Jinsi ya kupika wali

Top gun maverick

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
2,020
2,601
Habari wanajf nimekuwa nikijaribu kupika lakini naishia kupika bokoboko sasa nilikuwa naomba ushauri jinsi ya kupika wali vizuri kama wa hotelini yaan nisaidieni please.
 
Usitie maji mengi.mi wali napikia jiko la gesi na unatoka umenyooka!pia usiugeuze wakati bado maji hayajakauka
 
Sikia weka maji kidogo tu. Harafu maji yakikauka ukiwa bado na kiini kwa mbali ndo safi, unaipua unaacha pembeni unaiva na joto tu lile unaobaki nao. Then unaendelea na mboga, mpaka mboga iive wali tiari.


Ila ukiwa msela tafta rice cooker.
 
Katika upishi kitu cha kubalansi ni moto unaoigusa sufuria. Kama jiko lako ni zima (la mchina au la gesi) inatakiwa uwe na uwezo wa kuamua sasa hivi utoke moto kiasi au mkubwa.

Weka sufuria jikoni na maji kiasi (hua nachukua maji nusu ya kiasi cha mchele) moto uwe mwingi.

Maji yakichemka weka mafuta. Koroga kama sekunde 20.

Kisha tia mchele koroga tia chumvi funika na mfuniko.

Maji yakikauka Punguza jiko iwe kama vile moto unataka kuzima.

Kisha geuza wali wako.

Uache hivyo kwa dakika 20 mpaka 30.

Ila kwa kesi yako nahisi ni unakosea kwenye kipimo cha maji.
 
Back
Top Bottom