Mzuka wana Jamvi!
Wimbi la watu kuombaomba hela Sana (wapiga mzinga) limeshika kasi. Japo Kuna wengine kweli wahitaji ila asilimia kubwa imeshakuwa tabia. Utakuta wengi wao Ni wachezaji kamari/kubet Na pia hawana nidhamu ya matumiz ya pesa zao. Wengine hawaishi Na kuridhika Na vipato vyao. Wengine wanaona hela yako haina kazi Na Ni haki Yao uwagawie.
Ukimuona mpiga mzinga anakuapproach, kukusogelea ama kukufuata Yani muwahi faster Na mapema kwa kumkunjia uso Wala usimchekee kuwa mkali hata ukiweza utoe neno la ukali "usinisogelee". Ukifanya hivi utakuwa umemwin kisaikolojia na ataacha kukusumbua.
Wanatabia ya kukuchekeachekea toka mbaali bila sababu Na wakikukaribia wanakushobokea Na kukusifuu sana. Wengine watakuita dogo hata Kama unalingana Na Lemuuz.
Ila Kuna watu Ni wahitaji kweli utakuta mtu ana njaa anakuomba hela ya kula utakachofanya nenda naye dukani ama sokoni umnunulie msosi wa elfu kumi. Ukiombwa nauli umuulize unaenda wapi akikuambia ongozana naye Hadi kwa konda umlipe konda. Kama kweli mahitaji yake ya kweli ilikuwa chakula ama nauli hataona aibu.
Kuna watu kwenye jamii wanatabia mbaya sana ya kuombaomba hela Yani wanapiga mizinga balaa Na utakuta wanafanya Kazi nakulipwa mishahara. Yani kukaa Na kupigia mahesabu Na bajet hela za wengine siyo vizuri.
Hela Ni kitu Cha thamani Na inapatikana kwa kujituma Na kufanya kazi Iwe kwa weledi ama bidii.
Nidhamu ya matumizi ya hela Ni muhimu ndio chanzo Cha maendeleo katika Familia, Jamii Na nchi.