Jinsi simu iliyoibiwa inavoweza kupatikana

da irritant boy

JF-Expert Member
Oct 17, 2013
402
436
kuna njia nyingi ambazo zinaweza tumika kuipata simu yako iliyoibiwa, lakini hapa ntaorodhesha chache na nitaelezea moja ya uhakika ambayo ndio hutumiwa na polisi kuweza kupata simu iliyoibiwa

njia zenyewe nj hizi:

1.find my device app
2.icloud tracking
3. Samsung account
4.imei tracking

1. FIND MY DEVICE APP (android)

Hii sio njia ya kuaminika saaana kwa sababu ili iweze kufanikiwa lazima yafuatayo yawe yamekamilika katika simu
i. data iwe on
ii. gps iwe on
iii. device iwe na email active
iv. simu iwe on mda unaotrack

sasa hii njia wezi wakizima tuu simu au hata wakitoa tuu laini simu huipati tena, na pia wezi wakiweza kureset simu na kufyatua kitu kinaitwa FRP na kubadilisha IMEI number bhasi sahau kuipata simu yako hata ukienda polisi watakupiga tuu pesa yako na utaishia kuambiwa watuhumiwa wako wameuawa mkoa fulani au sehem ya mbali na hapo ushatoa hela.

simu ambazo ni rahisi zaid kufyatuliwa FRP na kubadilishwa IMEI namba ni hizi zinazotumia MEDIATEK CHIPSET (MTK) , nikimaanisha TECNO asilimia kubwa, INFINIX, ITEL, NA SAMSUNG hizi entry level smartphone .

simu ambazo hazibadilishilishiki IMEI number kiurahisi kwangu mimi ni IPHONE, OPPO zinazotumia SNAPDRAGON CHIPSET na baadhi ya huawei...

Pia kuna baadhi ya simu ambazo hazizimi mpaka uweke password zinaweza kukupa kamuda kidogo kakutrack simu kabla wez hawajachomoa laini. Mfano: wale vishandu wakisha kupora simu unaweza kuwa na muda wa dakika kadhaa wa kufuatilia simu yako kabla hawajatoa laini.

2. ICLOUD TRAcking
hii njia haina tofauti sana na njia iliyopita ila ni kwamba hii hutumika kwa vifaa vya apple nkiamaanisha simu za IPHONE na PC za MACBOOK

Mwezi uliopita kuna dada aliibiwa begi ndani likiwa na simu ya IPHONE 12 PRO MAX (MACHO MATATU) tuliweza log in icloud yake kwa device ingine na kuanza kufuatilia ile simu location yake, mwsho ilikuwa kwenye motion tuliifuatilia kama dakika 15 hatimae tukakuta ikiwa imetelekezwa na mali zingine ziliondoka.

haiwez faniliwa kama ulikuwa umezima data kwenye simu yako

3.SAMSUNG ACCOUNT
haina tofauti na njia ya kwanza na ya pili sema hutumiwa kwa vifaa vya samsung na lazima vifaa hivyo viwe logged in kwenye samsung account otherwise hutapata device yako


4. IMEI TRACKING ( INAFANIKIWA KWA ASILIMIA KUBWA) kama imei number haitakuwa imebadilishwa
IMEI number ni utambulisho wa simu yako kama ilivyo kwa majina ya binadamu ila hapana maana majina ya binadamu yanafanana unaweza kuta mtaa una wakina shabani 7, lakini sio kwa IMEI, kwa maana hiyo IMEI tunaweza kufananisha na alama za vidole za binadamu hazifanani.

kwa leo sitaelezea saaaana kuhusu imei kwani ni pana sana kila namba ina maana katika IMEI, ila nitaelezea simu inapatikanaje kupitia IMEI number.

kuna APPS nyingi sana huko mitandaoni ambazo zinadanganya kuwa unaweza kutrack simu yako kwa kujaza imei namba yake lakini laa hasha sio kwa Tanzania na ufahamu kabisa kuwa utapigwa vibaya na kuibiwa pesa zako.

KWA UFUPI ILI KILA MTU AELEWE
Unapokuwa umeibiwa simu cha msingi utaulizwa ni imei namba ya simu yako

* kama ni smartphone imei namba yako utaipata kupitia email account yako

* kama si smartphone imei unaipata ukienda kwa vodashop, tigosho, halotel shop, au kituo chochote cha huduma cha mtandao wako kilicho karibu,,,,, kumbuka lazima uwe na Namba ya NIDA na LOSS REPORT ambayo unaweza kuidownload mwenyewe siku hizi na kuiprint

IMEI NAMBA INAVOTUMIWA ILA KUPATA SIMU YAKO
baada ya polisi kupata IMEI namba yako kwa zamani ilikuwa mambo magumu kidogo mpaka waombe TCRA taarifa za IMEI husiku kama laini zilizoingia katika kifaa husika toka siku ya kupotea kwake kwa simu yako. kwa hapo watapata namba namba za laini zilizowekwa katika simu yako toka kuibiwa kwake na wakisha pata namba hapo kale walikuwa wakiwekea mitego watuhumiwa lakini kwa siku hizi database ya polisi iko linked na database ya NIDA, so wakiweka tuu namba wanapata taarifa zoote za mtuhumiwa kuwa alisoma wap baba yake nani , anaishi wapi anafanya shughuli gani na mengineyo.

pia kwa siku hizi ipo system ambayo imeunganisha polisi database, tcra imei database na nida, so wakishaweka imei yako kwenye system taarifa zooote zinakuwa ikiwemo namba zilizowekwa na taarifa za mmilikiwa wa kila namba.

KUTRACK: Mfani simu yako imewekewa laini ya tigo, bhas ile laini husoma katoka mnara wowote uliokaribu na kila mnara utakuwa na taarifa za eneo mfano,,,,, laini inaweza onekana inasoma mnara wa mzumbe, so mtuhumiwa kwa sasa atakuwa mzumbe, wakishafika eneo husika wanaweza mtega mtego mtuhumiwa mpaka anakamatwa.

iwapo mtuhumiwa hayupo hewani bhas polisi huangalia taarifa za mtuhumiwa mfano mtuhumiwa kamaliza shule ya msingi kijitonyama mwaka 2010, wanapata orodha ya watu aliomaliza nao mtuhumiwa kisha polisi humsaka mtuhumiwa kupitia classmates au ndugu wa mtuhumiwa in short kuna njia nyingi sasa za kumpata mtuhumiwa.

ONYO:
1. kutokana na baadhi ya polisi kitengo cha CYBERCRIME kutokuwa waaminifimu unapofuatilia simu yako yakupasa kuwa makini na kutotoa ghalama ambazo unahisi kabisa zitakuwa nje na ghalama za simu yako.

2. polisi wangine wanatabia ya kurefusha mufa wa ufuatiliaji ili kuongeza msululu wa watuhumiwa kulinga na jinsi simu inavozidi kuuzwa kutoka kwa mtuhumiwa mmoja kwenda kwa mwingine.

mfano unaweza kuta watu zaid ya watatu wameuziana simu yako n wote wakatiwa hatiani bhasi huchekechwa na kutishiwa hata kesi za mauaji au kubambikiwa gharama zingine mfano mtu anaambia hii simu aliibiwa dereva wa uba na kuuwawa na gari yake kuibiwa so itabid useme gari liko wapi.

mwisho wa siku simu ikishapatikana huichukui kienyeji labda utoe rushwa simu huchukuliwa kama kidhibiti na utapewa siku kesi imeisha.

3. polisi wanaweza ipata simu ila wakakuzima kama unaonekana kuzubaa kufuatilia au unaonekana wa kuja.

MIMI SIO MWANDISHI MZURI WA LUGHA ILA NADHAN UJUMBE UMEKUFIKIA

pia kama kuna mwenye uelewa zaidi yangu anaweza kuongezea.

ULIZA HAPA KWA FAIDA YA WOTE STOP THE PM THING.

----MWISHO----
 
Polisi wa Tanzania kitengo cha cyber crime ndio tatizo haswa. Unaibiwa simu ukifika unaulizwa ni aina gani? Ukitaja simu yenye thamani kubwa basi unaambiwa hela nyingi kutrack as if iyo huduma inalipiwa. Na wanaokamatwa nayo pia wanapigwa hela. Kimsingi unakuta simu ya laki tano mwenye simu kapigwa laki kutarck, elfu hamsini kufatilia, mkamatwaji na simu katoa laki tatu ili kesi iishe na bado mwenye simu unaambiwa toa hela ya maji. Unaona bora uachane nayo ununue mpya.
 
Polisi wa Tanzania kitengo cha cyber crime ndio tatizo haswa. Unaibiwa simu ukifika unaulizwa ni aina gani? Ukitaja simu yenye thamani kubwa basi unaambiwa hela nyingi kutrack as if iyo huduma inalipiwa. Na wanaokamatwa nayo pia wanapigwa hela. Kimsingi unakuta simu ya laki tano mwenye simu kapigwa laki kutarck, elfu hamsini kufatilia, mkamatwaji na simu katoa laki tatu ili kesi iishe na bado mwenye simu unaambiwa toa hela ya maji. Unaona bora uachane nayo ununue mpya.
kama hauna connection wala cheo chochote lazima uteseke as if siyo haki yako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom