Jinsi ya kubadilisha fonts kwenye windows 8 & 10 (bila ya kutumia 3rd party program)

xpl0it

Senior Member
Feb 21, 2014
124
88
Kwenye windows bonyeza Windows key + R , kitatokea kiboksi - we andika 'regedit' (bila kuweka ' ').

Itafunguka Registry Editor, sasa ingia na kuanza kutafuta hapa:

HKEY_CURRENT_USER\Con
trol Panel\Desktop\WindowMetrics


Fonts zinazotumika zinahifadhiwa kwenye values za binary hizi:

1) CaptionFont: captions za windows

2) IconFont: karibia maandishi yote yaliyokatika Windows utilities(ukijumuisha na icons za desktop)

3) MenuFont: pindo za menu na entries za submenu

4) MessageFont: boksi za ujumbe (message boxes)

5) SmCaptionFont: "maandishi kwa herufi ndogo"

6) StatusFont: pindo za status bar

Kila moja ya entry hizo zinaanzia na value yenye bytes 4 ikionesha saizi ya font. Ni namba katika little-endian na kufanyiwa binary-NOT baada ya kujumlisha 2, kwa sababu kadhaa. Vinginevyo uwe huitaji saizi za fonts zaidi ya point 255, unaweza tu ukaangalia kwenye byte ya kwanza. Kwasababu kinyume cha binary ya F4 ni 0B (11 katika desimali), saizi ya kawaida ya IconFont ni point 9. Kwa kupunguza byte hiyo ya kwanza itaongeza saizi ya font na kinyume chake.

Jina la font linaanzia kwenye byte 1C (byte ya 5 kwenye row ya 4). Kwa sababu ni UTF16-LE, lazima kutakuwa na byte 0 baada ya kila herufi. Kuingiza herufi ya kawaida, select text katikati ya window na chapa tu kama kawaida kwenye keyboard yako. Kwenda byte ya 0, iselect katikati (kwenye kategori ya heksadesimali) na kisha bonyeza kitufe cha 0.
00 00 inaonesha mwisho wa jina la font.

Hii ni default value ya IconFont:

file.php


Baada ya kubadilisha font kwenda Comic Sans MS

file.php


Zima na kuwasha kompyuta tena kuona mabadiliko.

file.php


Je, unachakuongezea? Au hujaelewa popote, post hapo chini na wengine wapate kunufaika na majibu. Na kama umeipenda post hii SHARE na wengine.
 
Back
Top Bottom