Mleta mada umeleta jambo zuri ...Ingawa kuna mapungufu makubwa juu ya ushauri wako wa kumzunguka aliyekusaidia kutatua maswaibu uliyonayo ...Njia ya kuzungukana inaudhi na inaamsha hisia za kumdharau na kumkejeli aliyepoteza muda wake kwa matumaini anafanya jambo likalomwezesha mwisho wa siku akapata chochote , kumbe wewe unamtumia kupata malengo yako kwa khadaa..una mawazo mabaya na hayana tija kwa maendeleo.,nimesema jambo ulilolianzisha ni zuri kwa maana ya kuwa madalali wanamchango mkubwa katika maendeleo na shughuli za kila siku za wanadamu...ndio maana kwenye biashara za kimataifa bila dalali huwezi kufanya biashara ,dalali ana uwezo wa kufanikisha biashara au kuihujumu...iwe hata ndogo kiasi gani...,,..kwa mantiki hiyo ingependeza basi serikali ingelifanyia kazi kwa kuwapa elimu stahiki ya udalali wahusika, na kuweka sheria kwa kuziboresha zilizoko pia wawe na ofisi maalum zitakazokuwa sehemu husika kwa malengo ya kuwatambua madalali halali, kwa mfano kama ni biashara za mboga mboga n.k sokoni kariakoo..au kama ni mahindi, tandale soko la mahindi n.k aliradi kunawekwa mpango mzima wa kuboresha mahitaji baina ya muuzaji na mnunuzi,kumbuka udalali ni AJIRA kamili.. Kazi za udalali zinapaswa kuboreshwa ili kuondoa na hata kuzuia utapeli usiwepo baina ya muuzaji na mnunuzi...