tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 22,378
- 19,213
- Thread starter
- #121
acha hadithi zako za alfu lela ulela.....kuvunja sheria kwa kuwazuia watumishi wa umma kupandishwa vyeo na kunyimwa maslahi yao hakuna manufaa yoyote kwa wafanyakazi wanyonge wanaolipwa mishahara uchwara. kumbuka kwamba kama ilikuwa mtumishi apande cheo mwezi wa tano mwaka huu na bado hajapanda hawezi kupanda tena hadi dr makufuri atakapotaka na elewa kuwa sasa hivi hakuna kupanda cheo kwa kuserereka....hata ikipita miaka 10 hujapandishwa cheo, utakuja kupanda cheo mara moja tu.....wewe huoni kwamba hii ni dhuluma dhidi ya wanyonge?Hata mghani mashairi ya namna gani, sisi watanzania tunamuunga mkono Mheshimiwa rais Magufuli na serikali yake. Unapofanya mabadiliko makubwa ya kimfumo katika nchi ni lazima ukubali kuumia kidogo. Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi akafikiri kufanya mabadiliko bila kupata maumivu. Nitoe mfano kidogo, wewe una nyumba ya kuishi ambayo imechakaa na inahitaji ukarabati mkubwa. Bila shaka huwezi kuepuka usumbufu wakati unapofanya ukarabati kwa sababu muda mwingine utalazimika kupanga nyumba kwa muda ili kupisha ukarabati huo. Kwa maana hiyo, kinachoendelea kwa sasa katika nchi yetu ni marekebisho makubwa ya kimfumo katika nchi yanayofanywa na MHESHIMIWA RAIS MAGUFULI. Adha ndogo ndogo tunazoziona kwa sasa ni za muda mfupi tu hivyo tusiwahadae wananchi kuwa Mheshimiwa rais Magufuli ni dictator. Tutumie muda mwingi kuwahamasisha wananchi kufanya Kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato chao. Ndani ya kipindi kifupi maisha ya watanzania yatakuwa ni mazuri sana.