The Peak Magazine
Member
- Jun 20, 2019
- 5
- 1
Kuna hisia mbalimbali zinazoathiri maisha ya binadamu. Hisia hizi zipo kiasili na zinaathiri mfumo mzima wa maisha.Mtaaalamu Gill Hasson anaelezea umuhimu wa kuzigawa hisia hizi katika makundi mawili, kundi hasi na kundi chanya.
Kwa kutumia njia hii tuelezee hasira ambayo iko katika kundi I la hisia hasi.
Tuanze kwa kuielezea hasira, ni hisia anayoonyesha mtu akikwazika na suala fulani. Hasira huwapata watu wote na ni jambo la Kawaida katika maisha. Suala la kipaumbele ni kujua jinsi ya kuidhibiti hasira Kwani isipodhibitiwa inaweza kukusababishia madhara.
KWANINI UDHIBITI HASIRA?
√Itakupa nafasi ya kujikita zaidi kwenye mambo yako.
√Itakuwezesha kuwa na afya ya kimwili na kiakili.
√Itakujengea amani ya moyo yaani "peace of mind "
Hivyo zifuatazo ni njia Za kukusaidia kuondoa hasira.........
1.CHANZO CHAKE.
Ukiwa na hasira, yakupasa kufikiri kuhusu chanzo cha hasira hiyo. Je ni mtu, au tatizo au hali inayosababisha uwe na hasira?.Usiwe mtu wa kukwazika bila hata kujua chanzo chake.
Baada ya kukijua chanzo hicho jiulize Kama unaweza kukibadili, au Huna mamlaka nacho kabisa (out of control). Itakuwa jambo la ajabu kuwa na hasira juu ya jambo usiloweza kulibadili.
2.SAMEHE.
Hapa haimaanishi kusamehe Wengine, tu jisamehe hata pale unaposhindwa kutimiza malengo uliyojiwekea. Kumbuka unawajibika moja kwa moja na matokeo yaliyopatikana bila kujali malengo au madhumuni uliyojiwekea.
Unaposamehe utapata amani ya moyo, kuliko kutumia Muda wako mwingi kufikiria vitu vinavyokupa hasira.
3.HASIRA HAINA FAIDA!
Huwezi kupinga ukweli kwamba hasira humtokea kila mtu, lakini tukubaliane kuwa haina faida yoyote hivyo ni muhimu kujua jinsi ya kuidhibiti. Buddha aliwahi kusema "you will not be punished for your anger, You will be punished by your anger ".Yaani hautaadhibiwa ukiwa na hasira bali utaadhibiwa na hasira yako".
Kuwa na hasira halafu kutegemea aumie mwingine ni Sawa na kunywa sumu, ukitegemea mwingine afe. Unakuta umempigia mtu Simu hajapokea unakasirika wakati si wewe uliyekataa ukipokea ni yeye aliyekataa kuipokea na hilo liko nje ya uwezo wako.
4.MAZOEZI
Ukiwa na hasira fanya mazoezi,itasaidia kuweka akili yako katika hali ya utimamu. Mazoezi yanayofaa wakati huu ni kukimbia au kutembea huku ukisikiliza muziki. Pia unaweza kufanya mazoezi ya kubana pumzi yaani inhale and exhale.
Mazoezi yatasaidia kuujenga mwili wako vyema, na hivyo kukusaidia kuondoa hasira.
Mwisho tukumbuke kuwa kama walivyosema wahenga, hasira hasara hivyo tujitahidi kuidhibiti.
Je huwa unafanyaje ukiwa na hasira?