Jinsi ya kuepuka maneno yenye kuumiza

Jinsi ya kuepuka maneno yenye kuumiza

Daudi1

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
15,629
Reaction score
25,761
Habari ya mapumziko wanakiji wenzangu, basi kama ilivyo kawaida ya kijiji chetu ni kushirikishana katika mambo yanayotujenga na kuimarisha mahusiano yetu na si kuboa ndo maana kijiji kina amani,nisiuze sna chai twende moja kwa moja kwenye maada

Kila mara mnapobishana, wewe na mwenzi wako mnatupiana maneno yenye kuchambua. Maneno yenye kuumiza yamekuwa ya kawaida katika ndoa yenu, hivi kwamba sasa mmezoea kuwasiliana kwa njia hiyo.
Ikiwa ndoa yako iko hivyo, unaweza kuzuia hali hiyo isiendelee. Lakini, kwanza, unahitaji kuchunguza ni nini kinachosababisha tatizo hilo na kwa nini kufanya mabadiliko kutakuwa na manufaa kwenu,zifuatazo zinaweza kuwa sababu zinazopelekea kutokuwa na lugha nzuri pale mnapo kwazana

Malezi.

Waume na wake wengi walilelewa katika familia ambamo watu walizoea kutumia maneno yenye kuumiza. Huenda mwenzi mmoja au wote wawili wakawa wanatumia maneno ambayo waliwasikia wazazi wao wakitumia.

Uvutano mbaya wa burudani.

Waigizaji wa filamu na televisheni hugeuza maneno ya kifedhuli kuwa jambo la kuchekesha, na hivyo kuwafanya watazamaji waone kuwa si vibaya kutumia maneno hayo.

Utamaduni.

Jamii fulani hufundisha kwamba “wanaume halisi” huwakandamiza wengine na kwamba wanawake wanahitaji kuwa wakali sana ili wasionwe kuwa dhaifu. Mabishano yanapotokea, huenda wenzi wa ndoa walio na mitazamo kama hiyo wakawaona wenzi wao kuwa maadui badala ya marafiki na huenda wakatumia maneno yenye kuumiza badala ya maneno yenye kuponya

Mambo unayoweza kufanya

Jiweke katika nafasi ya mwenzi wako
Jiweke katika hali ya mwenzi wako, na ujaribu kuelewa jinsi maneno yako yanavyofanya ahisi. Ikiwezekana, fikiria kipindi ulipongea maneno na mwenzi wako akihisi maumivu kwa maneno uliyosema,hiyo itakusaidia kupunguza ukali wa maneno ambayo yanaumiza zaidi hata ya kupiga

Jifunze kutoka kwa wenzi wa ndoa wanaoheshimiana.

Ikiwa uliiga mifano mibaya ya watu waliotumia maneno yenye kuumiza, tafuta mifano mizuri ya kuiga. Wasikilize wenzi wa ndoa ambao wanastahili kuigwa kwa sababu ya usemi wao.

Amsha hisia mlizokuwa nazo.

Mara nyingi maneno yenye kuumiza ni tatizo linaloanzia moyoni si kinywani. Kwa hiyo, jitahidi kuwa na hisia na mawazo yanayofaa kumhusu mwenzi wako. Zungumzieni mambo mliyofurahia zamani mkiwa pamoja. Angalieni picha zenu za zamani. Ni nini kilichowafanya mcheke? Ni sifa gani zilizomfanya kila mmoja wenu avutiwe na mwenzake.

Tumia neno “mimi.”

Badala ya kumshambulia mwenzi wako kwa maneno, mweleze jinsi mambo mbalimbali yanavyokuathiri. Kwa mfano, ni rahisi kwa mwenzi wako kukujibu kwa maneno mazuri ukimwambia, “Mimi huhisi kuwa nimepuuzwa unapofanya mambo bila kuomba maoni yangu” badala ya kusema, “Hiyo ni kawaida yako kila wakati unafanya mambo bila kuomba maoni yangu!”

Jua wakati wa kunyamaza.

Ikiwa hasira inaanza kupanda na mnashindwa kudhibiti maneno yenu, lingekuwa jambo bora kuahirisha mazungumzo. Kwa kweli, hakuna ubaya wowote kuondoka mabishano yanapokuwa makali na kusubiri hadi mtakapoweza kuzungumza kwa utulivu zaidi
****************************
Karibuni kwa michango zaidi
​
 
Malezi ya watoto yana athari kubwa sana...hasa kwenye mahusiano yao ya baadae...mm nmeshuhudia jinsi watu wanavyopeleka matatizo au tabia walizocopy kutoka kwa wazazi wao na jinsi zinavyo waathiri...sehemu nyingine ya kujirekebisha ni kuangalia maisha ya wazazi au walezi wetu..na kujitahidi kuacha tabia ambazo ni negative...
 
Well said mkuu
 
Mi najua the only way ya kuepusha maneno ni kunyamza mmoja anapoongea
Aongee hadi maneno yaishe mdomoni, nae muda wake ukifika hee....hadi anaomba poo.

safi sana ostaz...! ...
 
Mi najua the only way ya kuepusha maneno ni kunyamza mmoja anapoongea
Aongee hadi maneno yaishe mdomoni, nae muda wake ukifika hee....hadi anaomba poo.

mpenzi kuna wengine ukimnyamazia anahisi unadharau ukisema anahisi unamjibu kiburi basi tabu tupu
 
Hahhhahhha hahhha Evelyn banaa
 
Last edited by a moderator:
Mi najua the only way ya kuepusha maneno ni kunyamza mmoja anapoongea
Aongee hadi maneno yaishe mdomoni, nae muda wake ukifika hee....hadi anaomba poo.

tukinyamaza wanasema tumenuna. ila hiyo ni njia nzuri sana. unaongea wee mpaka ulimi unataka kunyofoka.
 
tukinyamaza wanasema tumenuna. ila hiyo ni njia nzuri sana. unaongea wee mpaka ulimi unataka kunyofoka.

Kuuchuna ni kipindi anaongea baada ya hapo baby zinaendelea
siku ikifika zamu yake kupewa vidonge atatamani akimbie kwa balozi wa mtaa
 
mpenzi kuna wengine ukimnyamazia anahisi unadharau ukisema anahisi unamjibu kiburi basi tabu tupu
Bora aseme nna kiburi tu, nae akiingia kwenye 18 ndo atajua ni kiburi au busara.....
 
Back
Top Bottom