Jinsi ya kufufua uchumi wa mikoa iliyo nyuma kiuchumi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Kuna baadhi ya mikoa iko nyuma kiuchumi.

Zifuatazo ni njia inazoweza kuzitumia kufufua uchumi wa hiyo mikoa.

1.Kuhamasisha wawekezaji na taasisi za elimu kufungua mashule ya bweni na vyuo kwenye mikoa husika.Shule nyingi za bweni na vyuo vikifunguliwa kilimo hufunguliwa pia kwani maashule hayo ya bweni yawe ya serikali au binafsi yatahitaji vyakula.Hivyo uchumi wa kilimo kuinuka eneo husika.Mkoa wa KIlimajaro ni mfano hai kwa hili.Unaongoza kwa kuwa na mashule mengi ya bweni na soko la wakulima la vyakula linakuwa zuri.Ajira kuongezeka za walimu na wafanyakazi wengine,nyumba za kupanga kupata wateja nk

Vyuo vikifunguliwa pia kunafungua uchumi wa Mkoa watahitaji vyakula,usafiri,mahitaji mbalimbali ya madukani,nyumba za kupanga kuishi wakati wanasoma nk Mji kama Iringa ni mmoja wa miji iliyokuwa imekaribia kufa kiuchumi uwepo wa vyuo vikuu vingi umesaidia kuinyanyua kibiashara na kiuchumi.

2.Kuanzisha viwanda ambavyo malighafi zake zinapatikana mkoa husika kwa kutumia wawekezaji wa nje au wa ndani.

Mfano kwenye Pamba kuanzisha viwanda vya nguo nk

Kama mkoa unalima mpunga kwa wingi kuna sababu gani wasianzishe kiwanda cha regional milling cha huo mkoa ambapo wataufunga mchele wao kama anavyofanya BAKHRESA na kuuuza ndani na nje ya nchi moja kwa moja tokea mikoani kwao?

Ni wajibu wa kila mkoa kuangalia wana nini na kuanza kutafuta wawekezaji wa kuwekeza viwanda kwenye maeneo yao vinavyotumia malighafi zinazopatikana mkoani kwao.Ukiweka kiwanda utainua mkoa

Ni wajibu wa kila mkoa kukaa kufikiria wawe na viwanda gani na waweke mbinu za kupata uwekezaji wa viwanda wanavyotaka ambavyo vitakuwa na impact ya kuinua uchumi wa watu wengi katika mkoa

Mengine ongezeeni wengine.Wenye mawazo ya namna ya kubadilisha mikoa kiuchumi leteni nondo hapa jukwaani.

yehodaya123@gmail.com
 
Niongezee kwenye viwanda,hakuna tija ya kuwa na viwanda vingi Dar wakati hawalimi.Makampuni yalipe kodi mkoa husika na si kila mwekezaji ofisi Dar. Bajeti igawanywe sawai kwa kila mkoa.Maana Nchi sio Dar na Arusha tu.
 
Maeneo ya serikali kama viwanja vya mpira na masoko yarudi serikalini ili zile kodi zitumike kwa maendeleo ya mkoa husika.Ziwepo bei elekezi za mazao maana wakulima wanapunjwa sana na madalali.Hapo kweli tutarahisisha maendeleo.Bila masoko ya maana hatutapiga hatua,zaidi sana tutahamia wote Dar maana huko ndiyo Tanzania.
 
Maeneo ya serikali kama viwanja vya mpira na masoko yarudi serikalini ili zile kodi zitumike kwa maendeleo ya mkoa husika.

Nadhani kwa hali ilivyo sasa ni vizuri mikoa ikashirikiana na sekta binafsi kujenga masoko makubwa ya jumla mfano ya mazao yote yawe yanapelekwa eneo moja kama la mnadani.Mfano kama mkoa unalima maharage waweza weka sehemu ya gulio kwa ajili ya soko la jumla.Wanunuzi wote wa kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje waende hapo wasiende kumfuata mkulima mmoja mmoja.Maana huko ndiko wakulima huumizwa sana na wanunuzi.Soko hilo la jumla laweza kujiwekea bei yake ya mazao tofauti tofauti au waweza amua kuuza kwa mtindo wa mnada kama inavyofanyika soko la samaki ferry dar es salaam
 
Uwepo mpango endelevu wa kuimarisha njia za reli zilizopo na kuanzisha njia mpya, kwa kufanya hivi gharama za usafiri zitashuka kwa kiwango kikubwa hatimaye kipato cha watu kitaongezeka. kwa kulitabua hili hata nchi zilizoendelea bado wanapanua reli zao ndo maana zina Railway contractors. Kwa kutegemea usafiri wa malori pekee hauwezi kututoa, unaharibu sana barabara ambazo zimejengwa kwa gharama kubwa
 
UNAREMBAREMBA NINI BHANA ? Njia pekee na ya uhakika ya kuondoa umasikini kwenye mikoa hiyo ni KUIKATAA NA KUACHANA KABISA NA CCM , utafiti unaonyesha kwamba mikoa yote iliyoikumbatia ccm imekumbwa na umasikini wa kutisha na kufedhehesha sana , watu wamefikia kula viwavi jeshi , Shame !
 
Hamuwezi kukimbizana name mikoa ya kaskazini asilani. Huku hatuna uvivu.. Hakuna dawa zaidi
 
UNAREMBAREMBA NINI BHANA ? Njia pekee na ya uhakika ya kuondoa umasikini kwenye mikoa hiyo ni KUIKATAA NA KUACHANA KABISA NA CCM , utafiti unaonyesha kwamba mikoa yote iliyoikumbatia ccm imekumbwa na umasikini wa kutisha na kufedhehesha sana , watu wamefikia kula viwavi jeshi , Shame !
Mkuu ni kama ulikuwa kichwani mwangu. Kwa nini mikoa ambayo ni base ya ccm ni masikini?
Hill ndio swali la kujiuliza. Ni swali jepesi kama kumuuliza mtoto wa darasa la tano kwanini familia ambayo haizingatii usafi inapata kipindupindu?
 
YEHODAYA, hili ni wazo zuri

mchango wangu

A - Vijana wahamasishwe kujiajiri na kushiriki Kilimo...vijana wawezeshwe..

wizara ya ardhi itenge maeneo yanayofaa kwa kilimo (land bank), vijana wanaozunguka na vyeti na wengine wasio na elimu wapewe kwa mkataba maalumu...Kijana aombe ukubwa wa shamba analoweza kulima, minimum eka 5, mazimum eka 20.

vijana watalima na kuuza mazao na wakivuna, watalipa kodi serikalini.....faida zake

1- Kwanza serikali itakuwa imetoa ajira kwa watanzania

2 - Nguvu kazi ya vijana itakuwa imetumika

3 - mazao kama mahindi, maharage, yatauzwa sudani, Kenya, Malawi..nchi itapata pesa kupitia kodi

4 - Kahawa, Korosho ----- Foreign money

5- Raw material za viwanda..

B- Maeneo yenye vivutio za utalii yatangazwe...

Songea, Mbaba bay.. Kondoa Irangi

Faida zake:

1 - Ajira kwa vijana

2- pesa za kigeni

3 - soko la mazao ya kilimo

4 - Elimu kuongezeka kupitia vyuo vya utalii
 
Kwa sababu hoja imegusia sana kilimo niseme tu kwamba agriculture is a science na kama science nyingine inahitaji ujuzi na utaalamu wa hali ya juu ambao Tanzania hatunao.
Kama vile ambavyo huwezi ukachukua watu barabarani tu ukawapeleka theatre na kuwaambia wamfanyie mtu operation ndivyo huwezi kuchukua tu vijana ambao hawana ajira ukawapa au ukawakopesha ardhi walime mazao halafu wakayauze. Hizo ndiyo fikra alizopandikiza Mchonga enzi za vijiji vya ujamaa na taifa halikufika popote.
Kuhusu kilimo tujifunze kwa wenzetu Afrika Kusini au Zimbabwe ilivyokuwa kabla yule kichaa hajaivuruga.
Hii ni profession na siyo jambo la kufanya kwa sababu tu eti ardhi ipo kwa wingi. Kilimo kinahitaji ujuzi mkubwa wa vifaa na mashine zake, utaalamu na ujuzi wa mbegu, mifumo ya umwagiliaji, distribution networks za kufikisha mazao kote yanakohitajika, cold storage facilities, na mengineyo mengi. Tumejiandaa katika haya yote?
 
Naaona mikoa ingepewa uwezo na madaraka zaidi ya kupanga maendeleo yao, wawe wanatumia kiasi cha kodi inayokusanyawa hapo hapo mkoani.wakuu wa mikoa wapewa malengo ya maendeleo na wawe na jukumu la kuyafikia. Uongozi wa mkoa uwe na wajibu zaidi kwenye manedeleo na sio siasa.
Serikali kuu ihakikishe mikoa ilioko nyuma inasaidiwa kwa mipango na rasilimali zaidi
 
Kwa sababu hoja imegusia sana kilimo niseme tu kwamba agriculture is a science na kama science nyingine inahitaji ujuzi na utaalamu wa hali ya juu ambao Tanzania hatunao.
Kama vile ambavyo huwezi ukachukua watu barabarani tu ukawapeleka theatre na kuwaambia wamfanyie mtu operation ndivyo huwezi kuchukua tu vijana ambao hawana ajira ukawapa au ukawakopesha ardhi walime mazao halafu wakayauze. Hizo ndiyo fikra alizopandikiza Mchonga enzi za vijiji vya ujamaa na taifa halikufika popote.
Kuhusu kilimo tujifunze kwa wenzetu Afrika Kusini au Zimbabwe ilivyokuwa kabla yule kichaa hajaivuruga.
Hii ni profession na siyo jambo la kufanya kwa sababu tu eti ardhi ipo kwa wingi. Kilimo kinahitaji ujuzi mkubwa wa vifaa na mashine zake, utaalamu na ujuzi wa mbegu, mifumo ya umwagiliaji, distribution networks za kufikisha mazao kote yanakohitajika, cold storage facilities, na mengineyo mengi. Tumejiandaa katika haya yote?

Hello, Umetumia muda mrefu sana ku criticize

sasa fikiri kidogo uje na solution....Kama Taifa tufanyeje?

ndio vijana wengi hawana hiyo elimu uliyosema, sasa tufanyeje?

Provide practical solution

hapa watu wanachangia mawazo,,,,, nini kifanyike
 
Kama umesoma vizuri utaona nimetaja mifano miwili ya Afrika Kusini na Zimbabwe. Maana yake ni kwamba tujifunze kwao hasa kwa kuleta wataalamu wao wa kilimo pamoja na wakulima wao. Wataalamu wafundishe na hapo hapo wakulima wao wapewe ardhi kwenye mikoa yote inayofaa kwa kilimo ili waanzishe mashamba ya mifano.
Sijakosoa katika mchango wangu.
 
Back
Top Bottom