Jinsi ya kujenga himaya na ngome bora

Jinsi ya kujenga himaya na ngome bora

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,231
Jifunze kwenye hili kisha na Mwenzio nae ajifunze kitu
Ili kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako, kupitia kazi au biashara unayofanya, kitu kimoja muhimu sana unahitaji, nacho ni kujenga himaya.

Ni lazima ujenge himaya kubwa ya watu ambao wanategemea sana kile ambacho unakifanya. Watu ambao wanasubiri kwa hamu kupata huduma au bidhaa yako. watu ambao wanajali kweli kwenye kile ambacho unakifanya.

Tumekuwa tunaona wengine wanajenga himaya zao, wanajenga biashara kubwa ambazo watu wanazizungumzia sana, wanafanya kazi bora ambayo inawafurahisha wengi.

Je wewe umeshaanza kujenga himaya yako?

Na unawezaje kujenge himaya hii?

1. Kwa kuwahudumia watu, kuwasaidia watu kutatua matatizo yao, kuwapatia kile ambacho ni muhimu zaidi kwao.

2. Kwa kujali kuhusu watu wale unaowahudumia, kuhakikisha kwamba kwa kukutana na wewe maisha yao yanakuwa bora sana.

3. Kwa kuwasaidia wengine kuweza kujenga himaya zao pia. Kumbuka unachotoa ndio unachopokea.

4. Kwa kuona tayari ile himaya unayotaka kuijenga ipo ndani yako, ipo mikononi mwako na jukumu lako ni kutekeleza.
Ndio unaweza kujenga himaya kubwa ambayo itakuwezesha wewe kufikia mafanikio makubwa. Sio kazi rahisi, ndio maana wachache sana ndio wanaoweza. Na wewe ni mmoja wao, unaweza, anza sasa.
 
Asante sana Galacha Maestro ...Somo zuri sana ..... Nimejifunza kitu cha kufanyia kazi kwa upya
 
Nimeipenda hiyo! ahsante kwa kuamsha hisia za kujenga himaya kwa wana JF
 
Back
Top Bottom