Jinsi ya kupika chapati za maji

MAHITAJI

Unga wa ngano nusu kilo

Mayai 2

Sukari robo kikombe cha chai

Chumvi kijiko kimoja cha chai

Hiliki nusu kijiko cha chai

Maji ya uvuguvugu kiasi

Mafuta ya kupikia

MATAYARISHO NA KUPIKA

Chukua bakuli kavu weka unga, kisha sukari, chumvi, hiliki na maji kiasi.

Koroga mpaka mchanganyiko wako uwe mzito.

Baada ya hapo weka mayai na ukoroge tena.

Mchanganyiko wako usiwe mzito sana au mwepesi sana.

Baada ya hapo onja kama kila kitu kimekolea.

Bandika chuma cha kupikia chapati (fry-pan) jikoni huku moto ukiwa wa wastani.

Weka nusu kijiko cha chakula cha mafuta ndani ya fry-pan kisha yatandaze.

Hakikisha chuma kinapata moto na mafuta yamechemka halafu weka upawa mmoja uji wa chapati na uutandaze mpaka uwe flati.

Subiri mpaka chapati ikauke juu kisha igeuze upande wa pili weka mafuta kijiko kimoja kikubwa cha chakula kwa upande wa chini na wa juu kisha uanze kuikandamiza kwa juu na kijiko ili iweze kuiva vizuri kwa chini.

Endelea kugeuza ukiona imebadilika rangi na kuwa ya brown itoe na uweke kwenye sahani, endelea kufanya hivyo mpaka umalize na hapo chapati zako zitakuwa tayari kuliwa.View attachment 2205208
Hizi navyozipenda labda mtu anipikie,maana kama ninapika mwenyewe zitaishia jikoni,ukitoa moja unaila unaendelea na ya pili,mpaka nimalize kupika hakuna chapati...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom