ac779631807e821bdc63d538c.jpg
Nyanya unamenya maganda au unatoa mbegu tuu?
 
Hukusema kwa kiasi hicho cha pilipili unatakiwa uweke nyanya kiasi gani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom