Jinsi ya kuondoa msongo wa mawazo

Mwanambugulu

JF-Expert Member
May 26, 2017
666
814
Wakuu habari za muda huu?
Niende moja kwa moja kwenye mada mimi ni kijana wa late 20's nilimaliza shule mwaka 2014 lakin paka leo sijapata ajira rasmi zaidi ya kuunga unga tu na mission town za hapa Dar es salaam

Mzee wangu ni mkulima pia mama ni mkulima nina dada na ma kaka bahati mbaya wote walikimbia umande (shule) basi mimi tu ndio nilichomoka kwenye familia nikafika paka chuo sasa mzee alikua na matumaini sana na mimi pia na ndugu wengine ni kama walielekeza sana matumain yao ya mafanikio kwangu.

Kama unavyojua kwa familia zetu za wakulima huko ni kwamba ili uonekane msomi basi inabidi ukimaliza shule upate kazi alafu usaidie issue kidogo za home

Sasa wakuu mimi nimehangaika sana kupata ajira huwa naishia kupata zile za mikataba miezi mi tatu lakini mwisho hakuna kitu na malipo yake hayakizi kabisa(saizi hata hizo sizipati yena).Nimepiga vibarua hadi na watu wa darasa la saba viwandani lakin pesa unapopata unaishia kula na kodi tu

Nimesambaza cv katika makampuni kibao (auditing firm) za Dar lakin paka leo naona kimya pia mabenk na sehemu zingine lakin kupata ajira imekua ngumu sana

Nime fight sana angalau nipate mtaji basi nifanye hata biashara lakin familia ninazotokea ( pamoja na familia za ndugu) wote kwanza ndio wanasema bora umesoma sasa utusaidie na ww

Nikiangalia home hali ni mbaya sana sasa kimbembe kipo saizi hapa nadaiwa kodi mwezi ujao alafu ndani pia misosi imekata kabisa pia baya zaidi pesa hata nauli ya kutoka ili nizunguke imekata kabisa nimebaki home tu.

Nazunguka viwanda vya karibu kidogo hapa angalau nipige mzigo nipate hata hela ya gesi nako wiki hii wamenizingiua vibaya yani wanaita watu kwa kujuana bahat mbaya mimi sina ninae mjua

Juzi nimepiga dili kwenye kiwanda cha kufyatua matofali aisee nimekimbiza mzigo kuanzia asubui paka saa kumi na moja beba sana matofali nikaja kuramba elfu kumi jioni lakin nimeamka naumwa vibaya sana paka sijielewi yani

Mbaya zaidi nikiwaangalia washikaji zangu ambao tulikua tunapiga msuli pamoja aisee wameramba ajira saizi maisha smooth kabisa yani wanafunga ndoa tu alafu mi nikucheki geto cha muhimu ni kitandani tu labda na ka kompyuta kangu mana kuna madini

Sasa wakuu kwa waliowahi kukutana na changamoto kama hizi hivi mliwezaje kuzitatua? Mana hapa nina mawazo kiasi kwamba mda mwingine nawaza hadi najiogpa

Mbaya zaidi nilikua na rafiki wa kike (girlfriend ) wakati wote hatuna mission ilikua poa bahati nzuri akapata kazi mkoani basi ahadi kikawa nyingi pia alikua ananipaga tafu sana ila baada ya kama miezi 6 hivi mambo yakabadilika akawa hasomeki tukawa tunawasiliana tu hivo hivo ila ghafla simu yake ikawa haipatikani mwezi uliopita nimeona picha za harusi yake

Usiku silali aisee kichwa kinauma pia naweza Kuhisi njaaa lakini mda mwingine najikuta nimekata hata masaaa 18 bila kutia kitu na niko fresh tu

Nikiangalia matumaini wakati nasoma daah pia nikiangalia wanavyonichukulia kule home mkoani na mategemeo yao basi napotea kabisa
Ushauri wenu wakuu ili niweze kujikontroll angalau hata nipate usingizi mana situmiii kilevi chochote sasa usiku unakua mrefu sana alafu mchana ndio natembea kama chizi vile sielewi napishana na watu siwaelewi wengine hata siwaoni

Vyeti vinapata vumbi tu pia mtaji ndio hakuna daaah. Wakuu hebu nipeni ushauri nipunguze huu msongo wa mawazo
Nawasilisha,,
 
Pole sana,kwanza mshkur Mungu kwa kila jambo kwasababu wapo ambao hata kitanda hawana ila wanaishi
Muombe Mola sana na usikate tamaa amin hata hao waliopewa bac vimetoka kwake hvy utapata tu uvumilivu na jitihada ndo vinahitajika bila kusahau maombi zaid
 
Mbaya zaidi zipo nyingi sana, pole mkuu!
Hii kitu sitaki kuisikia kabisa inafanya nisipone vidonda tumbo
 
Qualifications zako plz,jaribu kuweka vitu wazi hapa unaweza pata msaada hata hapa,
 
Pole sana,kwanza mshkur Mungu kwa kila jambo kwasababu wapo ambao hata kitanda hawana ila wanaishi
Muombe Mola sana na usikate tamaa amin hata hao waliopewa bac vimetoka kwake hvy utapata tu uvumilivu na jitihada ndo vinahitajika bila kusahau maombi zaid
Shukrani mkui kwa ushauri
 
Qualifications zako plz,jaribu kuweka vitu wazi hapa unaweza pata msaada hata hapa,
Mkuu nina bachelor of taxation from institute of finance management (2014)

Pia nguvu za kutosha kufanya kazi yoyote ile na eneo lolote lile kwa uwezo wote

Uzuri sichagui kazi kabisa
Pia ni mwaminifu na mchapakazia
 
Fanya hivi

Jisajili kwenye site yoyote ya freelance huku unaendelea kupiga hizo kazi za kitaa mdogo mdogo.

Hapa mwanzo lazima uwe focused

Mamia ya kampuni yanatafuta virtual assistance.

Tumia ujuzi wako kusaidia watu wanaohitaji muda na ujuzi wako.

Watu wanatengeneza $600 - $1000 kirahisi tu kama unajua unachofanya.

Usiwe na lengo la kuwa na chanzo kimoja cha mapato jitahidi uwe navyo hata vitatu.

Usiwazie chapaa mob kwa mara moja.

Kwamfano source number one unaingiza $3

Source number two unatengeneza $2

Source number three $4

Hapo tayari una $9

Hiyo ni Tsh 20,000 kwa siku.

Ukiweza fikia hilo lengo anza kuwa na njaa zaidi.

Tafuta njia nyingine. Hata kama ni kidogo kiasi gani.

If you are best at small things you will be good at large things.

Acha kuwazia hizi kazi za kibongobongo umezoea.

Leo upo kazini kesho boss kakasirika kakufukuza unaanza hangaika na kulaumu life.

Mimi toka nimemaliza elimu uchwara sijawahi omba kazi sehemu yoyote.

Na husle tu.

Nakutakia kila la kheri.
 
hongera kwa kuwa mstahimilivu na kaza mkuu, mi sikupi pole.

Kuna wakati unatakiwa kuweka vyeti ndani, na kuomba kazi ya ujumla, mfano
*juzi kati red cross walitangaza nafasi, ile ilikuwa fursa tosha maana kuna nafasi hazihijaji vigezo vya kitaaluma sana.
*restaurants nyingi wafanyakazi wanasumbua sumbua, tumia hiyo nafasi kuomba kazi popote hata kuhudumia wateja, baadaye haohao wateja wanaweza kuwa chanzo cha wewe kupata deal jingine.
*mtaani kuna vikundi vya vijana vilivyosajiliwa na vinakopesheka, unaweza tafuta kimoja ujiunge kama njia ya kutokea.
*badala ya kuchat sana mtandaoni, tumia mda kupitia sites za ajira,bila shaka unazifahamu mbili tatu kila baada ya siku kadhaa kuona updates.
* jifunze taaluma mpya kila siku ukiwa free kwa kutembelea workshops tofautitofauti za watu na kujenga nao urafiki.

hasta la vista
 
Wait umesoma Tax ? haki utaendelea kulalama labda ukajiajiri!
 
Uswauri mwingine wakukusaidia tu.

Anza kuuza vitu ambavyo uko navyo lakini hivihitaji.

Hapo ndani kwako kuna nini?

Uko na viatu havijaisha sana na huvivai?

Uko na chochote usichotumia?

Uza.

Nakwambia watu wanafikiri haiwezekani lakini inawezekana sana tu.

Ukipata chapaa kidogo nenda sehemu wanauza vitu bei rahisi nunu halafu uza kwa bei ya juu.

Watu watanunua tu. Muhimu uwe na "jicho" la kujua bidhaa watu wanahitaji

Lenga kwenye product inayotatua changamoto za wateja unaowalenga.

Kama umwemwona mtu amevaa shati kuukuu na wewe una shati zuri lakini hulivai mshawishi umuuzie.

Jifunze kuwa seller.

Usijiaminishe na hiyo elimu uchwara uliyonayo.

Hii njia yakujifunza kuuza inaweza tengeneza spirit ya ajabu siku moja ukawa mfanya biashara.
 
Nashukuru mkuu kwa ushauri mzuri
Lakin samahani sana unaweza kuniwekea japo site mbili tatu mana sikua nafahamu hili swala kabisa
Shukrani sana
Fanya hivi

Jisajili kwenye site yoyote ya freelance huku unaendelea kupiga hizo kazi za kitaa mdogo mdogo.

Hapa mwanzo lazima uwe focused

Mamia ya kampuni yanatafuta virtual assistance.

Tumia ujuzi wako kusaidia watu wanaohitaji muda na ujuzi wako.

Watu wanatengeneza $600 - $1000 kirahisi tu kama unajua unachofanya.

Usiwe na lengo la kuwa na chanzo kimoja cha mapato jitahidi uwe navyo hata vitatu.

Usiwazie chapaa mob kwa mara moja.

Kwamfano source number one unaingiza $3

Source number two unatengeneza $2

Source number three $4

Hapo tayari una $9

Hiyo ni Tsh 20,000 kwa siku.

Ukiweza fikia hilo lengo anza kuwa na njaa zaidi.

Tafuta njia nyingine. Hata kama ni kidogo kiasi gani.

If you are best at small things you will be good at large things.

Acha kuwazia hizi kazi za kibongobongo umezoea.

Leo upo kazini kesho boss kakasirika kakufukuza unaanza hangaika na kulaumu life.

Mimi toka nimemaliza elimu uchwara sijawahi omba kazi sehemu yoyote.

Na husle tu.

Nakutakia kila la kheri.
 
Back
Top Bottom