Jinsi ya kuendesha Ngalawa

Jinsi ya kuendesha Ngalawa

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
2,938
Reaction score
517
Jamani naomba msaada nina ndugu yangu amenunua ngalawa ya kuvulia samaki ila tatizo ni kwamba hajui jinsi ya kuendesha hicho kifaa. sasa kuna mwenye ujuzi na hiki kifaa anijuze hili nimueleze. anataka kujua jinsi ya kuipeleka mbele, kuongeza spidi na kupunguza spidi na kuipaki ufukweni.
 
Khaa! Kuogelea anajua? Maana kile kidude kupinduka ni dakika sifuri tu (baharini) na baada ya kupinduka kinahitaji ujuzi kukiokoa na kukipanda tena ili urudi. sasa huyo mdau wako sijui kama ataweza kukigeuza coz kikipunduka kinakua upside down, then kunashuhuli ya kukimwaga maji humo humo baharini then ukipande uendelee na shughuli or urudi nacho kwenu.

Anyway hilo ni angalizo tu (la muhimu)

Namna ya kukiendesha:
Ajifunze kukontroo tanga, ikiwa kinatumia tanga, tanga ni kama sukani. linahitaji ujuzi wa hali ya juu kilishusha, kilipandisha na kuliendesha. Ajue kusoma upepo.

Ikiwa ni la mashine ajifunze hata ujuzi wa mashine coz mashine likimgomea ajue kulibust, na lile mashine kugoma ni takika sifuri tu.

Ikiwa ni la kafi ajue kutumia kafi. ile ni skani yake.

General concepts.

Dereva anakaa nyuma kabisa ya ngalawa.

Ngalawa inaendeshwa kinyume nyume: akitaka kupinda kulia asukume kafi/mashine upande wa kushoto, na akitaka kupinda kushoto asukumie kulia. akitaka kunyoosha apige kafi kulia na kushoto. ikiwa ni ya mashine ni kuinyoosha tu.

Ni lazima ajifunze unahodha, hasa kwa vitendo, ili ajue kusoma upepo, mwelekeo wa maji, wimbi na hali ya hewa, asome na namna ya kukabiliana na hivyo.

NB: Usimshauri kuingia kwenye maji na chombo kabla ya mafunzo. ni hatari sana.
 
mkuu wewe ni mvumvi??...anyways maelezo ni mazuri kabisa.
 
kuna mahari huko rukwa nilisafiri kwa ngalawa masaa nane sijui kama tena nitakuja kupanda hichi chombo
 
Jamani naomba msaada nina ndugu yangu amenunua ngalawa ya kuvulia samaki ila tatizo ni kwamba hajui jinsi ya kuendesha hicho kifaa. sasa kuna mwenye ujuzi na hiki kifaa anijuze hili nimueleze. anataka kujua jinsi ya kuipeleka mbele, kuongeza spidi na kupunguza spidi na kuipaki ufukweni.

kiufupi ngalawa sio computer kama atafahamishwa kwa maelezo, hapa ata umfahamishe vipi akenda pwani hatoiweza, mlete pemba aje apate field huku
 
kuna mahari huko rukwa nilisafiri kwa ngalawa masaa nane sijui kama tena nitakuja kupanda hichi chombo

unaogopa sana, wenyewe wanaiamini ngalawa kuliko hata meli, na wana sababu zao
1 ngalawa haizami, ikizama waibirua na kufata maji
2 ngalawa una uwezo wa kufunga breki na ukasimama hapo hapo
3 kama utakuwepo upepo, basi ngalawa ina spidi kuliko boti
 
pamoja na hayo yataka moyo sana kusafiri na hiki chombo
 
Dereva wake hukaa nyuma daah nimeipenda Sana,ngoja nijifunze nivushe wadada Dar -Zenjy...
 
mkuu kwani kikoje

tulikua watu zaidi ya hamsini yaani ukiwa ndani ya chombo maji unaweza ukayashika hivi halafu goma limeinuka kwa mbele utashangaa wimbi hilo linakuja mwongozaji anavyolikwepa sasa kama linazama hivi tukafika mahari watu wakapungua tukaambiwa turudi nyuma ili injini iguse maji sasa mbele kuko juu huku nyuma kupo chini katika masaa nane sikusinzia hata dakika moja ni hofu tu wenyewe wanapiga stori hawana hata wasiwasi nikajisemea bora ningezunguka kwa gari
 
Hahahaaa, bora wewe ningekua mimi ningekufa kwa presha.Naogopa sana usafiri wa majini.
 
linakuja wimbi kubwa chombo kidogo anavyolikwepa halafu eti wana njia zao kuna muda lilizima ndio nilipojua kwenye shida ndugu Mungu tu mweh safari ya mateso kuliko matumaini unafika mahari unapoenda hupajui ila ulipotoka ni mbali mwehh safari ya historia hii
 
tulikua watu zaidi ya hamsini yaani ukiwa ndani ya chombo maji unaweza ukayashika hivi halafu goma limeinuka kwa mbele utashangaa wimbi hilo linakuja mwongozaji anavyolikwepa sasa kama linazama hivi tukafika mahari watu wakapungua tukaambiwa turudi nyuma ili injini iguse maji sasa mbele kuko juu huku nyuma kupo chini katika masaa nane sikusinzia hata dakika moja ni hofu tu wenyewe wanapiga stori hawana hata wasiwasi nikajisemea bora ningezunguka kwa gari

Kuogelea unajua?...jamani tujifunze tujue kuogelea ni muhimu...
 
tulikua watu zaidi ya hamsini yaani ukiwa ndani ya chombo maji unaweza ukayashika hivi halafu goma limeinuka kwa mbele utashangaa wimbi hilo linakuja mwongozaji anavyolikwepa sasa kama linazama hivi tukafika mahari watu wakapungua tukaambiwa turudi nyuma ili injini iguse maji sasa mbele kuko juu huku nyuma kupo chini katika masaa nane sikusinzia hata dakika moja ni hofu tu wenyewe wanapiga stori hawana hata wasiwasi nikajisemea bora ningezunguka kwa gari

mkuu ni hatari
 
Back
Top Bottom