Jinsi ya kupika vidole vya samaki

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
739
484
Leo nawaletea mapishi ya fish fingers ( sijui kama unaweza kusema vidole vya samaki)!, Ni mlo mzuri hasa kuliwa kama kitafunio au mboga ya pembeni au kitafunwa cha jioni.

Mahitaji
500g Fileti ya samaki
120g Chenga za mkate
100g Unga wa ngano
Mayai 2
Ndimu 1
Kitunguu saumu 1
Kotmiri
Mafuta ya kupikia

Matayarisho
Menya vitunguu saumu kisha visage

Katakata fileti kwa muundo wa mraba (kama vidole) kisha paka mchanganyiko wa vitunguu saumu

Kata ndimu na kamulia kwenye fillet yako

Weka chenga za mkate kwenye bakuli kisha uchanganye chumvi kiasi na kata kata kotmiri majani 3 na uchanganye pamoja.

Kwenye bakuli lingine weka mayai na uyapigepige yawe kama uji mzito

Weka unga kwenye bakuli jingine.

Chukua kipande cha fillet kiweke unga kidogo kisha kizamishe kwenye yai na baada ya hapo kizamishe kwenye mchanganyiko wa chenga za mkate. Fanya hivyo kwa vipande vyote.

Weka mafuta kwenye kikaago na subiri yachemke kisha weka fillet zako vizuri na zikaange pande zote hadi zimekuwa rangi ya brown ( hakikisha moto sio mkali sana).

Epua na weka pembeni mafuta yote yakauke

Weka kwenye sahani tayari kwa kula.

Unaweza kula na sosi spesho ya samaki (siku ingine nitawaonyesha jinsi ya kuitengeneza)

Enjoy!
 
Ubarikiwe sana, nizipenda sana na week 2 hizi nimekuwa nikiwazia kugoogle recipe yake maana mtaalam niliyekuwa namjua keshatangulia mbele ya haki. Nitapika this weekend, kwa Dar wapi naweza breadcrumbs, maana kuzindaa mwenyewe naona kazi
 
Je ile samaki itakuwa imeiva kwa ndani au mpk uichemshe kwanza?
Haichemshwi, ndimu na thoum inaanza kuiwivisha kabla hujakaanga. Ila kwa vile ni vidogo, size ya kidole ukiweka kwenye mafuta inaiva haraka sana. Nitumie fillet wa Sato basi?
 
Hahhahaaa.... Shouger nshahama Mza, mie mwenyewe nazitamani sana hizo sato acha tu!!
 
Aisee umeondoka mji wa maziwa na asali? Pole wee, mimi natamani ningekuja huko
 
Leo nawaletea mapishi ya fish fingers ( sijui kama unaweza kusema vidole vya samaki)!, Ni mlo mzuri hasa kuliwa kama kitafunio au mboga ya pembeni au kitafunwa cha jioni.

Mahitaji
500g Fileti ya samaki
120g Chenga za mkate
100g Unga wa ngano
Mayai 2
Ndimu 1
Kitunguu saumu 1
Kotmiri
Mafuta ya kupikia

Matayarisho
Menya vitunguu saumu kisha visage

Katakata fileti kwa muundo wa mraba (kama vidole) kisha paka mchanganyiko wa vitunguu saumu

Kata ndimu na kamulia kwenye fillet yako

Weka chenga za mkate kwenye bakuli kisha uchanganye chumvi kiasi na kata kata kotmiri majani 3 na uchanganye pamoja.

Kwenye bakuli lingine weka mayai na uyapigepige yawe kama uji mzito

Weka unga kwenye bakuli jingine.

Chukua kipande cha fillet kiweke unga kidogo kisha kizamishe kwenye yai na baada ya hapo kizamishe kwenye mchanganyiko wa chenga za mkate. Fanya hivyo kwa vipande vyote.

Weka mafuta kwenye kikaago na subiri yachemke kisha weka fillet zako vizuri na zikaange pande zote hadi zimekuwa rangi ya brown ( hakikisha moto sio mkali sana).

Epua na weka pembeni mafuta yote yakauke

Weka kwenye sahani tayari kwa kula.

Unaweza kula na sosi spesho ya samaki (siku ingine nitawaonyesha jinsi ya kuitengeneza)

Enjoy!
Nishaila sana hii sasa ni wakati wa kuitengeneza
 
Haichemshwi, ndimu na thoum inaanza kuiwivisha kabla hujakaanga. Ila kwa vile ni vidogo, size ya kidole ukiweka kwenye mafuta inaiva haraka sana. Nitumie fillet wa Sato basi?
unachemsha ndio au kusteam
 
n
Ubarikiwe sana, nizipenda sana na week 2 hizi nimekuwa nikiwazia kugoogle recipe yake maana mtaalam niliyekuwa namjua keshatangulia mbele ya haki. Nitapika this weekend, kwa Dar wapi naweza breadcrumbs, maana kuzindaa mwenyewe naona kazi
breadcrumbs zinapatikana village supermarket masaki au maduka yenye bakery
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom