Jinsi ya kufuga dagaa

bigvision203

Member
Nov 1, 2017
35
21
Wa ndugu,

Kati ya samaki wenye mpaka soko la nje ni dagaa na ufugaji wenye uhakika wa soko. Naona watu wanafuga sato na kambale na wale samaki wa mapambo ila bado sijaona wanao fuga dagaa.

Naomba wataalamu wanaojuwa mazingira ya kufugia dagaa,na uwezekano wa kufuga dagaa wanieleweshe natamani kufuga very soon

a0586fa4be129325f1ff9fee9f1ef8ac.jpg
 
huwezi kufuga dagaa dagaa wanatakiwa uwe na eneo kubwa sana.. kama ziwa kabisa.
 
Tatizo ni kwamba hakuna aliyejaribu na inawezekana wataalamu hawajatengeza mbegu,ni kweli soko la dagaa ni kubwa Kama utafiti ukifanyika inawezekana bwawa linaloweza kubeba Sato 500 likabeba dagaa wengi ambao pia wanaweza kuwa wanakuwa kwa muda mfupi kuliko samaki.
 
Na hapa ndo kunaonekana ombwe la wataalam wetu wa kiafrka. Wanaosema hadi uwe na ziwa ndo uwafuge hawajui factor moja kubwa ya dagaa kibiashra kuwa wanawahi sana kukuwa na matured almost 3weeks na ni moja ya samaki wanaozaliana kwa wingi na kwa kasi, so ukiwa na kibwawa chako hata cha kutoa debe moja kwa hizo week tatu ni hela ya maana coz debe linaanza na 10k+ fikilia kuku wa kienyeji unaemfuga hadi awe mkubwa wa kuuza 10k atakuwa ametumia miezi mingapi na atakuwa amekula Chakula cha sh ngapi?.

Mm naona hatuwafugi kwa sababu hawako kwa watu wa kutumia akili wakawezakutumia akili zao na ikawa furusa kwa jamii wakatuletea madesa ya namna ya kufuga ndo wataalam wetu waanze kujinadi na kituelekeza namna ya kufuga.
 
Huwez kuwafuga hao sababu haiwezekan wao kuvuliwa alafu wakafikishwa nch kavu wakiwa hai
 
Kwa Tanzania na duniani kote akuna anaefuga dagaa!! kuna aina zaidi ya 140 za dagaa duniani, Dagaa anapendelea kula mimea bahari, wakati sato anakula mpaka pumba.

Dagaa anachukuwa miezi 12 kufika urefu wa cm 6 mpaka 7. na pia ukae ukijua dagaa vile alivyo ndo amekamilika yaani ndo mkubwa na sio watoto wa samaki. na jinsi walivyo wengi kwenye maziwa na baharini wengi wanaona akuna sababu ya kuwafuga na upatikanaji wa mayai yake pia kutokana na size yao ni shida kiasi!

Nakushauri tafuta boti ya kuvua dagaa uingie ziwa tanganyika uanze kuvua upige pesa
 
Na hapa ndo kunaonekana ombwe la wataalam wetu wa kiafrka. Wanaosema hadi uwe na ziwa ndo uwafuge hawajui factor moja kubwa ya dagaa kibiashra kuwa wanawahi sana kukuwa na matured almost 3weeks na ni moja ya samaki wanaozaliana kwa wingi na kwa kasi, so ukiwa na kibwawa chako hata cha kutoa debe moja kwa hizo week tatu ni hela ya maana coz debe linaanza na 10k+ fikilia kuku wa kienyeji unaemfuga hadi awe mkubwa wa kuuza 10k atakuwa ametumia miezi mingapi na atakuwa amekula Chakula cha sh ngapi?.

Mm naona hatuwafugi kwa sababu hawako kwa watu wa kutumia akili wakawezakutumia akili zao na ikawa furusa kwa jamii wakatuletea madesa ya namna ya kufuga ndo wataalam wetu waanze kujinadi na kituelekeza namna ya kufuga.
Well said. Kuna mwalimu shuleni kwetu (Rungwe Sekondari) alishawahi kuwa na bwawa la dagaa). Kimsingi wanafugika.

Kinachokosekana hapa ni ujasiriamali ili ijulikane commerciability ya huu mradi. Mimi nina lengo la kuwafuga hawa dagaa (hawa wa Kyela tunaita USIPA). Nitakapopata info nitakuja kuziweka hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom