Jinsi ya kum-handle kijana aneanza balehe

Jinsi ya kum-handle kijana aneanza balehe

Jalibu kuwa mkali somtime kama hataki kutumia simu ya kawaida mkanye kwa ulimi mkali kidogo ikiwezekana mpeleke kwa mwalimu wake na umweleze kilichotokea ikiwezekana kuwa mkali na usimpe simu tena, atazoea tu usimdekeze sana litakuja kuwa tatizo kubwa, smat phone kwa mtoto kama huyo ya nini, na nyie mstake kujitia matajiri bana watoto wenu mnawaharibu wenyewe! Shauri yenu atakuja kuchora mazombi kwenye peper we mdekeze tu.

Sio utajiri ila nilikuwa na access ya kuipata hiyo simu ndio maana nilimpa
Ntajitahidi nitumie ukali japo hatukuzoeshana hivyo kutokana hapo mwanzo hakuwa mtoto mwenye makosa sana ilikuwa ukimkanya jambo anakusikia na harudii but sasa amebadilika
 
Taratibu za malezi ni kama ifuatavyo:

Mtoto hugombwa kuanzia miaka 2-hadi 7
Hupigwa kuanzia 7-hadi 14
hufanywa rafiki kuanzia 14-21 na
Hufanywa mshirika wa maisha kuanzia 21- na kuendelea.

Sasa mwenzetu upo katika stage ya 3...stage hii hutegemea vipi ulizianza mbili za mwanzo...kwa uwoni wangu ni kwamba ulimpenda kupita kiasi huyu mtoto....nakubali ni kwa sababu ya kua hakua na mama...na wewe ukamhurumia sana...

Ok what is the way forward?

Cha kufanya sasa ni kwamba huna haja ya kushuhulishwa na kununa kwake..cha misingi kua firm na kua mkali kama kawaida au umeshahu usemi usemao...huruma hailei mwana?...Mwache asicheke na asile...atakula tu uyo chezea njaa wewe?....Kuhusu tatizo la kubalegh..na kuanza mchezo wa baba na mama...inakubidi kumuingiza mwanao katika program za dini na umueleze ubaya wa kufanya mapenzi katika umri mdogo.....maana ya dhambi na vitu kama ivyo...kiufupi ni ngumu kwa sababu udongo upate ulimaji...

Asante sana kwa ushauri wako na ni kweli nampenda sana huyu mtoto myb hilo ndiyo inamapa kichwa
Sasa nambadilikia kiasi itanibidi niwe mkali haswaa na amri itawale
 
Miaka Hui kulea in kazi sana lakini nasi wazazi no tatizo pia. Hataki simu ya to hi name ukaona no saws? Mwanzo was Ngoma in lele usimchekee maana Hugo hajui ulimwengu salsa ulivyo..
 
Yaani ninavyomlea ni kama mtoto wangu wa kuzaa swala la kutokuwa mtoto wangu alipo kabisa
Kuna kipindi aliomba nimnunulie simu nikamajibu ukifanya vizuri zaidi shule ntakununulia....sasa alivyofanya vizuri nikatimiza ahadi yake ya simu aliyokuwa anaitaka sikuwazia kama anaweza itumia vibaya

Hata mimi nilipokuwa darasa la tano nilikamatwa nimeandika barua ya mapenzi nikachapa mbele ya darasa......... Ilinifedhehesha sana ila kawaida nina strong personality toka kitambo , haikuniathiri kwenye masomo wala maisha yangu ya shuleni na nilikuwa nina akili sana(namba moja darasani kila term).

Ninachotaka kusema kuna namna fulani ya approach inafedhehesha kwa mtoto , ni vizuri umjengee mwanao utamaduni wa kuwa na strong personality , ajue msimamo wako unapomuelewesha kipi kipo sahihi na kipi hakipo sahihi kwa umri wake.

usisahau kuangalia aina ya marafiki anaokuwa nao (usimchagulie marafiki) , ila kuwa mjanja kumtenga na marafiki wa hovyo kwa mbinu za kiutu uzima.

na mwisho lakini cha muhimu , kumlea mtoto katika maadili ya dini na kuwa na Hofu ya Mwenyezi Mungu itamsaidia sana katika kuelekea njia ya mema. (hii inategemea na dini yake zaidi).
 
a4.JPG

Changu mimi ni haka kana miaka 4 huaga nakafinyafinya...mama hua anakatishia kuwasha moto wa kiberiti...kana disipline kiasi
 
na mwisho lakini cha muhimu , kumlea mtoto katika maadili ya dini na kuwa na Hofu ya Mwenyezi Mungu itamsaidia sana katika kuelekea njia ya mema. (hii inategemea na dini yake zaidi).[/QUOTE]

Naanza sasa kumuwekea malezi ya dini naamini akiwa na hofu ya mungu italeta wepesi
 
Naanza sasa kumuwekea malezi ya dini naamini akiwa na hofu ya mungu italeta wepesi

nakutakia kila la kheri upate wepesi kwenye hilo..........

N:B; vipi ile ishu yetu lakini , mbona unaniacha peupe sikuelewi ujue.
 
Dah mitoto ya siku
Hizi inadekezwa jamani duh
 
Toto hili litakuja sumbua mno maofisini..linaona 'privilege'ni haki yake...
 
Si vizur kumpa mtt simu yenye internet
hata wtt wa obama mpaka leo hii hawarusiw kutumia internet na mama yao
 
Kanaonekana

mamii, huo umli alionao kuandika barua za mapenzi ni jambo la kawaida na natural kwa sababu keshaanza kuwa na hisia. katika umri huo niliandikiwa barua nyingi na watoto wa umri huo, pia niliandika pia, ni jambo ambalo lipo na haliepukiki. cha muhimu ongea nae kuhusu mapenzi na limitations kutokana na umli alio nao yaani asijihusishe na ngono, ajue kwamba ngono ni dhambi, pia anaweza pata magonjwa (mweleze aina ya magonjwa ) mweleze pia anaweza kumpa msichana mimba na ndoto zake zikaharibika(hakikisha unajua anapenda kuwa nani) kama kuna picha za waathilika waweza mwonyesha. kama mkristu fatilia vipindi gani vya vijana vimapatikana kanisani mshawiashi awe anaudhulia. kwenye simu usimpe tena smartphone subiri umli usogee. usitumie ukali sana haitasaidia sababu ataendelea kufanya siri usijue na matokeo ni mabaya sababu atapata information ambazo si sahihi kutoka kwa marafiki na vajana wengine zitamwalibu zaidi.
 
Back
Top Bottom