Jinsi nilivyofanikiwa kununua pikipiki

Jinsi nilivyofanikiwa kununua pikipiki

Habari za jumapili wakuu
Story yangu ya kumiliki boda boda ilianza kama utani tu siku moja niliamua kuchongesha kibox ambacho nitakua naweka coins ndani yake. Kwa hiyo nikajiwekea malengo kila siku nitakua natumbikiza coins yoyote kila nikiludi kutoka kwenye miangaiko. Kuna kipindi nilikua naweka ata 500 au zaidi siku nyingine siweki maana nakua sina. Ilinichukua miaka 2 atimae week ilopita nimekibomoa na kutoa coins zote nikahesabu na kupata milioni 1, laki nane na elf 90.
Hivyo kwa kua hamu yangu ilikua ni kumiliki boda fasta tu nikawai dukani hivyo kwa sasa namiliki na kuiendesha mwenye.
Mkuu hebu kuwa mkweli, mwaka 1 ni siku 365 na robo au tufanye 366. Chukua 366 x 2 = 732. Zidisha 500 ulokiwa unaweka kwa siku mara siku 732, unapata 366,000/- wewe hiyo 1.9 umepataje? Ili upate hiyo hela laba ulikiwa unasave 2,600 kila siku
Sio akili za kitoto alikua hajasoma vizuri. Kwa haraka haraka alikua yupo sahihi kuhoji.
Ila ukweli ni kua ukiweka nia unawezakufanikisha ata usichotegemea. Kwa kua nilishaweka nia ya kila sarafu kuitumbukiza ilikua ata nikiwa na sarafu za elf 3 lazima nitaziweka. Kumbuka hizo ni coins 6 tu za mia 5
Hongera sana kijana huo ni mwanzo mzuri nakuomba usiridhike na pikipiki tu wapo watu wanamiliki mali magari na hawajitangazi, jitahidi kujiwekea akiba pesa unayoipata ktk bodaboda siku moja utamiliki ndinga kama hii
IMG-20180414-WA0034.jpg
 
Mimi ni tomaso bado juu ya hili ila nimejifunza kitu hakika. Nitaifanyia ubunifu zaidi.
 
kuna njitu bongo zao n mwendo wa code error akijitahd kdg ataambiwa please wait au network loading..... Yan akiwa anawaza jambo akasika saut ya Inz au Mbu akipita tu anasahau kila kitu. Inamaana hapo kwenye "ata 500 au zaid" hapaonekan?
 
Hongera mkuu, Nimejifunza kitu

Mkuu ebu jaribu na wewe hizo sarafu za kila siku zisunde sehemu salama kwa kipindi. Usiwe unazichungulia unaweza kuziiba ingawa ni zako. Kama lengo ni mwaka basi jitahidi iwe mwaka kweli
 
Bila kusahau ukubwa hilo box la kuweza kuhifadhi 1.96 mil za sarafu........mwenyewe ninamtindo wa kuhifadhi sarafu yeyote nikirudi nyumbani, sarafu zinachukua eneo kubwa la kuhifadhi.

Ukubwa wa box inategemea na wewe mwenyewe utakavyo. Kwenye kuweka hizo sarafu zako uwa unatumia muda gani kuzitoa kwa matumizi mengine na huwa unapata kiasi gani??
 
Hongera kwa nidhamu hiyo. Jenga kiboksi kingine, weka noti kila siku(haijalishi ya kiasi gani) kwa kuwa utakuwa unaingiza pesa za boda boda, utakuwa mbali.

Kuanzia mwezi ujao naanza kuweka hela yote niliyokua napeleka kwa Boss kabla. Ambayo ni elf 7 nimejiwekea lengo la miaka miwili. Najua nitafanikisha.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Jibu murua sana. Wabongo wanapenda kubisha sana. Huyo jamaa alifikiri ulikuwa unaweka 500 kila siku. Ktk maisha ni rahisi kupiga hatua moja mbele na pia ni ngumu kupiga hatua mbele km hauna malengo. Hongera sana
Hata km umepanga kila siku unapotoka kwenye mihangaiko ukiwa unasave 1000 inatosha kulipa chumba.

Mkuu ni kweli kwenye hilo la kupanga elf moja kila siku inatosha sana tu
 
kuna njitu bongo zao n mwendo wa code error akijitahd kdg ataambiwa please wait au network loading..... Yan akiwa anawaza jambo akasika saut ya Inz au Mbu akipita tu anasahau kila kitu. Inamaana hapo kwenye "ata 500 au zaid" hapaonekan?

Hahahaha mkuu mada kama hii maswali lazima yawepo ni haki ya kila mtu tafadhari tusiwe madikteta kwenye kutoa majibu
 
Kuanzia mwezi ujao naanza kuweka hela yote niliyokua napeleka kwa Boss kabla. Ambayo ni elf 7 nimejiwekea lengo la miaka miwili. Najua nitafanikisha.
Mpango mzuri, kila la Kheri! Nidhamu ya fedha na kujiwekea akiba ndio kila kitu!
 
Hongera sana kijana huo ni mwanzo mzuri nakuomba usiridhike na pikipiki tu wapo watu wanamiliki mali magari na hawajitangazi, jitahidi kujiwekea akiba pesa unayoipata ktk bodaboda siku moja utamiliki ndinga kama hiiView attachment 768688

Daahhh huko kwenye huo usafiri nazani utasubilia kidogo nazani naitaji kupanda hadhi kidogo kutoka kwenye boda kwenda kwenye Taxi kwanza hivyo miaka miwili ijayo. Huku tukiomba uzima naweza kufanikisha
 
Mimi ni tomaso bado juu ya hili ila nimejifunza kitu hakika. Nitaifanyia ubunifu zaidi.

Hutojutia mkuu wewe jaribu tu ata kama sio kununua boda inaweza kukutoa kwenye kulipa chochote au kununua chochote. Bora kujaribu alafu ushindwe kuliko kutokujaribu kabisa
 
Then hiyo pikipiki ndo itaanza kuchukua hivo visent vyote ulivyokuwa unapata.
 
Then hiyo pikipiki ndo itaanza kuchukua hivo visent vyote ulivyokuwa unapata.

Poa mkuu lakini si nimejaribu na kutimiza lengo langu. Hivyo nitajitahidi kadri niwezavyo ili niweze kufanikiwa
 
Ukubwa wa box inategemea na wewe mwenyewe utakavyo. Kwenye kuweka hizo sarafu zako uwa unatumia muda gani kuzitoa kwa matumizi mengine na huwa unapata kiasi gani??
Mh.......kuhifadhi 1.96 mil?
 
a
Asante mkuu kwa kuuliza ni haki yako kupata jibu ingawa unaweza usiamini lakini ni kweli wahendesha boda kama una malengo hela unapata nzuri ya kutosha tu. Inshu ipo kwenye familia na starehe ukiweza kuzibiti starehe ukabaki na familia ambayo ni muhimu kila kitu kinawezekana tu. Inshu ya kukopa mimi sio muumini wa kukopa maana unaweza kukopa hizo hela likatokea la kukulazimu kutumia hiyo hela au sawa ukanunua hiyo boda alafu ikapata tatizo. Hapo unakua na deni na tatizo la boda. Kitu kingine ni uharaka wa kua nayo ambao sikuwa nao ila nilikua na hamu ya kumiliki ambao nimeutimiza.
Hivyo sikua mzembe na Sikua na kipato cha zaidi ya elf 20 kwa siku. Zaidi nilipunguza starehe ambazo sio za lazima. Kama kula gegeni chakula cha elf mbili basi nakula nyumbani na familia maana ilikua sio mbali.
Asante sana, hongera. Nisamehe kama at some point nilikukwaza. Kuna kitu nimejifunza, big up bro!
 
Back
Top Bottom