Jinsi ya kumrudisha umpendaye

Jinsi ya kumrudisha umpendaye

^^
Wakati mwingine si lazima kurudi 'jana' hata kama moyo unasema hivo, akili inahitajika
^^

Umenena kilichopo akilini mwangu mkuu, kusamehe tunasamehe na kusahau kwa roho safi kabisa, ila kuna fundisho huwa linabaki. Baadhi ya maswali ninayojiuliza:
1. Hata baada ya kurudi, sababu zilizofanya tukavunjika zitakuwa zimeisha?
2. Itawezekana kuvumilia makunyanzi yake sasa kama mwanzo ilishindikana?
3. Naamini huwezi kutarajia matokeo tofauti kwa kufuata mkondo huo huo
 
Nafikiri Wema alitumia hizo njia hapo juu kumrudisha Diamond..by the way ahsante mtoa mada
 
Umenena kilichopo akilini mwangu mkuu, kusamehe tunasamehe na kusahau kwa roho safi kabisa, ila kuna fundisho huwa linabaki. Baadhi ya maswali ninayojiuliza:
1. Hata baada ya kurudi, sababu zilizofanya tukavunjika zitakuwa zimeisha?
2. Itawezekana kuvumilia makunyanzi yake sasa kama mwanzo ilishindikana?
3. Naamini huwezi kutarajia matokeo tofauti kwa kufuata mkondo huo huo
Tunda la roho ni uvumilivu endapo unampenda bado,mtu anapokuja kukuomba msamaha na kutaka yaishe huwa unaelewa nini? kama umemfumania na ameomba msamaha kwamba ametambua thamani yako wakati huo huo na wewe unampenda kuna sababu gani ya kumkatalia? kuna watu wanaachana wakiwa kwenye ndoa lakini wanarudiana na maisha yanasonga watu hubadilika kutokana na mazingira na wengine hufanya maamuzi kwa hasira pasipo kufukiria ila kama na wewe moyo wako umemkinai basi huna budi kusonga mbele
 
Ndugu yangu kuna sababu nyingi zinasababisha watu wanaachana bila kupenda wao wenyewe ama kwa hasira na wivu uliopindukia,usije kila wanao achana wamechokana hapana,mimi mwenyewe ni mmoja wapo nilikuwa na mwanamke nilimuacha kwa sababu ninazozijua mimi ila nilikuja kugundua nilifanya makosa kwani ananipenda sana yuko tayari kufanya lolote kwa ajiri yangu siku nilipomuita na kumwambia lengo langu alilia sana kwa uchungu kwamba nimemtesa kipindi nilichokuwa nimemuacha na saizi tuko pamoja maisha yanaendela ni mwaka mmoja na nusu toka tulipofungua ukurasa mpya.

hongera sana
 
Sasa ngoja nifanye mchakato wa kukurudisha wewe kwanza....
 
Wapenzi wangu wote walikuwa manunda.

Hata ufuate step zote hizo lakini haifui dafu.

Ni kutafuta mwingine tu
 
^^
Ujue kila ulichoandika hapo juu ni mashauri mema kabisa, kuna mwanamke niliyempenda, ninaempenda na hata daima nitampenda! Lakini kwa ushenzi alionifanyia siwezi kurudi nyuma. Niko tayari kurudi kwa Mungu nikiwa single ikiwa tu ndiye aliyepangwa awe wangu. Vinginevyo aheshimu tabia na msimamo wangu
^^

mshikaj unahasira wewe
 
Do you mean to say we are unemotional??tactless??coz philosophical z so wide/general

^^
Not that way! Being philosophical is just an interpretation of those around you!
It happens because of straight forwardness in speaking (not tactful), of how you choose to tell truth that sounds like a bitter remark! Sometimes you may be regarded as unemotional but truth inside you is, you know how your cool, loving, caring, soft and of endless charming nature! Being philosophical is just used to keep your internal safe
sonnita
^^
 
Last edited by a moderator:
Habari ya muda huu wapendwa, bila kupoteza muda tungie kwenye maada kama kichwa kinavyojieleza

Kugombana ni sehemu ya maisha ya binadamu yawezekana kabisa ulikuwa na mwenzi wako ambaye ulimpenda kwa moyo wako wote na sasa mmeachana. Kutengana kuna mambo mengi, wakati mwingine ilikuwa hasira tu.

Siku zote baada ya hasira kuisha, moyo hubaki peke yake katika nafasi yake halisi ya kufanya maamuzi. Hapo ndipo kwenye lengo la mada yetu ya leo. kwamba kwa msingi huo umegundua kwamba kumbe mpenzi wako uliyeachana naye, bado unampenda.

kwamba hata makosa aliyokuwa akiyafanya, ulimsababishia au si makubwa kiasi cha kuachana na badala yake mnaweza kukaaa na kuzungumza kiutu uzima na kuyamaliza.

Baadhi ya watu huamini kwamba kurudi kwa mara nyingine kwa mpenzi wa zamani ni kujidhalilisha, kujishusha na kujisalimisha. kwamba hakuna mwanaume wala mwanamke mwingine yeyote atakayeweza kuwa naye tofauti na huyo anayemrudia.
jambo hilo si la kweli hata kidogo, kikubwa cha kuzingatia hapa ni moyo; je, unahisi bado unampenda? ni kweli naye anakupenda? kama sifa hizi zipo, hayo mambo madogo ambayo mmetofautiana ni ya kawaida kabisa ambayo mnaweza kurekebishana taratibu. Zifuatazo ni njia zinazoweza kukusaidia kumrudisha mpenzi uliyeachana naye na bado unampenda

1.Chunguza alipo
Kitu cha kwanza kabisa ambacho unatakiwa kuchunguza ni mahali anapopatikana kwa wakati huo, nasema hivyo kwa sababu yawezekana alihama makazi, kikazi n.k. kujua anapopatikana ni mwanzo wa kuelekea kwenye mafanikio ya kumkamata katika himaya yako.

2.Historia yake baada ya kuachana
Lazima ujue kuhusu historia yake kiuhusiano baada ya kuachana na wewe. hapo unatakiwa kufanya ‘ushushushu’ wako kimyakimya bila yeye kujua. ikiwa ameshafanya ‘vurugu’ sana, maana yake ni mtu asiye na msimamo na huenda anaongozwa zaidi na tamaa za kimwili na si mapenzi.
katika kipengele hiki, ni muhimu sana kujua kama muda huo ambao wewe unahitaji kurudi tena mikononi mwake kama ana uhusiano mwingine. kimsingi kama atakuwa ndani ya uhusiano, itakubidi uhairishe zoezi lako.

3.Mawasiliano
Ukishachunguza mahali alipo na kuridhika na historia yake ya kimapenzi baada ya kuachana na wewe, sasa unatakiwa kutafuta mawasiliano yake. 
kupata mawasiliano yake ni hatua ya kwanza, kitakachofuata baada ya hapo ni kujenga mawasiliano. hapo sasa inategemea na namna mlivyoachana, lakini kama hamkuwa na ugomvi mkubwa sana, basi unaweza kumtumia meseji za kichokozi mara nyingi uwezavyo kwa siku.
majibu yake ndiyo yatakayokupa mwanga wa kuendelea na kipengele kingine. kikubwa hapa ni kutozungumzia kabisa mambo ya mapenzi, badala yake iwe ni kumjulia hali na utani wa hapa na pale.

4.Mpe mwaliko

Baada ya kutengeneza mawasiliano naye, sasa unatakiwa kumwalika katika shughuli mbalimbali za kifamilia na binafsi. mathalani umepata mwaliko wa kwenda kwenye sherehe au hafla fupi ya usiku, omba kampani yake. kama mtu mzima atagundua kitu kilichopo moyoni mwako. hata kama atakuwa mwenye moyo wenye kutu, kutoka naye mbele za watu, kutamfanya akumbuke enzi zenu mlipokuwa mkitoka pamoja, hivyo kufikiria kurudi tena kwako.
ikiwa ataamua kukuambia kwamba anaona mrudiane litakuwa jambo zuri zaidi, maana atakuwa amekurahisishia, lakini akinyamaza, basi njia inayofuata hapa chini ni muafaka kwake.

5.Mvute karibu yako
Sasa unatakiwa kumsogeza karibu zaidi na wewe. lazima afahamu kwamba, kuna kitu fulani kipo ndani ya moyo wako. meseji zako zibadilike, kama ulikuwa unamwandikia, “vp uko poa?” au “mambo yanaendaje?”, sasa unatakiwa kubadilisha hadi “niambie sweetie, uko poa?”
meseji za aina hiyo zitamfanya aone tofauti na inawezekana kabisa akagundua kwamba upo kwenye mawindo ya kumrudisha tena kwako. katika hatua hii katu hutakiwi kufungua mdomo wako kumwambia kuwa unataka kurudiana naye na badala yake unatakiwa kuacha vitendo vizungumze vyenyewe.

6.Jadili penzi lenu
Hatua hii ndiyo muhimu zaidi hapa; sasa unatakiwa kuanza kuzungumzia juu ya uhusiano wenu. mwambie jinsi ulivyokuwa ukifurahishwa na mapenzi yenu. msifie alivyokuwa anajua majukumu yake na kukuonesha mapenzi ya dhati.
si vibaya kama utamweleza pia sababu ambazo unahisi zilisababisha wewe na yeye kuachana. Kwa kauli hizo utampa nafasi ya kuchambua/kumjua mwenye makosa na mahali pa kurekebisha.

7.Mweleze yako ya moyoni
Sasa huna sababu ya kuendelea kujitesa, toa dukuduku lako, mwambie moja kwa moja kilichopo moyoni mwako kwamba unahitaji nafasi nyingine kwake, maana umeshajua makosa yako.
hii ni nafasi ambayo si rahisi kabisa kuchomoka. itumie vilivyo sauti yako pekee itoshe kumaanisha kile kilichopo moyoni mwako lazima atakuelewa.
Kama utakuwa umefuata kwa makini vipengele vyote hapo juu, lazima urudi tena mikononi mwake. kuna nini tena? ameshakuwa wako huyo, ila kuwa makini usimpoteze tena.

Akikataa je?
pamoja na kufuata vipengele vyote hivyo, inawezekana akakataa. kukataa kwake lazima kuna sababu nyingi. mwingine anaweza kukuambia moja kwa moja sababu za kukataa kurudiana na wewe wakati mwingine anaweza asiseme chochote.

Huenda akakuambia kwamba tayari ana mtu wake, au hafikirii kurudi mikononi mwako; usihuzunike.
ni bora sana huyu anayekuambia ukweli, kuliko kurudi halafu ukutane na mateso yale yale.inawezekana labda hana mapenzi na wewe. kama ndivyo, kuna sababu gani ya kujikomba? kubaliana na ukweli, halafu subiri mwingine!
sikia, subiri mwingine na siyo utafute, maana mwenzi wa kweli huja mwenyewe, hatafutwi

Zingatia:
Mara nyingine kugombana kwenye mahusiano hakumaanishi ndiyo mwisho wa mahusiano ila kunaimarisha mahusiano hayo mnawea mkaachana kwa muda fulani na kuweza kurudiana.Mpende akupendaye na wala usimtese anayekupenda eti kwa sababu umemuweka kiganjani akikupokonyoka hapo ndiyo utagundua kuwa hukutakiwa kumuweka kiganjani bali moyoni Enjoy your time
Umetiririsha maelezo kama unatupa funzo la mapishi fulani,hah!
 
Back
Top Bottom