Jinsi ya kutafuta hela na kuzifanya zisikukimbie .....Tafuta hela kwa nguvu zako zote,sana sana ukiwa kijana,ukiajiriwa au ukijiajiri fanya kazi kwa bidii bila kusahau kumshukuru Muumba kwa sala na zaka.
Tafuta hela kama muuza machungwa anayeyamenya na hajui mteja atakuja saa ngapi?
Kama mkaanga chips,mihogo, samaki,maandazi na hajui wateja watatoka wapi?
Mtembea bure si sawa na mkaa bure,Atafutae hachoki,haba na haba hujaza kibaba.
Bila kusahau kuwa na matumizi kiasi,usinunue kitu ambacho hukukipangia bajeti. Bandu bandu humaliza gogo.
Wasalam
Ata asipopita kwani uzi huu nao ni wakutafuta kwamba ukimaliza kusoma na kuchangia unalipwaNilijua watasoma na kupita maana hili la kutafuta wengi hawamo ila kusifia matajiri tu
Mkuu, nikweli kabisa wakati mwingine tunapaswa tujiambie ukweli japokua wapo wenye waliubatiza kwa jina la ukweli mchunguHii ni kweli kabisa bila kupepesa macho
Barikiwa sana mkuuWatanzania wachache wanaupenda ukweli. .Wengi wanatamani dili la laki wapate 10M,which it's not possible