Jinsi ya kujenga msingi katika eneo lenye mchwa au vichuguu

Jinsi ya kujenga msingi katika eneo lenye mchwa au vichuguu

Forecaster

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2013
Posts
220
Reaction score
149
Ni mara nyingi kuona baadhi ya nyumba zikipatwa na tatizo la kushambuliwa na mchwa kwenye fdari . Fremu za milango nk. Sasa mimi nataka kujuzwa kwa wataalamu walio na ujuzi,

Je ili kuweza kujenga Msingi wa nyumba eneo lililo na mchwa ni mambo gani muhimu ya kufuata?
 
kuna dawa ya mchwa inauzwa kariakoo, lita moja ni 35,000/=
lita moja huwezwa kuchanganywa na ndoo 6 kubwa za maji.

kabla hujaanza ujenzi wowote ukichimba msingi wa nyumba mwaga mchanga kuzunguka mtaro wa msingi wa nyumba yako kasha mwagia maji kwa wingi halafu chukua hiyo dawa uliyokwisha changanya na maji kwenye huo mtaro wa msingi, dawa inadumu kwa miaka 50,

kwa wale ambao wameshajenga tayari kama hujaweka frem za milango chimba vishimo kwenye vizingiti vya fremu za milango kisha mwagia dawa,
 
Hiyo dawa ya ukweli sana, natafuta kikopo chake nisome jina, inaendelea kuua mchwa mita 100 kutoka eneo ilipowekwa, imenisaidia sana binafsi, na hata wakandarasi wa majengo ya serikali huwa wanaelekezwa kutumia hiyo dawa kwa maeneo yenye mchwa
 
Mkuu si nyumba yetu ni ya muda mrefu na tulijenga mahali panakichuguu na kuna mchwa sanaa naweza tumia njia gani walau kusolve ili tatizo?
mkuu itabidi kuchimba mtaro kuzunguka nyumba mita moja toka kwenye nyumba na mtaro uwe na kina cha mita moja kisha mtafukia hiyo dawa.

Kiongoz hyo dawa inaitwaje ili nikachukue kbs naomba jina lake plz
jina limenitoka kidogo ila ukifika pale kariakoo shimoni (kama upo dsm) ukiulizia tu dawa ya mchwa utaiona na ina maelekezo yote muhimu.
 
Back
Top Bottom