Jinsi nilivyopata mke, Mwanzo sikumpenda ila sasa nampenda sana

Mkuu asante kwa ushuhuda, maana naamini tunamshinda sheteni kwa shuhuda za maneno yetu.pia naamini kwa ujumbe huu kuna mtu atatoka alipo kwama.

Sifa na utukufu, uweza na nguvu vyote vina yeye alie kupa mke mwema, usiache kutoa sadaka ya shukurani kwa ajili ya mkeo.

Amen
Shetani hashindwi kwa "maneno" matupu bali Wanadamu humshinda Shetani kwa "kumtii" MUNGU na kumwamini YESU KRISTO. Soma Yakobo 4:7-8
 
Nilikuwa na mchumba wangu ambaye nilimpenda sana. Tulidumu kwenye mahusiano kwa miaka 4. Ujasiri wa kumpenda ulikua mkubwa sababu nilimjua tu baada ya yeye kumaliza kidato cha nne. Mtoto alikua na bikra na jinsi alivyokua mzuri ni kitu ambacho sikutarajia

Wakati huo tulikua Arusha, nilihamia Dar katika harakati za kusaka maisha baada ya kumaliza chuo. Tuliishia kuwasiliana tu ila niligundua ni mwanamke mvumilivu sana na mwenye upendo mwingi

Ugumu wa maisha ilinifanya nibadili mtimdo wa maisha. Niliamua kuzikimbia anasa za dunia na kumrudia Mungu. Nilianza kuwa mtu wa sala, kufunga na kuomba kwa bidii sana.

Kwa bidii hiyo Mungu alianza kunifunulia mambo mengi sana ya maisha na maisha yangu kiuchumi,kiroho n.k yalianza kufunguka taratibu. Nilianza kuomba mambo sio yangu hata ya watu wengine nilio wafahamu.

Sikuacha kumwambia Mungu anipe mke mwema pamoja na kwamba nilikua na mchumba wa muda mrefu nilimsihi Mungu mapenzi yake yatimie, si kama nitakavyo mimi ila yeye.

Siku moja niliota ndoto kwamba niko na rafiki yangu na tunaelekea kwa fundi wa suti ya harusi yangu, nilikuta bado fundi hajamaliza kushona na ndio ilikua siku ya harusi, tukaamua kwamba tuwahi kariakoo kutafuta nyingine sababu muda umeisha, wakati tuko njiani kuelekea kariakoo huyo rafiki angu aliniuliza, Bibi harusi ni nani? Na yuko wapi? Nilimjibu mimi mwenyewe simjui ila yuko saloon, twende tukamuome kwanza. Tulienda saloon na tulikuta binti mmoja ambae tulikua tukisali naye tayari amevaa shela na kupambwa vizuri. Nilipo mwona nilijibu, ooh kumbe ni huyu? Basi sawa hamna shida. Ndoto iliishia hapo.

Hii ndoto ilinifedhehesha sana sababu nilijua maana yake na huyu mwanamke nilie muona kwenye ndoto sikua na mazoe nae wala sikumpenda kimapenzi kabisa.

Nilipingana na ndoto hii kwa kuomba ruhusa kazini, nilienda kwa mchumba wangu. Nilienda na kujitambulisha kwa ndugu zake, nilibeba zawadi nyingi sana. Tulikubaliana wiki hiyohiyo nitume washenga kwa miongozo ya mahari na kuanza mchakato wa ndoa haraka iwezekanavyo.

Nilirudi mjini na baada ya siku mbili mchumba alikua hapatikani kwenye simu tena, nilimtafuta ndugu yake lakini majibu yake yalinimaliza. Alisema hapo alipo ana mimba ya mtu mwingine hivyo hatuwezi kuoana na baadae alisema kuna mwanamke amempigia simu akatishia kumuua kama hataachana na mimi. Ninacho jua mm sikua na mahusiano yoyote na mtu yoyote na ndoto ile ilibaki kuwa siri yangu.

Nilienda mkesha wa maombi ya vijana na wakati tunaomba nilisikia sauti kubwa ikisema geuka mtazame mkeo, niligeuka na kumuona yule ambae nilimwona kwenye ndoto. Nilipingana na hili tena na kuuambia moyo wangu HAPANA, hayo pengine yalikua mawenge na uchovu

Baada ya miezi kama miwili nilipigiwa simu na dada mmoja hivi mfanya biashara mkubwa na mcha Mungu Sana, alinambia Mungu amemuonesha maono kwamba kunakitu nilimwomba, akanipa ila sitaki kusikia. Nilimkatalia yule dada. Alinialika nyumbani kwake na nilikuba kumwambia kilichotokea, alisisitiza kwamba nilicho sikia ilikua sauti ya Mungu na hivyo natakiwa kutii.

Wakati huo mchumba wangu wa Arusha alinikataa katakata bila sababu yoyote ya msingi...

Niliamua kumtii Mungu ila kwa kujilazimisha, nilimtafuta binti, na hakusita hata kidogo. Haikuchukua muda tukaanza maandalizi ya ndoa

Mpaka siku ya ndoa nilihisi niko kwenye ndoto, na swali kubwa kwa Mungu lilikua Mungu kwanini unimpe mtu ambaye simpendi? Nitaishi naye vipi? Hisia za mapenzi kama mume na mke hazipo!! Itakuaje? Je, nitampenda lini? Haya maswali yalikua siri ya moyo wangu na Mungu. Nili-fake tabasamu tu lakini moyoni nilijawa na majonzi na maumivu makali.

Nilimuuliza Mungu kwanini hupendi hisia zangu? Na siku ya ndoa niliomba Mungu honeymoon iishe haraka turudi nyumbani.

Siku mpenda mke wangu kabisa, wakati mwingine nilitafuta wine iniondolee mawazo. Niligundua kwamba mke wangu ni mtu wa sala sana, anasali bila kuchoka na kukata tamaa, aligundua kwamba sina hisia kwake lakini hakuacha kuomba.

Kuna mambo alikua akifanya mke wangu yalinivuta sana na kuanza kumtafakari, bidii ya kazi, heshima, mpole, mwaminifu na asiye na makuu. Haya mambo yalinifanya nianze kumpenda mke wangu ghafla. Ghafla nilianza kuona uzuri ambao ulijificha ndani yake ambao kwa jinsi kibinadamu nisingeweza kuuona

Siwezi kuelezea uzuri wake nikamaliza. Leo I feel kama ndio tunachumbiana, kila siku namuona mpya kwangu. Namshukuru Mungu sana kwa kunipa wa kufanana naye.

Mwanzoni sikutambua kusudi la Mungu lilikua nini! Leo nimeona. Mambo mazuri yamefichwa katikati ya changamoto. Mungu akusaidie ujifunze kitu, Amen

Thank you Jesus, thank you LORD!
Asante sana mtumishi.Ubarikiwe sana kwa somo zuri.
 
Mwanamke mwenye hizi sifa, bidii ya kazi, heshima, mpole, mwaminifu na asiye na makuu, anakubalika na kila Mwanaume, Sio sura,umbo na mwonekano, Ila hizi sifa bidii ya kazi, heshima, mpole, mwaminifu na asiye na makuu ni ngumu sana kuzipata kwa sasa.
Kwa mwanadamu haiwezekani ila kwa Mungu inawezekana.
 
Mwanamke mwenye hizi sifa, bidii ya kazi, heshima, mpole, mwaminifu na asiye na makuu, anakubalika na kila Mwanaume, Sio sura,umbo na mwonekano, Ila hizi sifa bidii ya kazi, heshima, mpole, mwaminifu na asiye na makuu ni ngumu sana kuzipata kwa sasa.
Na ndo maana Mungu kamfunulia huyu jamaa kwa sababu aliamua kukaa vizuri na Mungu aka kutembea katika neema ya Mungu.

Mungu hawezi kumfunulia gumegume siri kubwa kama hii ambayo itajenga vizuri ufalme wake. The woman is a gem, a pearl something expensive. Ilibidi jamaa akae na Mungu vizuri kwa maombi, toba, kufunga na matendo mema plus sadaka ili kuipata zawadi nzuri lakini eti ubaharia hahaha...dj niletee mabaharia hapa mbele.
 
Hapa ndipo waamini wengi wanapoanza kujimiksi...

Mke mwema ni zawadi ya Mungu kwa mwanaume, mwanaume unapaswa kuitunza hiyo zawadi.

Mungu hushukuriwa kwa moyo uliojawa shukrani...

Je, baba yako akikutunuku wewe zawadi, nawe huwa unamrudishia zawadi nyingine kama shukrani?
Kwa kua sio muamini huwezi kuelewa mambo ya imani mkuu.

Kwanza kabisa Mungu hakupi mke, mke unajipatia mwenyewe kwa juhudi zako ila tu Mungu anaweza kusaidia na kukuongoza kupata mke. Na ndio maana bibilia inasema "apatea mke" sio "apewae mke".

Shukrani ni sauti ya imani na ndani ya shukrani kuna baraka na baraka ina nguvu ya kuongezeka, so kwa kutoa sadaka ya shukurani juu ya mke mwema ulie nae itatengeneza akiba na deni kwa Mungu la kumlinda na kumuepusha na baadhi ya ya mambo.
 
Nilikuwa na mchumba wangu ambaye nilimpenda sana. Tulidumu kwenye mahusiano kwa miaka 4. Ujasiri wa kumpenda ulikua mkubwa sababu nilimjua tu baada ya yeye kumaliza kidato cha nne. Mtoto alikua na bikra na jinsi alivyokua mzuri ni kitu ambacho sikutarajia

Wakati huo tulikua Arusha, nilihamia Dar katika harakati za kusaka maisha baada ya kumaliza chuo. Tuliishia kuwasiliana tu ila niligundua ni mwanamke mvumilivu sana na mwenye upendo mwingi

Ugumu wa maisha ilinifanya nibadili mtimdo wa maisha. Niliamua kuzikimbia anasa za dunia na kumrudia Mungu. Nilianza kuwa mtu wa sala, kufunga na kuomba kwa bidii sana.

Kwa bidii hiyo Mungu alianza kunifunulia mambo mengi sana ya maisha na maisha yangu kiuchumi,kiroho n.k yalianza kufunguka taratibu. Nilianza kuomba mambo sio yangu hata ya watu wengine nilio wafahamu.

Sikuacha kumwambia Mungu anipe mke mwema pamoja na kwamba nilikua na mchumba wa muda mrefu nilimsihi Mungu mapenzi yake yatimie, si kama nitakavyo mimi ila yeye.

Siku moja niliota ndoto kwamba niko na rafiki yangu na tunaelekea kwa fundi wa suti ya harusi yangu, nilikuta bado fundi hajamaliza kushona na ndio ilikua siku ya harusi, tukaamua kwamba tuwahi kariakoo kutafuta nyingine sababu muda umeisha, wakati tuko njiani kuelekea kariakoo huyo rafiki angu aliniuliza, Bibi harusi ni nani? Na yuko wapi? Nilimjibu mimi mwenyewe simjui ila yuko saloon, twende tukamuome kwanza. Tulienda saloon na tulikuta binti mmoja ambae tulikua tukisali naye tayari amevaa shela na kupambwa vizuri. Nilipo mwona nilijibu, ooh kumbe ni huyu? Basi sawa hamna shida. Ndoto iliishia hapo.

Hii ndoto ilinifedhehesha sana sababu nilijua maana yake na huyu mwanamke nilie muona kwenye ndoto sikua na mazoe nae wala sikumpenda kimapenzi kabisa.

Nilipingana na ndoto hii kwa kuomba ruhusa kazini, nilienda kwa mchumba wangu. Nilienda na kujitambulisha kwa ndugu zake, nilibeba zawadi nyingi sana. Tulikubaliana wiki hiyohiyo nitume washenga kwa miongozo ya mahari na kuanza mchakato wa ndoa haraka iwezekanavyo.

Nilirudi mjini na baada ya siku mbili mchumba alikua hapatikani kwenye simu tena, nilimtafuta ndugu yake lakini majibu yake yalinimaliza. Alisema hapo alipo ana mimba ya mtu mwingine hivyo hatuwezi kuoana na baadae alisema kuna mwanamke amempigia simu akatishia kumuua kama hataachana na mimi. Ninacho jua mm sikua na mahusiano yoyote na mtu yoyote na ndoto ile ilibaki kuwa siri yangu.

Nilienda mkesha wa maombi ya vijana na wakati tunaomba nilisikia sauti kubwa ikisema geuka mtazame mkeo, niligeuka na kumuona yule ambae nilimwona kwenye ndoto. Nilipingana na hili tena na kuuambia moyo wangu HAPANA, hayo pengine yalikua mawenge na uchovu

Baada ya miezi kama miwili nilipigiwa simu na dada mmoja hivi mfanya biashara mkubwa na mcha Mungu Sana, alinambia Mungu amemuonesha maono kwamba kunakitu nilimwomba, akanipa ila sitaki kusikia. Nilimkatalia yule dada. Alinialika nyumbani kwake na nilikuba kumwambia kilichotokea, alisisitiza kwamba nilicho sikia ilikua sauti ya Mungu na hivyo natakiwa kutii.

Wakati huo mchumba wangu wa Arusha alinikataa katakata bila sababu yoyote ya msingi...

Niliamua kumtii Mungu ila kwa kujilazimisha, nilimtafuta binti, na hakusita hata kidogo. Haikuchukua muda tukaanza maandalizi ya ndoa

Mpaka siku ya ndoa nilihisi niko kwenye ndoto, na swali kubwa kwa Mungu lilikua Mungu kwanini unimpe mtu ambaye simpendi? Nitaishi naye vipi? Hisia za mapenzi kama mume na mke hazipo!! Itakuaje? Je, nitampenda lini? Haya maswali yalikua siri ya moyo wangu na Mungu. Nili-fake tabasamu tu lakini moyoni nilijawa na majonzi na maumivu makali.

Nilimuuliza Mungu kwanini hupendi hisia zangu? Na siku ya ndoa niliomba Mungu honeymoon iishe haraka turudi nyumbani.

Siku mpenda mke wangu kabisa, wakati mwingine nilitafuta wine iniondolee mawazo. Niligundua kwamba mke wangu ni mtu wa sala sana, anasali bila kuchoka na kukata tamaa, aligundua kwamba sina hisia kwake lakini hakuacha kuomba.

Kuna mambo alikua akifanya mke wangu yalinivuta sana na kuanza kumtafakari, bidii ya kazi, heshima, mpole, mwaminifu na asiye na makuu. Haya mambo yalinifanya nianze kumpenda mke wangu ghafla. Ghafla nilianza kuona uzuri ambao ulijificha ndani yake ambao kwa jinsi kibinadamu nisingeweza kuuona

Siwezi kuelezea uzuri wake nikamaliza. Leo I feel kama ndio tunachumbiana, kila siku namuona mpya kwangu. Namshukuru Mungu sana kwa kunipa wa kufanana naye.

Mwanzoni sikutambua kusudi la Mungu lilikua nini! Leo nimeona. Mambo mazuri yamefichwa katikati ya changamoto. Mungu akusaidie ujifunze kitu, Amen

Thank you Jesus, thank you LORD!
Amen,Maombi yanajibu na pili unaweza kumpenda mtu lkn ukashindwa kuishi nae coz ya tabia kinachoitajika ni maarifa ,hekima itokayo kwa Mungu.Nawatakia maisha mema ya furaha mkiwa katika Kristo.
 
Mwanamke mwenye hizi sifa, bidii ya kazi, heshima, mpole, mwaminifu na asiye na makuu, anakubalika na kila Mwanaume, Sio sura,umbo na mwonekano, Ila hizi sifa bidii ya kazi, heshima, mpole, mwaminifu na asiye na makuu ni ngumu sana kuzipata kwa sasa.
Wapo ukiomba kwa uaminifu Mungu atakupa.
 
Back
Top Bottom