Innocent Kirumbuyo
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 4,646
- 4,489
Hata kama mbingu zitafunuka na jopo la watakatifu likashuka au nikawekewa mtutu wa bunduki shingoni sitabatilisha kauli. Bado nitaendelea kusisitiza sikukusaliti sababu moyo wangu ulianza kuzika hisia nawewe wala shetani hastahili kubeba msalaba wa lawama, kwamba yeye ndiye alinitumbukiza kwenye lile shimo la dunia ya matamanio..
Ila nilikusaliti kwasababu sikuwa na uwezo wa kuidhibiti mawazo ya tamaa za mwili tunapokuwa mbali kwa miezi kadhaa na pia nilikuwa sijapevuka kifikra nijue jinsi ya kuiokoa akili inapokuwa imezamishwa kwenye kina cha bahari ya kulitamani tendo la uzinifu..
Lilipokuja swala la future person fikra zangu ulizifunga kwenye gereza lamoyo wako kila nilipowaza hitimisho la mahusiano yetu picha ukiwa ndani ya shera madhabahuni ilinijia kichwani nilikuwa na malengo yakukufanya uwe malkia kwenye ufalme wa moyo wangu..
Ndio maana siku ulipogundua namchepuko, nilikueleza kila kitu nikaamini ukweli ndio kristo pekee awezaye kuliokoa penzi letu lakini moyo wako ulikuwa mgumu, kupita moyo uliokuwa kwenye kifua cha marehemu farao nilipambana zaidi ya miezi 3 nikiomba utengue maamuzi ya kuhitimisha riwaya nzuri ya mahaba kati yetu.
Lakini jibu lako muda wote lilikuwa hili mishipa ya moyo wangu imegoma kusukuma tena damu za mapenzi juu yako INNO baada ya kunisaliti umeuyeyusha uaminfu wote ndani ya moyo wangu juu ya kiumbe aitwaye mwanaume hisipokuwa tu baba yangu.
Mungu atakupa msichana mwingine mzuri kuliko mimi INNO machozi yaliyokuwa yakimwagika kwenye paji la uso wangu mithili ya theruji iliyo juu ya kilele cha safu za mlima everest muda wote niliokuwa naomba usiniache bado hayakuweza kuulainisha moyo wako unifungulie geti la msamaha ili niingie tena kwenye chumbani cha mahaba nawewe.
Jinsi mapenzi yetu yalivyoingia ndani ya kaburi haikuwa hadithi yenye mwisho wa kuyapendezesha macho ya msomaji hata kalamu niliyokuwa naitumia kuandika kitabu cha hadithi yako nayo ilikuwa inamwaga wino wa machozi kuashiria kwamba inaguswa na msiba wa maumivu ambao ulikuwa umeuleta ndani ya moyo bila hiyari ya nafsi yangu .
Kuachana nawewe lile lilikuwa tukio la pili kuwahi kuniumiza katika maisha yangu baada ya tukio lakwanza, sikuniliyotazama mama yangu akifukiwa ndani ya shimo ambalo wanadamu wamelibatiza jina kaburi uku akiwa amelala kwenye mbao ziitwazo jeneza nakolea zikifanya mashindano ya kulirushia udongo jeneza lake .. Ili asionekane tena kwenye uso wa dunia...
Nyakati zingerudi nyuma, huenda saizi ningekuwa nakaribia kukuoa. ''