Jambazi
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 16,654
- 18,792
Miaka kadhaa huko Uchina, Binti aitwaye Li- Li aliolewa na akaenda kuishi kwao mumewe na mama wa mumewe.Ndani ya muda mfupi Li-Li alijikuta hana maelewano kabisa na mama Mkwe wake.
Tabia zao zilikuwa tofauti kabisa, walipishana kauli kila mara na Li-Li alichukizwa sana na tabia nyingi za mama mkwe wake. Mbaya zaidi, mama-mkwe alimlaumu na kumsema vibaya Li-Li mara zote.
Kadri ya siku na wiki zilivyopita, Li-Li na mamamkwe wake walizidi kubishana na kugombana. Kilichofanya hali kuwa ngumu sana ni mila kuwa Li-Li alitakiwa kumnyenyekea na kutimiza kila alichohitaji.Ugomvi na kukosekana amani ndani ya nyumba vilimsababishia mfadhaiko na kumyima amani mume wa Li-Li kwani aliwapenda wrote.
Baada ya kushindwa kumvumilia mama Mkwe wake ambaye alinung'unika kila mara na kutaka kuwa ndiye anayefanya maamuzi yote ndani ya nyumba, Li-Li aliamua kwenda kwa rafiki wa baba yake,Huang, ambaye alikuwa anauza Dawa za mitishamba.
Itaendelea.....