Jinsi ya kuanza biashara kisheria

tizo1

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
856
145
Jamani wanajamii nataka kuanza biashara ya stationary na kuban cd ni hatua zipi napitia ili niweze kvambulika kisheria.
 
inategemea ni CD zipi anazotaka ku burn!labda ni kwa ajili ya seminar materials!ila sio nyimbo za wasanii.
 
Kwanza nenda BRELA kusajiri jina la biashara ofisi zao zipo 3rd na 4th floors pale lumumba jengo la ushirika lililoungua ambapo chini kuna CRDB branch, then baada ya hapo nenda TRA kufanya maombi ya TIN then ukifanikisha nenda ofisi ya manispaa ya wilaya uliyopo ukaombe leseni ya biashara hapo utakuwa umemaliza, legally... Kumbuka ukienda kufanya maombi kote huko useme unataka kufungua stationery tu usiseme kuburn CD, hizo ni extra services katika biashara yako coz hiziruhusiwi kisheria. ukianza biashara tafuta wazoefu na wajuzi wa biashara hizo waliowahi kufanya na ''kufanikiwa'' pamoja na wadau wa uchumi na biashara kwa ushauri zaidi jinsi ya kuendesha na kusimamia biashara yako.
 
Back
Top Bottom