Jinsi Ya Kujichunguza Dhidi Ya Saratani Ya Matiti Na Korodani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi Ya Kujichunguza Dhidi Ya Saratani Ya Matiti Na Korodani

Discussion in 'JF Doctor' started by X-PASTER, Dec 5, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Jinsi Ya Kujichunguza Dhidi Ya Saratani Ya Matiti Na Korodani

  Video hizi hazijapachikwa hapa kwa kuwa zina zuio la umri. Kila atakayetaka kuziona hana budi kujisajili na umri wake kuonesha kuwa ni zaidi ya miaka 18. Bofya linki zifuatazo kwa maelezo zaidi.

  1. Video inayoelekeza jinsi ya kujichunguza matiti inapatikana:


  2. Video inayoelezea jinsi ya kujichunguza korodani inapatikana:  3.Video zinazoonesha jinsi ya kujichunguza mwanaume dhidi ya saratani ya matiti: youtube bofya hapa.

  Pengine utauliza, ni kwa nini mwanaume ajichunguze matiti? Angalabu watu wengi wamekuwa wakidhani ni kejeli na mzaha kwa wanaume kujichunguza matiti lakini ukweli ni kuwa, saratani ya matiti pia huwapata wanaume na mara nyingi hugundulika inapokuwa imefikia hatua ya mbali kabisa isiyoweza kutibika.

  Kwa hivyo, ingawaje idadi ya wanaopatwa na saratani hii ni ndogo, bado haitoshi kuwa sababu ya kupuuzia kwani anapodhurika mtu mmoja, ni huzuni kwa familia nzima na wote wanayomzunguka, na, ikiwa kinga ni bora kuliko tiba, ya nini basi kuyaonea maradhi aibu hadi kifo kikuumbue?

  Wakati mwingine madhara makubwa yanayotupata hutokana na aibu kwa misingi ya mila na destruri zetu. Mtu anahofia kuchekwa kwa kujichunguza na kuuliza maswali yanayohusu masuala ya "sirini" na kuwa radhi kufa kwa ugonjwa kuliko kuchekwa. Hatima yake ni aibu zaidi wakati wa ugonjwa, kilio na kuacha wosia.

  Masuala haya hayazungumziwi na katika kuyafumbia macho, yamekuwa sababu ya ongezeko la vifo vya magonjwa ya zinaa pamoja/au na saratani Common Cancer Types - National Cancer Institute.

  Katika orodha ya vifo vinavyotokea zaidi katika nyakati za sasa duniani, saratani imeshikilia nafasi kubwa, hasa saratani ya matiti, viungo vya uzazi kama vile matiti, shingo ya kizazi na korodani, hivyo ili kuongeza ufahamu na kuwahimiza watu kujua afya zao, ni muhimu kukumbushana na kueleimishana jinsi ya kujichunguza.

  Vile vile kazi ni mazoea, na kwa kuwa hii ni sehemu ya mengi ya kutoa huduma kwa wagonjwa, kwangu imekuwa siyo kitu kigeni wala cha kuonea aibu tena, ndiposa, sioni taabu kufikiri na kuweka video kama hizi kwa kuwa ni mojawapo ya elimu muafaka kwa wale wanaopenda kujifunza kabla ya kufika kwa daktari.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Hapa kila mtu atasema ana miaka zaidi ya 18 hata km ni mtoto wa darasa la kwanza ili mradi tu aone kilichomo,
  Asante sana mkuu x-paster!
   
Loading...