Jinsi ya kupika utumbo mchicha

Simara

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
7,511
23,908
Mahitaji
1. utumbo 1kg
2. Mchicha fungu 2
3. kitunguu 1
4. karoti 1
5. pilipili hoho 1
6. currypowder
7. chumvi
8. Tangawizi
9. Limao
10. Nazi / karanga

MAANDALIZI
1. Bandika utumbo wako jikoni weka limao, tangawizi na chumvi.

2. Ukishaiva ipua, weka sufuria jikoni weka mafuta...yakipata moto weka kitunguu, hoho na karoti...kitunguu kikianza kupata brown weka curry powder

3. Tumbukiza mchicha wako ambao utakua umeukatakata kama yanavyokatwa majani ya maboga, acha uchemke kwa dakika 5 - 10 tia utumbo wako, utaweka na supu ya utumbo kidogo ili mboga ijichanganye vizuri.

4. Ikichemka utamalizia kwa kuweka karanga iliyosagwa au kama utapendelea kuweka nazi haina shida, unaeza kulia wal, ugali au ndizi za kukaanga !!
 
Mapishi ya kupika Kwa kutumia mafuta na nazi Kwa wakati mmoja naona Kama haiwi Poa ! Huwa naona Chakula au mboga inakuwa nzuri zaidi Kwa kutumia Kimoja tu Yani Kama ni nazi basi mafuta yasitumike hata tone!
 
Huwa unapikaje samaki wa nazi? Nyanya, vitunguu, hoho na karoti unavipikaje vipi? Au unavichemsha?
 
yes unachemsha, vikiiva vizuri, tia tui la 2 zen liache lichemke kidogo, tia samaki zen tui la 1 acha lichemke hadi iwe rosti, ipua.

hakikisha nazi yako ni nzuri ile yenye mafuta vizuri. inakua bomba kuliko mafuta plus nazi pamoja.

note: ukipenda weka mafuta, ila kidogo mno, ya just kukaangia kitunguu. but bila mafuta ni bomba mno.
 
Hii mboga ni hatari sana, unaeeza maliza hadi ugali wa watoto.... ngoja leo nimwambie mama watoto aniandalie aseee
 
Hivi hapo mchicha bado unakuwa na virutubisho vinavyotakiwa? Au tunaangalia ladha tu!
Na usinywe soda kama kwako kila kitu ni virutubisho !na mkitambi huu sitaki virutubisho bali viburudisho !
 
Kupika mboga au chakula kwa mafuta pamoja na nazi kwa mboga moja au chakula kimoja ni makosa kiafya!

Hata ukichanganya na karanga ni makosa vile vile!

Yakiwa mazoea ya hivyo Ndiyo wengine hupata magonjwa ya presha ya kupanda na visukari.
 
Mahitaji
1. utumbo 1kg
2. Mchicha fungu 2
3. kitunguu 1
4. karoti 1
5. pilipili hoho 1
6. currypowder
7. chumvi
8. Tangawizi
9. Limao
10. Nazi / karanga

MAANDALIZI
1. Bandika utumbo wako jikoni weka limao, tangawizi na chumvi.

2. Ukishaiva ipua, weka sufuria jikoni weka mafuta...yakipata moto weka kitunguu, hoho na karoti...kitunguu kikianza kupata brown weka curry powder

3. Tumbukiza mchicha wako ambao utakua umeukatakata kama yanavyokatwa majani ya maboga, acha uchemke kwa dakika 5 - 10 tia utumbo wako, utaweka na supu ya utumbo kidogo ili mboga ijichanganye vizuri.

4. Ikichemka utamalizia kwa kuweka karanga iliyosagwa au kama utapendelea kuweka nazi haina shida, unaeza kulia wal, ugali au ndizi za kukaanga !!
Ngoja weekend niingie jikoni, hapa ugali lazima
 
Huwa unapikaje samaki wa nazi? Nyanya, vitunguu, hoho na karoti unavipikaje vipi? Au unavichemsha?

Unaweza kuwapanga samaki kwenye sufuria au chungu kisha ukaweka viungo vyote yaani vitunguu, nyanya zote , carrot, hoho n.k kisha ukaweka tui la pili ndilo la kupikia kwa kulipigapiga hadi lichemke,
Badae unaweka bamia /bilinganya pamoja na tui bubu likiiva mboga tayari.
 
Mahitaji
1. utumbo 1kg
2. Mchicha fungu 2
3. kitunguu 1
4. karoti 1
5. pilipili hoho 1
6. currypowder
7. chumvi
8. Tangawizi
9. Limao
10. Nazi / karanga

MAANDALIZI
1. Bandika utumbo wako jikoni weka limao, tangawizi na chumvi.

2. Ukishaiva ipua, weka sufuria jikoni weka mafuta...yakipata moto weka kitunguu, hoho na karoti...kitunguu kikianza kupata brown weka curry powder

3. Tumbukiza mchicha wako ambao utakua umeukatakata kama yanavyokatwa majani ya maboga, acha uchemke kwa dakika 5 - 10 tia utumbo wako, utaweka na supu ya utumbo kidogo ili mboga ijichanganye vizuri.

4. Ikichemka utamalizia kwa kuweka karanga iliyosagwa au kama utapendelea kuweka nazi haina shida, unaeza kulia wal, ugali au ndizi za kukaanga !!
11. Panado vidonge vinne(4).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom