Basi baada ya kucheka huku kimoyo moyo nikiombe iishe kabisa na maombi yalijibiwa,kufika iringa simu imeshazima[emoji1787][emoji1787][emoji706]
Nikaona poa, at least atakua na muda na mimi tutaongeaa kidogo.
Badala ya kuongea naona mtu amesinzia
[emoji848]Nikasema kimoyo moyo hii pisi sio charming ata kidogo.
Tumefika dodoma gari lilisimama kwa dakika chache ambapo ulikua ni wasaha wa kuchimba dawa na kupata lunch.
Lakini Cha ajabu naona mtu hainuki afu anapiga mihayo ya kufa mtu kama papa mwenye njaa.
Nikaona haipendezi nimeshuka na kubeba chips kuku mbili Moja yangu Moja kwaajili ya Binti.
Nilipofika na kumkaribisha alishukuru sana mpaka nikahisi huyu Binti hakua na pesa
Ni kweli alikua Hana cash na alikiri kwamba kweli pesa zilikua kwenye simu ila alikua anaona aibu kuniomba simu aweke chip yake ili afanye miamala.
Nikacheka[emoji1787][emoji1787]
Nikamwambia hakuna haja, nitakupa power bank.