Jinsi mshahara wangu wa kwanza ulivyonizuzua!

Jinsi mshahara wangu wa kwanza ulivyonizuzua!

TADPOLE

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2015
Posts
3,344
Reaction score
11,027
October 17,1997 Friday night

Ilikuwa kosa kubwa sana Mshahara wa Ajira yangu ya kwanza hapa DAR kuingia kwenye Account yangu wakati Weekend ndio inaanza.

Sikujiuliza mara mbili, nikatoa mshahara wote nikaujaza kwenye wallet ambayo sasa ilituna hadi ikikaa mfuko wa nyuma nakaa kiupande upande kama nina sindano za Masaa.

Nikaita TAXI
Mimi: "Dereva, kiwanja gani kina Burudani za kutosha?"
Dereva: "Bosi wangu umeshawahi kuingia Club Bilicanas?"
Mimi: "Sijawahi kabisa, kiwanja pekee nilichowahi kwenda ni Taifa tena na baba yangu kwenda kuangalia parade ya Uhuru, aisee hebu nipeleke hapo Bilicanas nikatoe Tongotongo!"

Dereva akaondoa gari mpaka Club Bilicanas!.
Club Bilicanas ni hatari, mataa yanamulika kama rangi za binzari. Usiku huu watu wote ni wazuri, wapo kina Beyonce kama mia hivi. Leo hata haka kashati kangu kalikofubaa kamepigwa Disco light kanaonekana kapya kabisa!

Nilikunywa pombe pale asikwambie mtu, watu wa mjini wamenizunguka eti naitwa Shaba Ranks!
"WAITER MPE KILA MTU ANACHOTAKA" hizo ndio kauli zangu na hata yule DJ alipokuwa ananirusha kwenye MIC, watu waliulizana sana hivi huyu jamaa atakuwa Ikulu nini? Fedha iliongea.

Basi nimekula mitungi mpaka saa 9 za usiku, that day nilipiga mpaka Cocktail ya Smirnoff na Malta! Kweli nilipagawa. Sasa nikawa nayumba lakini kuna Mwanamke nisiyemjua alikuwa anani-handle na care ya ajabu sana mule ndani.

Kuna muda wakati ameniegemea nilimsikia akiwaambia wenzake "Jamani this is my baby, naona kalewa nitamfikisha mpaka kwake nyie windeni vichwa vingine niachieni Mgodi wangu"

Sasa nilikokotana na yule mwanamke mpaka home, very intouch kama fungate na nilipofika home nikafungua mlango na funguo na kuingia ndani huku huyu mama mlezi wa leo akiwa amenilalia kifuani eti linadeka, teh!

Nikawasha taa, HAMAD!!! Kasheshe ni baada ya taa kuwaka aisee pale sebuleni alikuwepo Baba na Mama yangu mzazi wamekaa kwenye Masofa wametulia tuli wananitazama kwa makini. Macho yalinitoka Kingwendu kasingiziwa! Hili mama hapa Partner la Mahaba nimelisukuma kushoto linashangaa shangaa!

BABA : Karibu sana wanetu wapendwa; Kitorondo pita huku ukae hapo na huyo mwenzio (kwenye masofa).

Yaani kwa aibu kuu tukapita na kukaa, sura zote chini namtazama mama ameshika tama analia vibaya mno.

BABA : Enhe huyo ni nani?
MIMI: Huyu niii.....(yaani hata jina simjui nimetoa mimacho kweli, hapo ndio nikagundua mataa ya Club yanadanganya. Hapa ndani sasa tubelight inamulika mbaya, huyu dada kumbe ni Mbibi kabisa na amekoboka usoni kama kokoto za lami ya Strabag. Sura imekomaa kama kitako cha mtungi wa gesi ya ORYX. Siamini kama domo lile la Ugoro ndio liliomaliza pombe zangu pale Club, aisee kwa kweli hata Mama yangu pale sofani ni Mzuri mno! Nikainama chini kwa aibu!

BABA: Yaani kukusomesha kote huko ili uwe kijana Mstaarabu na Hazina ya Taifa ndio umegeuka na kuwa ZINZI na SHENZI kwa familia? Mimi baba yako miaka ya 70 wakati nimeanza Kazi kiwanda cha Tumbaku Mshahara wangu Wa kwanza wote alikula bibi yako na sikuonja hata senti, lakini Wewe Mpumbavu umekula na hili Bibi la Buguruni wakati mama yako aliyekuzaa na kukulea hata buku hajala, haya hebu haraka nionyeshe pesa iliyobaki!

Duh! kinoma noma kwa aibu nikatoa wallet yangu ambayo kwa sasa ilikuwa imekonda kama bahasha ya A4, Mama wee! kuna Tsh 1800/= wakati nilikuwa na 320,000/= nikainamisha sura kwa aibu.

Lile Guberi nalo lilipoona nimetoa Wallet imekauka kama Clips za Mihogo ndipo likaanza kuzingua pale pale. "We kinyago umenileta huku hela huna?! Utanipa changu leo Shenzi, mimi ndio Siwatu Mafirigisi, utanijua leo!(huku likinipiga Masingi).

BABA : Aisee Mama Kitorondo leo naua mwanao.

Sikumbuki kilichotokea zaidi ya kujikuta nipo hospital na tangu siku hiyo nikawa na respect na mshahara. Sikuwahi kuhonga tena. Nakumbuka pesa yangu ya kwanza baada ya tukio hilo aliila mama yangu na mke wangu bibie Rhoda Chechezamoto na ndio mtu pekee anayefaidi mshahara wangu hadi sasa😂
 
Uko vzur kwa kutunga. Sasa hapa wasanii wa bongo freva ( wa zaman ) ndipo pa kuchukulia story za kutungia mziki.

Wa ckuiz sihelewi wanatuimbiaga manini. Mara nibebe. Yan vurugu tupu. Hwana msaada wowote wa kuelimisha jamii mambi ya msing
 
Duh!720000 mkuu kwa mwaka huo,na malt ilikuwepo.you must be very rich now
 
Back
Top Bottom