Jinsi ya kupika kabichi pekee na yenye mchanganyiko na mboga za aina nyingine

Mkuu huko mambo yalikua ugali haragwe aisee inafika time hutaki kuskia kitu haragwe so alternative in kupita kwa mama muuza mboga kuchukua kabichi lilikua linaleta mizuka kinyama kupiga ugali ndondo
Na ugari wa dona ni kama unapewa dawa umeze bila maji.
 
IMG_6937.JPG
hata kama hamlipendi kabichi si kumfanyia ivi uyu mkulima
 
Hivi ni nani aligundua kwamba kabichi ni Mboga asee,

Mbona tunatesana hivi si ni bora aliyegundua mrenda japo unatereza lakini ni mwake na ugari kitu kinaenda.

Hivi ugali na kabichi kuna ambae anauelewa kweli ?

Tuache tuseme tu ukweli ni bora nile ugali bila mboga kuliko kula ugali na kabichi.
pole boss! nimepiga hii kitu asubuhi kabla sijatoka home na chapati mbili huku nikihatarisha kampeni ya bomoa kitambi na jana usiku nilikula na wali kiduchu kabichi mlima.
utayarishaji wa kabichi unachangamoto nakumbuka hata nilipokuwa home enzi zile ilikuwa mboga nisiyoipenda lakini bibie anaipika vizuri mno siiogopi kuila.labda nikuibie kidogo inavyopikwa
  1. ikaange kabichi bila kuchemsha na vitunguu nyanya, pilipili hoho,karoti bila kuchemsha kwenye maji kwanza.
  2. ongeza soya source kama unayo
  3. itoe jikoni mapema usiruhusu iive sana
  4. songa ugali mdogo wa dona au mhogo
  5. ambatanisha vipande vichache vya nyama ya kuchemsha iliyochanganywa na tangawizi na limau au samaki wa kuchoma.
 
Zamani nilikua sili kabeji, sasa siku moja niko shule nimepigika kinoma na msosi wa shule haipandi, nikaenda prepo bila kula imefika saa mbili njaa ikawa Kali sana nikakumbuka yule nesi wa shule anajuana na mama nikaona huu ndio muda wa kwenda kumtembelea nyumba yake iko ndani ya eneo la shule, kufika nakuta wali ndo umewekewa mkaa juu nikaona yeeess, nimekaa hadi amepakua kuangalia mboga ni kabeji sikua na jinsi ikabadi nile tokea siku hiyo nilianza kula hiyo mboga japo sio kitu ninachokipendelea!
 
Kabichi sio mboga, ila ni kiungo cha mboga. Sema utamaduni wetu wa lishe ndio tatizo. Hivi ulishawahi kupata utumbo rost iliyochanganywa na viungo kama vyoooteeee, mixer na kabichi kiasi?..........hapo ndio utaamini niliyoyasema kwenye aya ya kwanza hapo juu.
 
Kabichi inakaangwa haipikwi kama makande ndio maana huielewi. Pili kabichi inavirutubisho vingi muhimu mwilini na ni kinga ya maradhi mengi hasa saratani mbalimbali. Kwahiyo kula kabichi acha mbwembwe.
 
Kabichi mbona ni zuri Lumix na nyama rost.

Unapika kwanza rost nyama hadi iwive unawekea Na kabichi kwa mda mdogo tu,inakua Na ladha zaidi ikiwa haijalainika sana.
 
Kabichi mbona ni zuri Lumix na nyama rost.

Unapika kwanza rost nyama hadi iwive unawekea Na kabichi kwa mda mdogo tu,inakua Na ladha zaidi ikiwa haijalainika sana.
Tunasemea kabichi bila mchanganyiko wowote mkuu
 
Kabichi inakaangwa haipikwi kama makande ndio maana huielewi. Pili kabichi inavirutubisho vingi muhimu mwilini na ni kinga ya maradhi mengi hasa saratani mbalimbali. Kwahiyo kula kabichi acha mbwembwe.
Lakini siyo kwa ugari mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom