Jinsi ya kupika tambi za papayu/papai

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,563
3,708
Leo hii tujifunze jinsi ya kupika tambi za mapapayu,usishangae ni katika ubunifu wa mapishi

MAHITAJI

  • Tambi za mapapayu (papayu lilokatwa maganda na kukatwa kwa urefu kama tambi) kiasi bakuli moja la kiasi
  • Tui zito kikombe 1
  • Tui jepesi kikombe 1&1/2
  • Sukari kikombe 1
  • Iliki kiasi

MATAYARISHO

  • Weka tambi kwenye sufuria na maji kiasi cha kufunika tambi, zifunike na uziache zichemke mpaka ziive(zibonyeze na ukiziona ziko laini basi zimeiva) Tambi nyingine ni cherema na huenda zikachukua muda mrefu zaidi kuiva
  • Kisha mwaga maji ya ziada

  • Weka sukari, tui jepesi na iliki kwenye zile tambi ulizozimwaga maji na urejeshe motoni kwa takriban dakika 10
  • Kisha weka tui zito na uziache motoni kwa takriban dakika 5

  • Baada ya hapo tambi zipo tayari ipua anda mezani na chai ya maziwa.
"Nina mpango wa kufungua Mkahawa kwaiyo najiwekea kumbukumbu hapa na kufanya practice nyumbani"
 

πŸ™†πŸ™†πŸ™†πŸ™†πŸ™†πŸ™†πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…