Jinsi ya kuijua asali orginal | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kuijua asali orginal

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Simba Mkali, Jul 18, 2012.

 1. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 595
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45


  TUNAFAHAMU kwamba asali ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binaadamu, lakini watu wengi wamekuwa wakipigwa kwa kuuziwa asali feki, sasa leo nimeona niwape darasa wanunuzi wa asali ili wasiweze kununua asali feki.
  Maana sehemu nyingi hasa Kariakoo, wafanyabiashara wamekuwa wakiuza asali ambayo haina ubora kwa kuchanganya maji na sukari guru.
  Njia ya kwanza, chukua njiti ya kibiriti kisha ichovye sehemu yenye baruti kwenye asali unayotaka kuinunua, kisha iwashe njiti hiyo kwa kutumia kibiriti chako, ikiwaka, ujue hiyo ni asali kweli.
  Njia ya pili, dondosha asali chini katika mchanga, ukiona sehemu ya mchanga iliyolowana ikijikusanya pamoja ujue hiyo nii asali orginal.
  Njia ya tatu, Chukua karatasi jeupe, dondoshea asali njia juu yake, kama ikichelewa kutokea upande wa pili, ujue hiyo asali safi na inafaaa kwa matumizi ya binaadamu.
  Bado kun njia nyingine ambayo hutumiwa na baadhi ya watu, kama vile kuimwaga katika kiganja cha mkono wako, ukiona tone la mwisho linabakia kwenye chupa kuja mkononi, hiyo ni asali, pia wengine huangalia kama ikiwa kwenye chupa huwa inatengeneza alama yenye mfano wa korosho. Nadhani hutaibiwa tena kwa kuuzia asali feki.
   
 2. K

  KWA MSISI Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo anayeuza atakuruhusu ufanye hizo tests zako?
   
 3. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hilo nalo swali, maana mara nyingi inakuwa sealed-labda ungeelewesha vizuri hiyo njia ya ikiwa ndani ya chupa na alama yake ya korosho
   
 4. Lateni

  Lateni JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 685
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Asante kwa somo zuri, japokua kwenye kui test ndio mtihani, muuzaji hawezi kukubali kirahisi, hasa akishajua asali yake ni ya magumashi.
   
 5. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280

  Wa TZ bwana! kila kitu mnakuwa negative.
  Mtu kajitolea kutoa elimu ya muhimu bure, mnaleta ukauz u.

  Haya, ukiona ni sealed kafanyie uchunguzi nyumbani kwako then ukikuta feki ndio urudishe na vigezo ulivyoelekezwa.

  Need we say more ?
   
 6. T

  Teko JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Somo zuri,ila sasa itabidi tu ukubali hasara kwa afya yako,baada ya kuinunua ndipo utest,na kama matokeo ni mazuri endelea nayo,na matokeo yakiwa mabaya usitumie!
   
 7. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Fafanua vizuri ikiwa nani ya chupa. Je kuna asali mbichi na iliyo iva?
   
 8. N

  Nzagamba Yapi Senior Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 168
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Au chukua asali kidogo jipake halafu katiza mahala penye nyuki,ukiona khawakufati hiyo feki

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
 9. m

  msaragambo Senior Member

  #9
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Asante Mkuu
   
 10. m

  maliyamungu JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 481
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  kaka si wabongo tuna matatizo sana kila kitu kujifanya tunakosoa badala ya kushukuru..watu wanaojifanya wajuaji wananiuzi sana
   
 11. salito

  salito JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,366
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  mkuu asante kwa kunielimisha.
   
 12. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Good lesson. Do the tests on your own setting.
   
 13. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 595
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Yaaa, binafsi nimeshatesti mara nyingi tu na wauzaji hawakuwa na matatizo, ila akiwa hataki ufanye testi huyo atakuwa na matatizo kuwa makini.
   
 14. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ni mtihani mgumu kiasi
   
 15. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  asante kwa somo
   
 16. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  "Asiyejua maana haambiwi maana"

  hahahaaaaa,Hakyanani hii ndo JF. Hata siku yako ikiwa mbaya utafurahi tu.Asante mkuu kwa kuniongezea siku za kuishi.
   
 17. Tmlekwa

  Tmlekwa Senior Member

  #17
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  teh,teh,kwel hum jf kuna kila aina ya watu,hata ma-comedian kama ww wapo.
   
 18. 654

  654 Senior Member

  #18
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 173
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Congratulations for the timely information Sir!
   
 19. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha!
  Jf bwana, raha tupu!
   
Loading...