Jinsi nilivyopata mtaji wa bodaboda - TRUE STORY | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi nilivyopata mtaji wa bodaboda - TRUE STORY

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by meningitis, Jun 22, 2012.

 1. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  nimebahatika kumuhoji kijana mmoja huko mjini arusha na kwa ufupi haya ndiyo aliyoniambia....

  "kabla ya kumiliki Toyo nilikuwa kibaka nikivizia kinadada na walevi hasa nyakati za jioni na mapema asubuhi.siku moja nilishikwa na kupigwa vibaya na baadaye kulazwa hospitali ya mt.meru kwa muda wa miezi miwili.
  Kitendo hiki kiliniuma na kuniabisha sana mbele ya familia yangu.hivyo baada ya kupona nilimuomba baba yangu auze shamba lake dogo kiasi cha milioni moja na nusu.nilitumia fedha hii kununulia Toyo(bodaboda).
  Bodaboda hii inaniwezesha kulisha familia na kununua mavazi.uendeshaji wa bodaboda unaniweka kwenye hatari ya kutekwa au kupata ajali lakini sina jinsi!
  Nimesikia wameondoa kodi kwa waendesha boda boda lakini wameweka kodi kubwa sana kwa wamiliki wake kama mimi.kwa kweli inaniuma sana''
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Tunapitia mengi sana kabla hatujatoka wakati kuna akina riz1 wanaotoka moja kwa moja! My God!!!
   
 3. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  inashangaza sana!serikali imeshindwa kutoa ajira lakini iko makini kudai kodi pale vijana wanapojiajiri.
   
 4. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Sasa tusubiri vibaka hao walioamua kuwa wajasiriamali washindwe kuendesha biashara hiyo kwa sababu ya kodi kubwa. Watarudi wote mitaani kukaba upya.
  Ndiyo maana ukipata ajali na wenye bodaboda wanakuzama mifukoni na laptops zinakwenda, kumbe walikuwa vibaka na bado ipo ktk mishipa ya damu.
  Nashukuru mkuu kwa kunijuza
   
 5. Mracho Ngongoti

  Mracho Ngongoti Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 90
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Pole sana Ndauwoo!
   
 6. Brown73

  Brown73 JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 866
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 80  Kama unasema kweli na umeweza kujotoa katika balaa hilo la kuwaibia watu basi tunakuombea mungu azidi kukuokoa na akuzidishie anachokupa ili uweze kuwa saidia wazazi wako na ndugu zakoa.
  Nafahamu vizuri tatizi hilo na ni la sugu. wako vijana wamesha pigwa karibia kufa lakini ndia kwanza wezidi.
  Kuna mdogo wetu yeye tatizo ni kuiba ndani kwao, tuseme anajiibia mwenyewe na ni kwa ajili ya ulevi. Anapotaka kulewa basi lazima aibe hata kama kuna kilo ya nyama ndani basi ataiba. Tume mpa msaada wa kila aina lakini hela zinaishia kwenye pombe. Siku tatu anakua mchapa kazi mzuri, akisha pata faida nzuri tu basi, faida na mtaji unaishia kwenye pombe. Nimemleta tractor lakilimia pia limemshinda.
  Sasa sijui hiyo ni laana au ni kitu gani. wakati kuna mtu mwingine anafikira laki mmoja aipate vipi ili aanzishe kiji biashara.
  Kwahiyo kijana nafikiri ulukua na marafiki uliokua ukishirikiana nao, na hao pia inabidi uwaaonyeshe huo mfano wako na wewe usikate tamaa. Maisha ni mtihani. Kuiba utaiba lakini kumbuka siku za mwizi ni...

   
 7. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Mbona mtaji wenyewe wa kupewa then easy tuu!
   
Loading...