Jinsi ya kupenda kwa vitendo

Jinsi ya kupenda kwa vitendo

neha mimi

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
344
Reaction score
152
Kama ilivyo mambo mengine kuwa "affection" ni swala la kujifunza, baadhi ya wanaume waliokuzwa/kulia kwenye jamii yenye mfumo Dume (Waafrika kwa ujumla) huwa hawajui kuonyesha hilo hitaji, embu tuliite "kupenda kwa vitendo" hivyo huenda sio kwamba hataki bali hajui.

Kwa maana hiyo sio mbaya ikiwa wewe mwanadada ukamfundisha nini cha kufanya, ikiwa na wewe ulikuwa huji basi jifunzeni wote ili kuwa una uhusiano bora wenye furaha. Mpaka hapo umeelewa nazungumzia nini sio? Sasa Ili kufupisha maelezo nitaorodhesha mambo machache ambayo wanawake wengi huwa tunapenda kufanyiwa (kiujumla ukiachilia mbali utofauti wetu) ili tujue kweli tunapendwa kihisia na kivitendo.

1-Hakunakitu wanawake tunazimia kama kukumbatiwa nakupigwa busu mara kwa mara.

2-Kabla hujakurupuka kitandani hakikisha umekumbatia na kubusu hata kama kalala (hakuna raha kama kuamshwa na busu au mkumbatio).

3-Mwmabie jinsi gani unampenda na unavyopenda chapati/mayai/viazi alizopika au hata jinsi alivyoandaa mlo wa asubuhi.

4-Wakati unatoka ndani kumbatia chap-chap na busu kiduchu ndio utokomee kazini, hata kama mnatoka wote kwenda kwenye kituo cha daladala unafanya hivyo kabla hujakanyaga vumbi la nje.

5-Onyesha unajali kwa kumjulia hali kwa sms au sauti mara baada ya kufika kwenye mihangaiko yako na vilevile kumbuka kufanya hivyo kabla hujaondoka eneo la shughuli zako pia hakikisha unamueleza utakuwa saa ngapi nyumbani au kama kuna mahali unapitia basi mfahamishe utakuwa huko kwa muda gani n.k.

6-Ufikapo nyumbani kumbatia na busu mdomoni sio shavuni, badala ya kukimbilia kusema yaliyojili huko utokako.

7- Mnunulie vijizawadi mara kwa mara, wazaramo hununuliwa Khanga au hereni na mikifu ya dhahabu, Wazungu hununuliwa maua, kadi au vidani vya madini tofauti, kuna wengine ukipeleka kitoweo (aina ya nyama) basi umemaliza kezi mwana mama anafurahi kweli- kweli sasa wewe fanya kile unachomudu………..hey sio kila siku wala kila mwezi.

8-Msaidie kusafisha mez/jamvi mara baada ya mlo wa jioni, ikiwa umechoka hata yeye kachoka pia hivyo mkikutana nyumbani mna-share kufanya usafi ili kuokoa muda.

9-Lolote litakalo tokea kila la kheri, lakini hakikisha unabusu na kukumbatia kabla hujaanza kukoroma. Kila la kheri katika hili.

Nb: nmecopy na kupaste ......enjoy
 
10. Mwanamke anapendwa kupewa pesa, mpe pesa kila wakati, ukiamka asubuhi kabla ya kumsalimia mpe pesa, atakupenda daima, hili la muhimu hayo mengine hapana
 
7777.jpg
 
Ukitaka mwanamke akupende mpe pesa, mpe pesa, mpe pesa asubuhi,mchana na jioni,mpe ukiamka,mpe kabla hujalala,ukiwa kazini mtumie kwenye M-PESA we mpe pesa, mpe tuuuu mpaka!Mpe bila kuchoka,ukiishiwa kopa mpelekee yaani atakupenda kufa! kama uwongo Miss Chagga athibitishe hili!

Yaan sikufichi hakuna mapenzi bila pesa!

DONE!
 
 
Last edited by a moderator:
10. Mwanamke anapendwa kupewa pesa, mpe pesa kila wakati, ukiamka asubuhi kabla ya kumsalimia mpe pesa, atakupenda daima, hili la muhimu hayo mengine hapana

Sio wote , binafsi sikubaliani nalo. Kwangu Mimi-sijali hela zako , nathamini sana upendo, ukiweka hela , na Mali zako mbele kuliko upendo usushangae nikikuachia vyote bila hata kujali. Kama hela na Mali hata mimi pia naweza kuzitafuta, na nirahisi kuvipata , but Love not easy to find it .
 
Mpe makofi mara tatu kwa siku atakuwaza sana hii ndo njia mubadala.
 
10. Mwanamke anapendwa kupewa pesa, mpe pesa kila wakati, ukiamka asubuhi kabla ya kumsalimia mpe pesa, atakupenda daima, hili la muhimu hayo mengine hapana

Ha ha ha ha ha h ha ha..
.
 
10. Mwanamke anapendwa kupewa pesa, mpe pesa kila wakati, ukiamka asubuhi kabla ya kumsalimia mpe pesa, atakupenda daima, hili la muhimu hayo mengine hapana

we ndo umesema, wengine woote naona wanatiana moyo tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom