Mafanikio ni nini?
Ni mali? Ni furaha? Ni afya? Ni umaarufu?
Wengine wanataka umaarufu, wakiupata wanaona ni mzigo!
Kwanza kabisa, kufanikiwa kwa mtu mmoja si lazima kuwe kufanikiwa kwa mtu mwingine.
Kuna wakina Prince Harry wamezaliwa familia za kifalme, wana maisha ambayo wengi wanaona ni ya mafanikio makubwa.
Lakini wenyewe wanayakimbia.Prince Harry na mkewe anajitoa kwenye shughuli za familia ya kifalme.
Malkia wa Japan hivi karibuni ameeleza jinsi anavyokuwa na msongo wa mawazo sana.
Mfalme wa tahiland kamshusha hadhi mke wake.Ana matatizo katika masuala ya ndoa.
Ted Turner, bilionea aliyeanzisha CNN na mtu mwenye ardhi kubwa kuliko wote Marekani nafikiri mpaka sasa, alisema kwamba, mafanikio yake yote aliyoyapata maishani anasikitika kwamba maisha yake ya ndoa hayakuwa na mafanikio.
Hawa ni watu ambao kwa viwango vya watu wengi ni watu waliofanikiwa sana, lakini na wao wana changamoto zao.
Sasa tungeanza kwa kujiuliza labda.
Mafanikio ni nini?