Jinsi wanafunzi wa 43 walivyopotea.............

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
2,101
Reaction score
5,393
Mwaka 2014 mwezi wa tisa, wanafunzi wakiwa wamekodi mabasi wakielekea katika maandamano ya kupinga kitendo cha aliyekuwa mke wa Mayor wa mji wa Iguala huko Mexico kutaka ndiye awe mrithi wa kiti cha mumewe. Wanafunzi hao kutoka katika chuo cha ualimu kijulikanacho kama Ayotzinapa Rural Teachers College walizuiwa na gari za polisi kisha kuanza kushambuliwa kwa risasi.

Chuo hiki kimekuwa mwiba sana kwa wanasiasa wa Mexico kwakuwa kina historia ya kuzalisha wanamapinduzi wengi wenye mlengo wa Communist ambao wameshiriki sana katika kuleta mabadiriko.

Wakati wanafunzi hao wakiwa njia kuelekea mji wa Iguala, walizuiwa na gari za polisi na kuanza kuwarushia risasi, wanafunzi walianza kupiga mayowe wakiwambia askari kuwa wao ni wanafunzi na hawana siraha ya aina yoyote lakini polisi waliendelea kuwashambulia. Katika tukio hilo mwanafunzi mmoja alifanikiwa kurekodi video ambayo ndiyo ilikuwa kusaidia kuthibitisha ushiriki wa polisi.

Kelele zilisikika toka kwa wanafunzi wakidai kwamba wameua wenzao lakini polisi hawakukoma waliendela kurusha risasi. Baadhi ya wanafunzi walifanikiwa kutoroka lakini 43 walishindwa kwakuwa walikuwa wamezungukwa kila mahali. Polisi waliwakamata na kuwapakia kwenye magari yao na kuondoka nao na hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kwa wanafunzi hao kuonekana tena.

students.jpeg

Wazazi na wanafunzi waliokoka walijaribu fuatilia hilo suala lakini polisi walikana kuwa hawakuhusika katika kushmbulia na kuteka wanafunzi hao. Raia walishirikiana na wazazi na wanafamilia kufanya maandamano kushinikiza serikali kuchukua hatua. Lakini juhudi hazikuzaa matuna.

Vyombo vya kimataifa navyo vilianza anazia tukio hili maanamano yaliendela na kupelekea Gavana wa jimbo la Guerrero ajiuzulu. Siku kadhaa mbeleni mayor naye aliandika barua ya kuomba likizo na kesho yake yeye na mke wake wakapote pasipo kujulikana walipo.

Wazazi wakaamua kwenda kumuona raisi ambapo walimlazimisha asaini document kuonyesha kwamba kitaundwa kikosi cha kuwatafuta wanafunzi hao wakiwa hai toafuti na awali ambapo walikuwa wanatafuta miili yao kama vile walikuwa wakijua kuwa tayari wamekwishauawa.

Wananchi wakajiunga pia kutengeneza vikosi ambavyo vilikuwa vikizunguka maeneo ambayo polisi walikuwa hawaendi kama misituni mabondeni kujaribu kutafuta wanafunzi hawa. Na juhudi zao zilizaa matuna baada ya kukuta kaburi moja kubwa llikiwa lina miili 13 ambapo baada ya kuchukuliwa na kupimwa DNA iligundilika siyo ya wanafunzi hao.

Wananchi waliendela na juhudi zao na wakiwa katika eneo moja ambalo linajulikana kama ni eneo linalotawala na genge moja wapo la kuuza madawa, mmoja wa wao alipokea simu kuwa wamepewa dakika 10 wawe wameondoka eneo hilo la sivyo watashambuliwa na kuawa kama kuku.

Iliwabidi waondoke na baada ya wiki mbili kiongozi wa hao wananchi aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa anatembea tu mtaani.

kutokana na mambo kuwa mazito, Mwanamashtak mkuu wa serikali akishirikiana na kikosi maalumu amabapo walifanikiwa kuwakamata watu kadhaa ambao walidai kwamba mke wa mayor ana mahusiano na kundi lijulikanalo kama Guerreros Unidos drug cartel. Ambalo yeye ni mtu wao katika kufanikisha mambo yao serikalini.

Wakadai kwamba polisi walipowakamata wale wanafunzi waliwapeleka na kuwakabithi kwa Guerreros Unidos drug cartel ambapo walianza kuwatesa wakiwahoji wametumwa na nani. kisha waliwapakia kwenye gari kisha wakiwa njiani 13 kati yao waliuawa kwa kuwafunga mifuko ya plastic wakose hewa, waliobaki waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye dampo, kisha miili yote ilichomwa moto na mabaki kupakiwa kwenye mifuko ya plastic kisha kutupwa mtoni.

Polisi walivamia ule mto wakaanza tafta mabaki na wakapata baadhi ya mabaki. Lakini wananchi hawakuamini kama kweli tukio ndivyo lilivyokuwa na walitaka waletwe wapelelezi wa kigeni wafanye upelelezi.

Mayor na mkewe walikamatwa wakiwa wamejificha kwenye hotel na kufunguliwa mashitaka kwakuwa ilibainika ndiye alitoa order kwa polisi kwamba wazuie wale wanafunzi wasiharibu mkutano wa mkewe kwa hali yoyote.

Mpaka leo yamebaki maswali mengi sana maana hata report toka kwa wamarekani na chuo kikuu kimoja inadai isingewezekana kuchoma miili yote katika eneo lile na kwa muda wanaodai miili ikaungua na kuisha kabisa ikabaki vipande vidovidogo vya mifupa.

Pia toka mwanzo serikali na jeshi la polisi hawakutaka kukubari uhusika wa polisi katika tukio lile isngekuwa ile video aliyo rekodi kijana yule huenda wangebaki kukataa.

mayor.jpg
 
Mkuu,
Inasikitisha,ila watawala mahali kokote duniani uyalinda mamlaka yao kwa namna yeyote ile.Binadamu ni mnyama hatari sana kupata tokea.Asante sana kwa habari hii!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: SDG
upumbavu wa wanasiasa huwa unastaajabisha, huwezi ficha hisia za kukataliwa kwa kuua watu

ni bora kukaa pembeni tu kwa amani kuliko kuishia jera ama kuuawa na wewe
 
Mwaka 2014 mwezi wa tisa, wanafunzi wakiwa wamekodi mabasi wakielekea katika maandamano ya kupinga kitendo cha aliyekuwa mke wa Mayor wa mji wa Iguala huko Mexico kutaka ndiye awe mrithi wa kiti cha mumewe. Wanafunzi hao kutoka katika chuo cha ualimu kijulikanacho kama Ayotzinapa Rural Teachers College walizuiwa na gari za polisi kisha kuanza kushambuliwa kwa risasi.

Chuo hiki kimekuwa mwiba sana kwa wanasiasa wa Mexico kwakuwa kina historia ya kuzalisha wanamapinduzi wengi wenye mlengo wa Communist ambao wameshiriki sana katika kuleta mabadiriko.

Wakati wanafunzi hao wakiwa njia kuelekea mji wa Iguala, walizuiwa na gari za polisi na kuanza kuwarushia risasi, wanafunzi walianza kupiga mayowe wakiwambia askari kuwa wao ni wanafunzi na hawana siraha ya aina yoyote lakini polisi waliendelea kuwashambulia. Katika tukio hilo mwanafunzi mmoja alifanikiwa kurekodi video ambayo ndiyo ilikuwa kusaidia kuthibitisha ushiriki wa polisi.

Kelele zilisikika toka kwa wanafunzi wakidai kwamba wameua wenzao lakini polisi hawakukoma waliendela kurusha risasi. Baadhi ya wanafunzi walifanikiwa kutoroka lakini 43 walishindwa kwakuwa walikuwa wamezungukwa kila mahali. Polisi waliwakamata na kuwapakia kwenye magari yao na kuondoka nao na hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kwa wanafunzi hao kuonekana tena.

View attachment 982721

Wazazi na wanafunzi waliokoka walijaribu fuatilia hilo suala lakini polisi walikana kuwa hawakuhusika katika kushmbulia na kuteka wanafunzi hao. Raia walishirikiana na wazazi na wanafamilia kufanya maandamano kushinikiza serikali kuchukua hatua. Lakini juhudi hazikuzaa matuna.

Vyombo vya kimataifa navyo vilianza anazia tukio hili maanamano yaliendela na kupelekea Gavana wa jimbo la Guerrero ajiuzulu. Siku kadhaa mbeleni mayor naye aliandika barua ya kuomba likizo na kesho yake yeye na mke wake wakapote pasipo kujulikana walipo.

Wazazi wakaamua kwenda kumuona raisi ambapo walimlazimisha asaini document kuonyesha kwamba kitaundwa kikosi cha kuwatafuta wanafunzi hao wakiwa hai toafuti na awali ambapo walikuwa wanatafuta miili yao kama vile walikuwa wakijua kuwa tayari wamekwishauawa.

Wananchi wakajiunga pia kutengeneza vikosi ambavyo vilikuwa vikizunguka maeneo ambayo polisi walikuwa hawaendi kama misituni mabondeni kujaribu kutafuta wanafunzi hawa. Na juhudi zao zilizaa matuna baada ya kukuta kaburi moja kubwa llikiwa lina miili 13 ambapo baada ya kuchukuliwa na kupimwa DNA iligundilika siyo ya wanafunzi hao.

Wananchi waliendela na juhudi zao na wakiwa katika eneo moja ambalo linajulikana kama ni eneo linalotawala na genge moja wapo la kuuza madawa, mmoja wa wao alipokea simu kuwa wamepewa dakika 10 wawe wameondoka eneo hilo la sivyo watashambuliwa na kuawa kama kuku.

Iliwabidi waondoke na baada ya wiki mbili kiongozi wa hao wananchi aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa anatembea tu mtaani.

kutokana na mambo kuwa mazito, Mwanamashtak mkuu wa serikali akishirikiana na kikosi maalumu amabapo walifanikiwa kuwakamata watu kadhaa ambao walidai kwamba mke wa mayor ana mahusiano na kundi lijulikanalo kama Guerreros Unidos drug cartel. Ambalo yeye ni mtu wao katika kufanikisha mambo yao serikalini.

Wakadai kwamba polisi walipowakamata wale wanafunzi waliwapeleka na kuwakabithi kwa Guerreros Unidos drug cartel ambapo walianza kuwatesa wakiwahoji wametumwa na nani. kisha waliwapakia kwenye gari kisha wakiwa njiani 13 kati yao waliuawa kwa kuwafunga mifuko ya plastic wakose hewa, waliobaki waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye dampo, kisha miili yote ilichomwa moto na mabaki kupakiwa kwenye mifuko ya plastic kisha kutupwa mtoni.

Polisi walivamia ule mto wakaanza tafta mabaki na wakapata baadhi ya mabaki. Lakini wananchi hawakuamini kama kweli tukio ndivyo lilivyokuwa na walitaka waletwe wapelelezi wa kigeni wafanye upelelezi.

Mayor na mkewe walikamatwa wakiwa wamejificha kwenye hotel na kufunguliwa mashitaka kwakuwa ilibainika ndiye alitoa order kwa polisi kwamba wazuie wale wanafunzi wasiharibu mkutano wa mkewe kwa hali yoyote.

Mpaka leo yamebaki maswali mengi sana maana hata report toka kwa wamarekani na chuo kikuu kimoja inadai isingewezekana kuchoma miili yote katika eneo lile na kwa muda wanaodai miili ikaungua na kuisha kabisa ikabaki vipande vidovidogo vya mifupa.

Pia toka mwanzo serikali na jeshi la polisi hawakutaka kukubari uhusika wa polisi katika tukio lile isngekuwa ile video aliyo rekodi kijana yule huenda wangebaki kukataa.

View attachment 982762
Mbona sura ya msitahiki meya ni ya ki Durtete! Kuna uhusiano gani wa mauaji ya kikatili na hizi sura?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yote tunamuachia Mungu kwakuwa tunajua na kuamini uwepo wake
 
Back
Top Bottom