Jinsi ya kupika wali mzuri wa nazi na maua wenye kunukia

Bacyclerbacy

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
1,743
3,017
Mahitaji
-Mchele
-Karoti
-Hoho
-Iliki
-Njegere
-Kitunguu saumu
-Tangawizi
-Nazi ya kukuna ni nzuri zaidi
-Chumvi

-Kuna nazi yako vizuri uikamue na uichuje kidog kidogo kiasi cha maji yatakayotosha mchele wako kisha bandika tui jikoni lichemke
-Osha njegere zitoe kwenye maji
-Chambua iliki kisha zisage ziwe unga/robo kijiko cha chai
-Chambua mchele na uoshe
-Chambua kitunguu saum menya na tangawizi kisha visage kwa pamoja na mafuta ya kula kisha chota kijiko 1 kikuwa cha chakula cha mchanganyiko huo
-Katakata karoti na hoho muundo wa vibox vidogodogo

Jinsi ya kupika

-Bandika sufuria yako jikoni,weka mafuta kidoogo saaana
-Kisha kabla hayajapata moto weka njegere hii inazuia njegere kutorukaruka,koroga hadi njegere zibadilike rangi
-Kisha weka Karoti endelea kukuroga
-Weka mchanganyiko watangawiz na kitunguu saum koroga hapa usichelewe sana maana vitunguu huwa vinawahi kushika chini
-Weka unga wa iliki kisha mchele
-Koroga hadi vichanganyike haswaaa
- Weka tui lako la Nazi lote ulilochuja kisha weka chumvi koroga na ufunike


Baada ya muda angalia wali wako kama umekauka ile nazi uliyoweka kisha palilia(weka moyo juu na chini kidogo)

Subiri kama dk 20 angalia kama umeiva weka hoho ulizokwisha zikata hapo awali kisha geuza kidoogo na funika tena kwa dk 5.

Baada ya hapo waweza pakua wali wako ukiwa na harufu nzuuri na mauwa yake ambayo ni karoti ,njegere na hoho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom