Jobless_Billionaire
JF-Expert Member
- Aug 9, 2022
- 3,903
- 9,915
Mu hali gani wakuu...
Nakumbuka kuna demu niliwahi kuwa naye kwenye mahusiano ya kuibaiba miaka kadhaa nyuma ambae muda huohuo alikuwa ni shemeji pia sababu ya urafiki wake na mwanamke wangu wa kipindi hicho. (Around 2015-2020)
Mahusiano yenyewe yaliibuka kwakuwa mpenzi wangu halisi alipata safari ya kwenda mkoa mwingine. Kwakuwa walikuwa na desturi ya kuja kunitembelea wakiwa wote, kipindi yeye kasafiri, nilibaki mkoani na huyo rafiki yake (shemeji) ambae walikuwa wameshibana sana na mpenzi wangu.
Kwakuwa tulizoeana sana, tulikuwa tukiwasiliana tu kama mtu na shemeji na wala haikuwa na tatizo. Siku ambayo tuliingia nae mahusiano ya kucheat ni asubuhi moja weekend aliponiambia amemiss kuja kunitembelea maana hatujaonana tangu rafiki yake (mpenzi wangu) asafiri. Nikaona hakuna tatizo, maadam nipo, nikamruhusu akaja. Tukapiga story na movies hatimaye ikaingia moment ambayo tulijikuta tumefanya mapenzi na kuanza mahusiano rasmi na huyo shemeji yangu.
Tulienjoy kipindi chote ambacho mpenzi wangu yupo safari, hata kipindi aliporudi tuliendelea kwa siri sana na niliepuka meetings za kukutana wote watatu sababu ingekuwa ngumu kuficha hisia na kupelekea kugundulika. Nilisajili line mpya ili niwe nawasiliana na huyo shemeji yangu tu na tulikula viapo kuhakikisha rafikiye (mpenzi wangu) hatogundua..
TUlikuja kukata mawasiliano na huyo shemeji baada ya yeye kuondoka mkoa husika. Na mimi tulikuja kuachana na mpenzi wangu baada ya kudumu kwa takribani miaka mitano ya mahusiano.
--------****
TUKIO LA KUAMBUKIZWA
Katika ufanyaji wa baadhi ya shughuli zangu kimtandao nilibahatika kukutana na huyu binti tena baada ya kugundua naye ni mmoja ya wafuasi wa ukurasa wangu tukaanza kuwasiliana tena na kujua kila mmoja alipo. Tukakumbushia tu maisha ya nyuma ya cheating tukaishia kucheka na akanieleza kuwa walikuja kuleteana shida na mpenzi wangu hadi kuvunja urafiki kwakuwa alikuja kugundua tulikuwa tukicheat japo tulikuwa tumeshaachana naye..
Kipindi kile yametokea mafuriko ya kufumuka kwa mlima huko Manyara na kuleta maafa, Huyu binti (shemeji) alikuwa anafanya kazi huko.
Baada ya tukio lile, shughuli zake ziliyumba ikabidi afanye utaratibu wa kurudi mkoa X (tulipokuwa kipindi kile tunacheat) ambapo ndio nyumbani kwao ili kupumzisha akili kidogo. Ikumbukwe mimi sikuwa tena mkoa ule.
Siku aliyosafiri, aliomba afikie kwangu kwa siku hiyo kwakuwa nilikuwa mkoa wa njiani na alipokuwa akielekea, alale kisha siku inayofuata aondoke. Sikuona shida nikaruhusu. Hapa ndio ilikuwa chanzo cha matatizo.
Alifika majira ya saa 12 jioni, nikamuelekeza boda akamchukue akaenda. Alifikishwa hadi nilipo, akajifanyia usafi nikamuacha kajipumzisha nikaenda kuchukua chakula. Kwenye saa 3 mambo yakaanza, haikuwa ngumu kuomba game kwakuwa hatukuwahi kugombana. Nilimpelekea moto usiku ule , asubuhi pia tukaamkia mchezoni mambo yakawa fresh tu. Alinielezea kuyumba kwake, nikampa kiasi fulani cha kujikimu huko aendako. Aliondoka siku hiyo saa tano.
Shida ikaja kuanza jioni, mwili nikawa siuelewi elewi. Nikawa najihisi uchovu usio kawaida na kupata joto kali. Ukojoaji ukawa unaambatana na maumivu japo hayakuwa makali. Nikachukulia poa wala sikufikiria kama shida ingekuwa imeletwa na mwanadada. Siku iliyofuata ndio ilikuwa balaa. Kuamka tu nakuta boksa ina unyevunyevu halafu maumivu makali. Nilipoenda kukojoa, kikaona kichwa cha uume kinatoa usaha, taa nyekundu ikawaka kichwani. Maumivu niliyopata wakati wa kujisaidia hayakuwa na mfano.
Kwakuwa sikuwahi kuwa na hiyo shida before, sikuwaza itakuwa gono. Nilijipa moyo hali itaisha badala yake kila ilipoitwa leo ndio nikawa nazidiwa. Nilienda kupima UTI, nikakutwa nayo ikiwa kwenye kiwango cha juu sana. Nilitumia dawa nikapata nafuu ila shida ikabaki kwenye Gono ambalo sikuwa nalifahamu kabla. Nilijua ni UTI tu kuwa kali ndio hufikia huko. Uzalendo ulinishinda nikamfuata nesi mmoja nikamueleza nilivyo. Haikuwa ngumu kwake kubaini nasumbuliwa na nini, akanieleza ndio akili ikakaa sawa.
Alinipatia dawa Azuma boksi kadhaa, nikazitumia kwa maelekezo yake ila hazikufua dafu. Nikamrudia, akanipa zingine pamoja na dawa za kusindikizia lakini bado hazikuwa chochote mbele ya hali yangu. Nilijikuta namchukia yule aliyeniambukiza, nikawa sitaki hata mawasiliano nae tena. Kibaya zaidi nesi akaniambia Gono na UKIMWI ni kama Sunche na Kapeto, yaani asilimia za kuwa na Boko ni kubwa pia, kwahiyo nisubiri miezi mitatu huenda kipimo changu kikasoma reli (mistari miwili)
Nikakosa nuru, nikaona nimerisk maisha yangu kwa starehe ya muda mfupi kiasi kile. Nikawa nafikiria kama nitakuwa nimeathirika itakuwa ni kwa uzembe wangu, kumuamini mtu niliyekuwa nae mbali kwa miaka kadhaa, tena kama mchepuko halafu bado nikauza mechi baada ya kukutana nae.
Nilibadili tabibu nikaenda kwa daktari mwingine akaniandikia sindano. Nikalipia, nikaanza kudungwa ila cha ajabu hazikufanya chochote, nikaona sasa hapa nakaribia kufikwa parapanda. Cha ajabu bidada akawa ananicheki kwenye simu as if hajachafua hali ya hewa huku alipotoka. Nikawa natamani nimwambie akapime UKIMWI antumie majibu ili niwe na uhakika na afya yangu nikae kwa amani ila ikawa ngumu. Nikakaza moyo nikamwambia ila akawa mkali, nikajua tayarii.. Nikamlamba block utadhani ingenusuru chochote. Nikakonda kwa mawazo huku nikiwa bado sijapata hata tiba ya Gono.
Nikawa nashinda mtandaoni naangalia dawa za ugonjwa husika kisha naenda dukani kuchukua ila bado bure kabisa. Akili haikufanya kazi kwa usahihi, tangu nikapime tu zahanati, sikuwaza kwenda hospitali kubwa kwa matibabu, nikawa natembelea pharmacy tu.
Siku moja niliona mtandaoni dawa ambayo sikuwahi kuitumia, nikaenda duka la dawa la daktari mmoja mkubwa majira ya usiku nikanunue. Nikamkuta mfanyakazi wake bahati nzuri nae alikuwepo. Wakati nanunua dawa hiyo, akawa kaniita chumba cha wagonjwa akaniuliza, nataka kutibu nini? Nadhani alitambua kwa haraka. Nikamueleza, nikamwambia na harakati zote za kujitibu hadi kufikia hapo. Akaniambia hata hiyo isingeninusuru. Ikabidi aniandikie dawa complete, na ile niliyoenda kununua ikiwemo. Nikawa an mashaka kama zitafanya kazi, akaniambia kama ukinywa usiku huu ukaamka bado unatoka usaha ijia hela yako. Nikahisi ni lugha tu za kibiashara, nikaondoka na mashaka tele.
Nilitumia usiku ule dawa zile kwa mtiririko elekezi nikalala. Sikuamini baada ya kuamka nikakuta hakuna kabisa usaha. Nikakojoa, maumivu yakawa kwa mbali sana. Nilitumia dawa na asubuhi ile, mchana kisha usiku. Siku iliyofuata nilikuwa mpya kabisa. Sikutaka kukatisha dawa, nilimaliza na nikawa version nyingine kabisa. Nikakaa week, nikaenda kupima mkojo ukawa upo fresh kabisa. Kipengele kikabaki kwenye UKIMWI. ilipita miezi minne nikapima nikawa niko fresh. Furaha ikarudi upya kabisa na kuanza kufurahia maisha tena.
Yule bidada siwasiliani nae tena, aliwahi kunicheki kama mara mbili kwa namba ngeni, na siku anarudi Manyara akaniambia anapita nikamwambia mie sipo na sihitaji mazoea nae..
Let's Play Safe Guys.. ni hayo tu