Jinsi ya kutambua gari iliyoshushwa Km!

LEGE

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
5,122
9,204
Technolojia ina mengi na inaumiza wengi tusio kuwa na uelewa nayo. Kumbe kuna wimbi kubwa sana la watu wana agiza magari kutoka nje na hata kununua kwenye show room za hapa bongo kwa kigezo cha kuangalia kilomita zilizotembewa na kufanya ndio kipimo cha ubora na ubora wa gari.

Hapo wengi wanaingia sana mkenge kwa kuwa kilomita za gari zinashushwa ili kukuvutia mnunuaji kwa nchi za wenzetu ni kosa kisheria ila sijajua kwa bongo imekaaje.

Lengo la mada hii la kuiweka hapa ni kuwa hapa ni sehemu sahihi sababu kuna wataalam wa IT.

Swali langu kubwa, Je haiwezekani kutambua kuwa gari hii iliwahi kushushwa kilomita?
Nimeshawishika kufikiria hivi baada ya kukumbuka kuwa kwenye hard disc au memory card vitu vikifutwa unaweza kufanya back up na ukavipata tena.

Sasa kwa kuwa kwenye dash board za magari/cluster kilomita zilizotembewa na gari huwa zinahifadhiwa kwenye EEPROM, Je hakuna namna ya kutambua kwamba data zilizomo kwenye eeprom zilisha wahi editiwa?

Iwe kwa kutambua mwanzo ilikuwa na km ngapi au hata kwa kutambua tu kuwa eeprom hii ishawahi fanyiwa ujanja??

Ni mawazo yangu tu kama nimekosea nikosoeni coz sina utaalam sana wa hayo mambo lakini ukinambia nikushushie KM kwenye gari yako nakushushia tuu na mashine
 
Back
Top Bottom